Kanisa katoliki mmekubali kujichafua na pesa za Lowassa?

Hakuna justification yeyote kwa Kanisa Katoliki kumtumia EL.Tunajua huyu anatuhuma ambazo hajawahi kukanusha na wananchi tukiwemo waamini wa RC tunaamini zipo hoja za msingi.kama kanisa limeona hana hatia wamsafishe wao basi ili tujue sababu! Michango ni ya sisi waamini na kanisa ni letu sote sasa ni kwa maono gani kanisa kumtumia huyu kila jimbo tena mtu mwenye tuhuma zisizo na majibu? Kanisa halina watu wa kufanya hayo zaidi ya EL? Kama leo kanisa linasema haliwezi kuhukumu mtu wanasahau elimu waliyotupa kipindi cha uchaguzi? Zile sifa huyu El yupo? Sasa anaitwa kwenye harambee kama nani? Wanafikiri tumesahau kauli ya askofu kule mwanza kuhaidi kumsaidia El kujijenga? Kanisa limepotoka na tutawaambia ukweli!

Naomba nitajie tuhuma za Lowassa zinazomyima kwenda kanisani!
 
Naona EL anazidi kupata wafuasi wengi! Pesa bwana, inaweza kukusafisha ukawa mweupeee! Kanisa langu la RC sasa nalo sahani mmoja na mafisadi...upo wapi PENGO? Hivi mikwara yako yoote kwa mafisadi ni danganya toto?
Asikudanganye mtu, EL is evil.

Halafu ndugu yangu Isango uwe macho, huyu jamaa is capable of doing anything....anaweza kukuondoa kaka.....mbojo isii wang'u.
 
Pole sana ndugu yangu,

Anyway...Siku huyo EL atakapokuwa rais mtarudi tu hapa kuyakumbuka maneno yetu.

Sumaye alisema kuwa mtu anayetumia media kumaliza wenzake kabla ya kuingia ikulu, basi akiingia atatumia risasi za moto...Hamjayaona?

Haya bwana endeleeni na kampeni zenu.....Laiti madhara ya uchafu wenu yangeishia kwenu na yasituguse wengine!!

Lowassa amemchafua nani kwenye media? Wanayoyafanya Sitta et lal kwenye media kuzusha mambo ya hovyo unaona Sawa?
 
Si kweli hata kiduchu.

Kabla Richmond haijaleta hata mtambo mmoja hapo Dar sisi tulijua ni matapeli baada ya kufanya uchunguzi hapa USA na kujua ni wauza karatasi -Stationary.

Tulianza kupiga kelele za nguvu sana kuiambia serikali kwamba wameingia mkataba na matapeli. Muda si mrefu tukajua kwamba Lowassa kwa kutumia nafasi yake ya uwaziri mkuu alisimama kidete kuwatetea wezi hawa kwa vile so zima lilikuwa la kwake.

Kelele zetu na kutaja jina lake Lowassa na kumuhusisha moja kwa moja ndizo zilifanya Bunge liingilie kati na muda ulipo fika akaachia ngazi huku mashabiki na wapenzi wake wakishindwa kuamini macho na masikio yao.
Yeye anadai alifanywa Mbuzi wa kafara.
Ukweli ni kwamba wezi ndani ya seriakali ya CCMni wengi kama si wote, kwa vile so la Richmonduli ilikuwa ni janja yake na maji yalifika shingoni walimwambia hata ukiacha uwaziri mkuu usihofu, tutaendelea kuilipa kampuni yako kwani sisi ndo wahuni wenyewe wa CCM.

Kutajwa tajwa si hoja, hoja unatajwa vipi.
Kwa utaratibu uliopo na mazingira yaliyopo Lowassa anaweza kuwa Prezidenti bila hata kuteuliwa na CCM wala kupigiwa kula na mwananchi yeyote wa Tanzania.
Akishindwa kuipata nafasi hiyo Ataiiba.

Mambo Tanzania yameharibika sana kiasi cha sisi wananchi kushindwa kuelewa lililojema na lililo baya kwetu.
Ukifuata sheria na taratibu Tanzania utawalaza wanao njaa. Kuruka viunzi na kuvunja taratibu ndiyo Gold STD.
Taabu kwa wale ambao ofisi zao ziko tupu hazina cha kuiba, hao wanaipata joto ya jiwe.

