Kanichunia baada ya kumwambia namuhitaji awe mpenzi wangu.....

tindikalikali

JF-Expert Member
Jan 14, 2011
4,855
1,117
Ni rafiki yangu toka o'level, hatujawahi kwaruzana wala kupishana kauli. Kwa kipindi chote nimejitahidi kumuonesha kwa vitendo kwamba namjali na kumpenda. Miaka imepita tukiwa marafiki na nimeweza kumfahamu vizuri kitabia. Hivi majuzi niliamua kuvunja ukimya, na nimwandikia hivi "naomba unielewe ninachotaka kusema, sidhani kama itakuwa busara kwangu kumung'unya maneno, kwa kifupi nakuhitaji uwe mpenzi wangu, sisemi haya kwa bahati mbaya kwani najua nini nafanya na kumaanisha. Kumbuka ni ngumu kuukwepa ukweli, hata nisingesema leo basi ningesema kesho, naomba hekima na busara itawale maamuzi yako".....toka nimemtumia hiyo text kauchuna kimya wakati siyo tabia yake, sifikiri kama nimekosea kumwambia niliyomwambia, lakin nifanyeje ili nimlete katika mud yake ya mwanzo, maana nahisi hata urafik unaweza kwisha. Ushaur wenu wadau unahitajika.

UPDATED
Jamani nawashukuru wote mlionipa ushauri kunikosoa na kunipa zaidi. Tumepanga tukutane leo jioni, kitakachojiri nitawajuza. jumapili njema kwenu nyote
 
Acha woga wewe, mtoto wa kiume lazima ujiamini. Umefanya upumbavu kumtumia sms kqa issue muhimu kama hiyo, ulipaswa kutafuta muda wa kutosha umtoe outing ya nguvu mnaenda sehemu tulivu then mnakaa na kuongea vizuri mkiwa mmetulia sehemu isiyo na bughudha then unaongea naye vizuri kwa kujiamini huku ukimtazama usoni.
Ktk hayo maongezi yenu jitahidi sana kumhakikishia juu ya mustakabali wa maisha yake ya baadaye ktk uhusiano wenu, hayo mambo kwao ni muhimu sana.
Kuwa kwake kimya kusikutishe, huenda amepatwa na mshtuko coz haamini kama uko serious ama lah, na pia njia ulotumia ni ya kitoto zaidi inamfanya akuone kuwa hauko serious. Kama unaweza mpigie simu.
 
mkuu unayoyasema inawezekana yana ukweli ndani yake, lakini nikimpigia simu si inawezekana nikawa naendeleza unaoitwa utoto?
 
mkuu unayoyasema inawezekana yana ukweli ndani yake, lakini nikimpigia simu si inawezekana nikawa naendeleza unaoitwa utoto?
Hamna unajua wanawake wanapenda sana kupigiwa simu. Hiyo itakusaidia kujua yuko kwenye mudi gani, kuliko kukaa unajiuliza maswali mengi na kudhani umeharibu kumbe amefurahia ujumbe. Halafu ujue watoto wa kike kamwe hawazoi kutongozwa, lazima atakuwa na aibu tu labda ile mikahaba iloshindikano. Ila ukipiga mtake hali tu na wala usiulizie chochote kuhusu ujumbe labda mpaka aanze yeye.

Ila ni muhimu sana ukatafuta siku nzuri mkae pamoja kwa utulivu umseleze bayana tena bila kupepesa kope.
 
mkuu unayoyasema inawezekana yana ukweli ndani yake, lakini nikimpigia simu si inawezekana nikawa naendeleza unaoitwa utoto?

Yah!Itaonekana kweli unaendeleza utoto maana plan uliyoanza nayo ilikuwa ya kitoto pia!Usingetumia sms method.Sasa bado hujapoteza point.Nenda na plan B,Mtafute umvae face to face!Naujitutumue kweli,,halafu ujipe moyo kwamba hata akikataa hamna kesi na wala hawezi kukuchapa.GO AHEAD!
 
Next time usirudie kuandika andika text ni tabia za kitoto na kutokomaa vizuri,wasichana wengi ni wajanja sana na wanahitaji mtu mwenye msimamo na msimamo unauonyesha wapi,unauonyesha kwenye mazungumzo ya ana kw ana na si kutumiana msg,umuhimu wa ana kwa ana unamsoma mwenzako(body language) anavyobadilika kulingana na unaloongea kwa wakati huo na kama muud inabadilika unajua namna ya kui-control mapema....anyway tusiandike mengi nafasi unayo mtafute upange mashambulizi vizuri uso kwa uso jino kwa jino wajanja wanafanya hivo...
 
Back
Top Bottom