Kanisa Katoliki: Wassira atoe ushahidi wa Dk Willibrod Slaa kufukuzwa upadre

Viongozi wa ccm ni gharika sioni hata mmoja mkweli kwa hawa waliooko madarakani kutueleza kitu tukamuamini. Tuliahidiwa maisha bora kwa ari, kasi, na nguvu yako wapi?
Huyu mzee apumzike kwa amani.
 
Mbona Dr.Slaa alishajibu swali hili hapa JF? Msome hapao chini



icon1.png
Re: Dr.Slaa atajibu hoja juu ya Chadema na kueleza Sera za Chadema hapa JF


quote_icon.png
By mayenga
Swali kwako Dk Slaa,

Je ni kweli kwamba ulipokuwa Padre wa kanisa katolilki na ukiwa kama katibu mkuu wa baraza la maaskofu uliondolewa kwa ufisadi wa kutafuna michango ya ziara ya Papa Yohane Paulo wa pili?



Mayenga,


Jibu
Asante sana kwa maswali mazuri sana. Ningependa kujibu tu kwa ufupi kama ifuatavyo:

a) Kuwa nilipokuwa Padre na Katibu Mkuu wa Baraza la Maskofu Katoliki Tanzania (TEC) niliondolewa kwa Ufisadi na kutafuna michango ya Ziara ya Papa Yohane Paulo wa Pili. Ah, sijui nisemeje, anayetafuna michango na kufanya ufisadi hufikishwa kwanza mahakamani na akipatikana na hatia hufungwa gerezani kwa mujibu wa Sheria.

b) Kama hoja hii siyo ya Propaganda na kama mtoa hoja anaelewa Sheria za Kanisa Katoliki, au na wale wanaopigia debe hoja hii, basi ningelitegemea mambo kadhaa i) Wangeliweka hadharani "Hati"( Decree) ya kuondolewa kwa ufisadi. Kanisa Katoliki ina very elaborate procedure kwa mujibu wa Sheria zake, hivyo isingelimwondoa tu mtu aliyetafuna michango, na hata kumwondoa Upadre, ambao kama nilivyosema ni Sakramenti na haufutiki, isipokuwa kwa Taratibu elaborate za " Laiciztion", hati ambayo hutolewa na Papa peke yake kupitia Wizara ( Idara yake husika). Hati niliyonayo inayonirudishia hadhi ya Ulei (Laity) haitoe mahali popote process yoyote dhidi yangu, bali inajibu Maombi niliyowasilisha mwenyewe kwa mandishi yaliyosainiwa na mimi mwenyewe chini ya Kiapo, na kwa kuwa maombi yangu yalifikia viwango vinavyotakiwa nikapewa Decree husika.

c) Katika Kampeni ya 1995 ndiyo hoja kubwa iliyotumika na CCM na kwa bahati mbaya kila uchaguzi unapokuja hujaribu kufufua tena propaganda hiyo.

Hata hivyo, iwapo si propaganda, basi ningeliwategemea kwenye Jamvi hili wangeliweka angalau Indicators (viashiria) kuwa huyu bwana aliondolewa na Kanisa, aidha kwa document, au kwa kiashiria kuwa kuna chuki kati ya Dokta Slaa na Maaskofu au viongozi wa Kanisa Katoliki. Badala yake Dr. Slaa ameendelea ku enjoy uhusiano na Kanisa Katoliki katika ngazi zake zote, na hata siku wazee wa Karatu walipokuja kuniomba katika delegation kulikuwa na Mapadre wawili Fr. Reginald Barhe ( class mate wangu) na Fr. Dominick Rahhi aliyekuwa Parokia ya Karatu wakijua kuwa nikiwaona wenzangu, basi nitakubali kugombea. Nami kwa Historia yangu ndani ya CCM nikakubali na kuwaambia nitagombea kwa Tiket ya CCM kwa kuwa ndiyo chama nilichokijua hadi wakati huo. Hata ccm wenyewe katika hoja ya kuniengeua kuwa Mgombea kwa tiket ya CCM walieleza kuwa "nimesaidiwa na Kanisa Katoliki, japo hawakuweza kuonyesha uthibitisho wowote, wala sikuhojiwa kuhusu hoja hiyo) badala yake wakaamua kuniondoa kwa msingi wa "siyo mwenzetu".