Wengi wanaamini kwamba kurudisha utawala wa sheria ni kurudisha maendeleo nyuma.
Wasichojua ni vurugu na vurumai kubwa ya kiuchumi iliyo njiani kuja kuangamiza kila nguvu ya kuleta maedeleo Tanzania.
Siku inakuja ambayo watu watatoa uvivu na kusema liwalo na liwe.
Tukiona yale matukio ya Uarabuni tunadhani eti wale ni waarabu hapa kwetu haiwezi kutokea.
Tnajidanganya mchana kweupe.

Nimekaa ughaibuni miaka zaidi ya 15 kila baada ya miaka 2 narudi Bongo.
Kila nikirudi hali mbaya kuliko ile ya mwanzo lakini kwa aliye pale siku zote kwake ni kawaida.
Na yule ambaye utawala mbovu wa CCM umemnyea hudai kwamba in short time Tanzania itakuwa First world.
kila nikiranda na kupita mitaani kuongea na wenye nchi sioni unafuu.
hata maclass mate wangu walio na vyeo vikubwa serikalini nao wana wasiwasi na hali ya baadaye ya nchi yetu.
Wangependa kuona mtu muadilifu akiongoza nchi na utawala wa sheria ukirejehwa.

Lowassa kwa vile hana chembe ya aibu wala simile anatumia mwanya huo kujipenyeza kwa nguvu zake zote za giza ili awe Prez.

Tulimtaja sana jina lake hapa kwa maovu yake Kikanywa.
Leo tunamtaja tena kwa maovu eti tunaambiwa sasa ataula?
Akiula ni kwa sababu amebebwa na system inayo jiangalia yenyewe zaidi kuliko Watanzania na si sisi tunaosema uovu wake.

Sisi hatumbebi Lowassa waache mapadri wa Katoliki na wachungaji wa makanisa wambebe.

Roman Catholic Priests have nothing to lose in this because they dont have real kids and families. We do.


Kama CHADEMA wasipojipanga vizuri sioni ni kitu gani kitakachomzuia Lowasa kuwa Rais wa Tano wa nchi hii, sababu za msingi ni hizi hapa:
1. Kumekuwa na upumbavu wa kila siku kuliandika jina la Lowasa humu mitandaoni uku watu wakidhani wanazidi kumtia dosari kumbe bila kujuwa ndio wanampigia Promo ya uhakika.

2. Lowasa tayari ana sifa muhimu ya Rais ajaye, yaani lazima awe ni mkristo na hii ni karata muhimu ambayo Lowasa anaifahamu na kwa upande wa kanisa lake la Lutheran kazi imeshakamilika na ndio maana sasa anahamia upande wa kanisa katoliki.

3. Lowasa alishasema hakuna alilokuwa amelifanya ambalo halina baraka za JK, sasa ufisadi wa Lowasa hapa ni nini? kwa nini mnamuogopa JK? hapa watetezi wa Lowasa watasema anachukiwa kutokana na dini yake na kwa sababu anatoka kaskazini.

Ushauri: kama umpendi Lowasa ni busara zaidi kumpotezea tu kuliko kumuanzishia thread hapa JF, ni kwamba unazidi kumjenga zaidi kuliko kumbomoa. kwa CCM dhaifu ya JK hakuna wa kumzuiya Lowasa kuwa mgombea na akishinda ugombea ndani ya CCM Lowasa ni kwamba tumeumia hakuna chama chochote cha upinzani chenye jeuri ya kushindana na mtandao wa Lowasa.
 
Wewe ni msafi? Naona umekuwa Farisayo wa kizazi kipya?

Mie siyo msafi ila sibebi tuhuma zozote kwenye jamaa ambazo natakiwa kujisafisha au kusafishwa na mtu mwingine yeyote!

Kwani Nape keshawapa certificate of clearance kwamba Lowasa siyo gamba??

Babu DC!!
 
Kanisa huwakutanisha watakatifu na waovu. Bila shaka yaweza kuwa ndio njia ya lowasa kwenda kutubu na kuokoka kupitia changizo hilo
 
Lowassa ni muumini wa dini hiyo, kanisa si chombo cha uchunguzi kama ilivyo kwa PCCB iweje litoe hukumu kwa Lowassa wakati hakuna chombo cha uchunguzi kilichotangaza hukumu kwake Lowassa.
huu uzi umekaa kidaku sana,pengine angealikwa asiende usingeaacha kulipuka acha wivu wa kike...
 
yesu hakukaa na wenye dhambi ili wamsaidie(KUMLISHA) bali yeye yesu aliwasadia.
wewe u-nani mpaka umnyooshee mwenzako kidole?

This is a sign of desperation, kama Lowasa ni mwizi, alistahili kushtakiwa na serikali hii ya CCM na Jakaya.
Kama serikali hii imeshindwa kumshtaki, na ku-prove kwamba yeye ni mwivi, mnyonyaji na ndiye aliyesababisha maisha magumu kwa wizi wa fedha zetu.

