Kanisa katoliki sumbawanga latolea ufafanuzi waumini waliotengwa

theophilius

Senior Member
Nov 19, 2010
150
54
Kanisa katoliki limetolea ufafanuzi suala la kutengwa kwa baadhi ya waumini wake kwa sababu zinzohusiana na matukio ya uchaguzi mkuu ulipita.

Leo majira ya saa 4 asubuhi wakati wa ibada ya misa, baada ya mahubiri, Paroko wa Sumbawanga mjini Pd. Deo, alitolea ufafanuzi suala la idadi ya baadhi ya waumini waliotengwa, makosa yaliyosababisha hatua hiyo, na wanachopaswa kufanywa ili kurudiswa ndani ya kundi la kanisa

Alisema taarifa kwamba waumini wapatao 400 wametengwa na kanisa hilo jimbo la sumbawanga zimepindishwa na kwamba idadi sahihi ya waliotengwa ni 27 na kati ya hao walio katika parokia hiyo ambayo ndiyo makao makuu ya jimbo hilo ni watano tu;

Wengine ambao hata hivyo hakutaja idadi yao wamewekewa pingamizi na hivyo kutoondolewa ndani ya kanisa japo wamesimamishiwa baadhi ya huduma hadi hapo watakapojieleza au kuomba msamaha.

Alifafanua kwamba kutengwa na kanisa ni adhabu ya juu ambayo hutolewa kwa makosa makubwa ambapo mhusika anakuwa amekihuka imani au nguzo za kanisa, na kwamba si kwa mara ya kwanza waumini wa kanisa hilo kupewa adhabu hiyo, na haihusu waumini pekee bali hata watawa na mapadre kulingana na uzito wa kosa.

Waumini hao, walikihuka mojawapo ya nguzo kuu tano za kanisa hilo ambayo ni kukejeli utatu mtakatifu pale walipowafananisha wagombea wao na utatu mtakatifu, kwamba mgombea wao wa uraisi ni mungu, wa ubunge ni mungu mwana na udiwani ni mungu roho, na kwamba walihusika na kosa hilo ama kwa kutamka wazi wazi, au kushabikia ukengeufu huo jambo ambalo alisema kwa kuhusika na kosa hilo husubiri kutengwa bali 'unakuwa umejitenga' automatically na kanisa hilo.

Makosa mengine ni kutukana na kukejeli viongozi wa kanisa ikiwa ni pamoja na ku-chakachua maubiri ya viongozi wa kanisa kwa kusambaza maneno ya uongo ambayo hayakusemwa na viongozi wa kanisa.

Wanadaiwa pia kukejeli msalaba kwa ama kushiriki kuuchoma moto au kushabikia kitendo hicho kiovu kwa kanisa na ukiristo.

Kwa hiyo alisema kanisa liliamua kutangaza kutengwa kwa waumini hao 27, kwa kuwa tayari walishajitenga pale walipohusika na makosa yanayowakabili.

Hivyo kulingana na kanuni za kanisa waumini hao hawaruhusiwi kushiriki ibada ya misa takatifu, iwe ile inayoendeswa kanisani au katika jumuhiya ndogo ndogo na kutopokea huduma yoyote ya kanisa ikiwa ni pamoja na huduma ya kuombewa wakati wa mazishi ikiwa watafariki wakiwa bado wametengwa.

Hata hivyo alisema waliowekewa pingamizi wanaruhusiwa kushiriki ibada ya misa japo wamesimamishwa kupokea huduma za sakramentu hadi hapo itakapogundulika hawakuhusika na makosa yanayowakabili au watakiri makosana na kuomba msamaha na kusamehewa.

Hadhabu kama hii nayo si ngeni katika kanisa kwani hata wahumuni wanaotelekeza familia zao au kushiriki mambo yaliyo kinyume na imani ya kanisa katoriki kama kushiriki ndoa za mitala hupewa adhabu kama hii.

Paroko huyo ameonya kuwa hakuna mamlaka yoyote ya kidunia inayoweza kuwaondolea hadhabu hiyo waumini hao na hivyo kuwataadharisha kuwa vikao wanavyofanya kutaka kuchukua hatua mbalimbali hazitawasaidia isipokuwa kutumia nguvu zilezile walizotumia walipokuwa wanakashifu kanisa kujirudi, kumrudia mungu na kuja mbele ya kanisa na waumini wenza kufanya malipizi na kuomba msamaa.

Wakati na kabla ya kipindi cha kampeni kanisa katoliki nchi nzima lilihusika katika kuwahamasisha waumini wake kujitokeza kupigia kura wagombea waadilifu, wasiokuwa mafisadi na wenye lengo na wanaoonekana kuwa na lengo la kuwaletea wananchi maendeleo.

Licha ya kuwa hakuna ushahidi wa maandishi ya kanisa au katika mahubiri ya viongozi wa kanisa ama madhabahuni au nje ya kanisa ambapo viongozi hao waliwataka waumini wao kutochagua wagombea wa dini zingine, baadhi ya viongozi walioona kuwa kampeni hiyo iko dhidi yayo kutokana na kutokuwa na sifa za uadilifu walianza kulalamika kwamba kanisa linaendesha kampeni ya udini.

Kutokana na mkanganyiko huo, hata baadhi ya waumini ama kwa kushawishiwa kwa rushwa au sababu nyingine, walijikuta katika mkumbo huo wa kupaka makosa kanisa ambali hata kwa chaguzi zilizopita limekuwa likishiriki kikamilifu kuandaa waumini wake katika wakati wa uchaguzi.

Sasa, kama ambavyo paroko huo amesisitiza dhamila yao (kanisa) itaendelea kuwa wazi bila kuogopa maneno ya viongozi wasiokuwa waadilifu na kuchukulia hatua waumini wake ambao nao wanajihusisha na hujuma hiyo dhidi ya kanisa, bila kujali kanisa litabaki na waumini wangapi japo, pamoja na hatua zilizochukuwa kanisa bado limejaa kama zamani.
 
Back
Top Bottom