Hivyo sina zaidi ya kusema hiyo ni propaganda isiyo na mshiko kwa kuwa Wananchi wa Karatu ndio walionifanyia Sherehe ya Upadre, ndio walioshiriki siku ya Upadre wangu, ndio walioniomba kugombea na kunifanya nishinde kura za maoni ndani ya CCM (kabla ya kuondolewa kwa mizengwe) na ndio walioendelea kunichagua katika chaguzi zote 3 toka 1995.

d) Kwa mtu yeyote mwenye kutaka ukweli, angelienda TEC na kuomba in confidence, Handing Over notes zangu kwa Katibu Mkuu aliyenifuata, Mhe. Methodius Kilaini, kama alikwazik na jambo lolote katika Handing over yangu kwa maana ya fedha zilizotafunwa au dosari nyingine yeyote ya kifisadi. kupenda kujenga proganda bila utafiti wa kina inaonyesha dhahiri kutokuwepo kwa dhamira safi.

Nadhani kwa ujumla maelezo haya yametoa picha kamili ambayo imeendelea kurudiwa mara kwa mara na wana CCM katika jitihada zao mbalimbali, hasa wana CCM wanaotoka nje ya Karatu, kwa kuwa Karatu hadi leo majina yangu ni Willy, Dr. na Padre kwa maana ya ukaribu wa watu wa Karatu na Dr. Slaa.





 
Hivi huyo Wassira (Mike Tyson) , si ni waziri katika serikali ya JK?
Huyu si ndio shoga mkubwa wa Warioba, aliyemnyang'anya ubunge hadi akaenda Upinzani?
Leo amesahau kwamba hata yeye aliwahi kuwa Mpinzani ananasimama na kukashifu wapinzani?

Hawa ndio viongozi tuliono leo!
Wasimamizi wa Kilimo Kwanza!
 
Aibu kubwa hii kwa ccm!
Kauli zote za kimasaburi!
1.Dr Slaa aliiba fedha za ziara ya Papa...................................................................Wassira
2.Vicent Nyerere si mtoto wa Familia ya Nyerere......................................................MkaaHapa
3.Mpeni kura Sioi ili mumfute machozi na aweze kulea Familia......................................Lusinde
4.Vicent Nyerere aende kwao Musoma, anatafuta nini huku kwa Wameru na Wamaasai....Olesendeka
 
amezoea vibaya na wataona haya tu mwisho wa siku. Midomo isiyo na gavana madhara yake ni makubwa. Hatari ya masuala yalotokea Rwanda miaka ya kati ya 90 yalianza kwa propaganda za chinichini na baadaye za wazi kabisa tena kwenye mikutano lakini mengi kati ya yalosemwa hayakuwa na ukweli. Mungu tunusuru na mabalaa wanayotaka kutuletea hawa ndugu zetu.
 
Kampeni za Arumeru mash zimeonyesha habari njema kwa wanaukombozi wa kweli wa nchi hii. Viongozi waote wa ccm waliopiga kampeni wakiongozwa na bwk wameonyesha kabisa kukerwa na sera za ccm za kuwadanganya wananchi kila kukicha na kuamua kuzitupilia mbali na badala yake wakaamua kumwaga sera za kuiua ccm!
Hongereni sana, saa zinakimbia sana kuelekea kifo cha ccm kuuawa na ccm.
 
Viongozi wa CCM wazidi kuaibika, baada ya Mkapa sasa ni zamu ya wasira ambapo Kanisa katoliki limekana kuwepo kwa ulaji fedha wakati wa ziara ya Papa na kumtaka Wasira atoe ushahidi............... Sinema zaendelea.