Kama hili halijafanyika na serikali hii, then kwa nini mnataka taasisi zingine zimhukumu? kwanini nataka kanisa katiliki limhukumu?
Kwa nini hamjawahi kuliambia bunge liunde tume ya kumchunguza?.........Kwanini mwizi anakuwa mbunge?

TUACHE UNAFIKI!!
TUACHE KUMUOGOPA LOWASA, who is he?
KWamba akichangia kujenga kanisa basi atapewa kura? kwamba atakuwa rais?
Is that how you people elect your leaders?
 
Wazazi hivi mtu mzima EDO anapiga dili gani! na mapadre waacheni wavute mbona KKKT washa vuta sana wakiacha huo mpunga haita saidia kitu maana makanisa mengine yakisikia mapdre wamesusia fungu lao zitapigwa harambee za haraka haraka mtu mzima EDO aalikwe watu wavute;baada ya Katoliki ni zamu ya masheshe na msiwabanie kuvuta kwa zamu; Mzee mzima Kadinali Pengo ziba masikio halafu kaa mkao wa kula mtu mzima EDO ndo huyo ndani ya kanisa katoliki ,Pesa kitu ingine waseeeeeeeeeeeeeeee
 
Kama Lowassa angekuwa na makosa ambayo tunataka ahukumiwe basi asingekuwa Bunge, asingekuwa mjumbe wa NEC - CCM, asingekuwa mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya bunge. Lowassa angefunguliwa mashitaka tungejua kweli ana makosa.

hapa ni kulionea kanisa kwa kumtumia Lowassa wakati chama chake hakijathibitisha hilo ama kwa kumfungulia mashitaka au kumpokonya uanachama. Kwa nini tunataka kanisa ndilo limuadhibu Lowassa wakati kisiasa haijawekwa wazi kama ni fisadi/si muadilifu?

Kama si mwadilifu angeendelea kukitumikia chama chake?

Chama gani kifanye yote hayo? hiki cha akina Rostam? unaongea nini wewe? kajiuzuru kwa utapeli wao wanamwita PM mstaafu, Luhanjo naye na tuhuma zake leo katibu mkuu mstaafu sijui Jairo itakuwaje. CCM hakuna hayo unayoyadai. subiri uone kama akina Jairo watashtakiwa au nao huoni kama wanamakosa?
 
Lowassa ni muumini wa dini hiyo, kanisa si chombo cha uchunguzi kama ilivyo kwa PCCB iweje litoe hukumu kwa Lowassa wakati hakuna chombo cha uchunguzi kilichotangaza hukumu kwake Lowassa.

Watanzania ugonjwa wetu ni uleule ni wepesi kusahau. EL hajawahi kukiri aliiba rasilimali za watanzania na kila leo anakataa kuhusika huko na ufisadi. Niliwah kudokezwa kudokezwa kuhusu lowasa kuingia kanisa katoliki ilikuwa ngumu mwanzo lakn mwisho amefanikiwa. Kanisa langu limeingia mkenge wa mbio za urais za lowasa. Nawasikitia watz kwani jxa hakika dini sio tena mtetezi wa wanyonge kiroho na kimwili bali imefanywa njia za watu kutafuta uongoz tumekwisha. Kwa hili wakatoliki tumeprove failure, hatujashndwa kuchangia pesa za jasho letu lakni 2mewekwa pembeni mafisadi yatuchangie.
 
unajua nini hatupaswi kumuhukumu mtu bali mtoa hukumu ni mungu pekee, na hata kwenye biblia Yesu alisema ambaye hana dhambi na achukue jiwe mrushie huyu mama akuna aliyefanya hivyo unajua kwa nini? kwa sababu no one is perfect in this world, na pia Yesu aliandaa kalamu na wenye dhambi wale wanojihisi ni wasafi wakakasirika lakini Yesu akasema sikuja kuwaita watu wema bali wenye dhambi ili wapate kutubu.

Uko sahihi sister ila haina maana kuwa kwa kuwa sote ni wakosefu basi tusikemee maovu. Sidhani kama Jesus alimaanisha hilo!!!!
 
At least the churches are claiming the Billions which were and are still stolen from the Tanzanians every day.

Hainiingi akilini kuwa EL amefanya kazi serikalini na kupata pesa ya halali ambayo anagawa hadi leo hii. Pesa hii imetoka wapi na kwa nini inagaiwa kama karanga? Is there anything for free in this world?

Misikitini wamezubaa, hamtaki kuchangamkia hayo mapesa. Hii pesa ni ya watanzania, msione vibaya kudai pesa yenu. haya shauri yenu.

The Roman Catholics (kama kawaida yao) wameweza kuona outside the box. Siamini kama wanamapenzi ya dhati kwa bwana EL wakati wao ni wapinzani wakubwa na Ufisadi.

WITO kwa watz: Chukueni pesa zenu zilizoibiwa na mafisafi, lakini 2015 akili kichwani mwenu.
 
kama wewe ni muumini utakubaliana na mimi kuwa siku hizi kanisani masuala kuhusu fedha yanapewa kipaumbele sana kuliko kuhubiri neno la Mungu. Suala la kulifanya kanisa lijitegemeze limegeuka kuwa msingi wa imani. Michango ya fedha kwa ajili ya shughuli za kanisa ndicho kipaumbele, uanzishwajiw a miradi unachukua nafasi ya mahubiri nk.nk.nk
hivi unafikili nani ajenge kanisa? hiyo miradi wakina nani wananufaika nayo? kama shule, hospital, vyuo na benk nani anavitumia? wangapi wanawasomesha watoto wao kwenye hizi shule, vyuo? wangapi wanatibia kwenye hizo hospital? benk inawakopesha watu gani? huduma za kijamii unategemea serikali tu ndo zilete? kama ndo hvyo hembu fikilia kama serikali ingeachwa yenyewe kwenye huduma za kijamii tungekuwa wapi katika swala la elimu, huduma za afya na kadhalika? think twice hii yote ni kwa faida zetu sisi wenyewe.
michango huwa inafanyikaga baada ya ibada ndo utaratibu uliopo kwa sisi.
 
Lowassa amemchafua nani kwenye media? Wanayoyafanya Sitta et lal kwenye media kuzusha mambo ya hovyo unaona Sawa?

Maskini nchi yangu ya Tanzania,

Naona IDs za mwaka 2011 na 2012 kazini kuandaa njia na kutengeneza mapito ya bwana mkubwa kwa ajili ya kuingia Magogoni 2015!!

Anyway...Mwenye mapenzi haoni ingawa macho anayo!!

Babu DC!!
 
Kwa kawaida tunachagua mtu kuwa kiongozi;
Akitupikia wali
akigawa Shs 10,000.
Akitugawia Kofia Khanga na Tshirt za kijani
Akisema anakubalika na Wananchi
Pia tukijua kwamba ana pesa

Haki has a Price Taq.

If you pay the price we let you go free and we forget what you did.

You dont pay you belong to Segerea and Ukonga to lot forever and we will always remind you what you did.

CCM elites is just another gathering of thugs, can Thugs sue each other? Can we trust Thugs?

wewe u-nani mpaka umnyooshee mwenzako kidole?

This is a sign of desperation, kama Lowasa ni mwizi, alistahili kushtakiwa na serikali hii ya CCM na Jakaya.
Kama serikali hii imeshindwa kumshtaki, na ku-prove kwamba yeye ni mwivi, mnyonyaji na ndiye aliyesababisha maisha magumu kwa wizi wa fedha zetu.

Kama hili halijafanyika na serikali hii, then kwa nini mnataka taasisi zingine zimhukumu? kwanini nataka kanisa katiliki limhukumu?
Kwa nini hamjawahi kuliambia bunge liunde tume ya kumchunguza?.........Kwanini mwizi anakuwa mbunge?

TUACHE UNAFIKI!!
TUACHE KUMUOGOPA LOWASA, who is he?
KWamba akichangia kujenga kanisa basi atapewa kura? kwamba atakuwa rais?
Is that how you people elect your leaders?
 
Kanisa Katoriki limekosa msimamo, linakemea Ufisadi unaoendelea hapa nchini. Upande mwingine linakubali kupokea fedha kutoka kwa mafisadi wanatuhumiwa ikiwa mmoja wa watuhumiwa hao ni Bwana Lowasa. Wengine wanachangia kuwa ni moja ya toba inayotolewa, nataka kujua kama anatubu kimya anatoa sadaka na michango kwa Kamera na vipaza sauti. Naomba tuwe wakweli kwa hili, pale Yesu alipoingia kwa Yule Mtu mfupi Zakayo, Zakayo alitubu na kuahidi kuwa kwa yule aliyemdhurumu atamlipa mara 2. Je huyu alidhurumu wananchi wa nchi hii au alilidhurumu kanisa Katoriki, na ndio maana anafanya toba huko.
 
Back
Top Bottom