Kanisa Katoliki Lamshukia Wasira



MY TAKE:
Ni aina gani ya viongozi wa CCM tulionao kila wakati maneno yao yanakanushwa na kubainika kuwa ni uongo? Alianza Mkapa kudanganya sasa kafuata Wasira. Who is next??


Maandiko yote hayo, hakuna sehemu Kanisa limekanusha, linasema tu, "leta ushahidi".

Inanikumbusha Kikwete alipotakiwa kupeleka ushahidi wa kanisa kujihusisha na madawa ya kulevya, alipokamatwa mchungaji. Likakaa kimya.

Kanisa liseme nini kilimuondoa Slaa katika uongozi wa kanisa?
 
watu wa kizazi hiki kusikiliza viumbe wa stone age ni kupoteza rasilimali muda muhimu
 
Kwani Dr. Slaa ndio anagombea ubunge? Hivi ile orodha ya Mwembeyanga inaonesha nani ni mwizi? Hivi EPA, Kagoda, Power tiller, Radar, n.k. sio wizi huu? Na nani ni mwizi?!
 
Je,wassira,aliwaambia wana arumeru,nini kilifanya mahakama kuu mkoani mara ikafuta ubunge wake alioupata 1995 akiwa nccr mageuzi?
 
Dr. Slaa alisema kwamba kwa uongo huu wa mchana kama anaitambua nafasi yake ni bora ajiuzulu au Mkuu wake amwajibishe.
 
Watu wa Arumeru sasa waelewe ya kuwa CCM inawafanya wajinga. Mtu akija kwako na maelezo ya hadaa mwanzo mwisho ujue kakudharau na kukuona mjinga. Sasa waliyofanya Mkapa,Wassira na wenzao huko Arumeru ni dharau ya hali ya juu sana.
Adhabu yao ni nini? Wana wa Arumeru wanapaswa sasa hivi kufanya, wawaonyeshe CCM kuwa wamechukizwa na dharau hizo za kufanywa wajinga na CCM kwa kutoenda kuwasikiliza na hatimae kila mmoja siku ya uchaguzi pia kuhakikisha CCM haipati kura kabisa. Hilo litakuwa jibu sahihi na lakueleweka kwa waliowafanyia ubaradhuli huo.
 
Pengine katika maisha yangu ningependa baba yangu awe waziri, lkn si Wassira. Kulala bungeni, kuongea kwa jazba, kuongea uongo live. Ni aibu kuwa na mzazi muongo namna hii.

Kwanza katika hali ya kawaida, Wassira alitakiwa aombe radhi kwa uhuni aliousema. Kanisa sio chama mpk ajifanye msemaji wake.
 
Just imagine Waziri wa Serekali iliyopo madarakani anakurupuka na kuongea utumbo wa aina hii... Mola atunusuru na hili janga. Leo amejibiwa anasema kuwa hiyo sio habari... Mimi nashauri Dr. Slaa aende mahakamani adai mabillioni ya shilingi halafu tuone evidence ya huyu jamaa ninini.
 
Ni kweli siasa za kuchafuana hazina tija kwa jamii. Lakini napata wazo sasa kwamba kukashifiana kunakoshamiri leo hii ni muendelezo na ulipaji wa visasi kwa mwasisi wa SIASA ZA KASHFA hapa nchini WILBROUD SLAA pale alipoamua kuwakashfu watu tena kwa kuwataja majina kuwa ni mafisadi, wakati yeye akiguswa tu utasikia majibu "WENYE USHAHIDI na waende Mahakamni"! Majbu marahisi ambayo yanakuwa kama kejeli fulani huku Watanzania wakijua kabisa kwamba ni kodi zao ndizo anazichezea kama ambavyo amekuwa shujaa wa kuyakemea hayo Majukwaani.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom