Kaniahidi upendo anafunga ndoa leo

Ulikuwa unampenda lakini bado hukuwa na uwamuzi.

Sasa mwenzako ameoa unaumia roho. Basi tena kama unampenda kwa dhati usimuharibie ndoa yake. Piga moyo konde uendelee mbele na maisha yako.
 
kapata kitu mnato kama supa glue ....we wa nini sasa...kwanza hilo jina nalo linachangia sana kuchelewa kuolewa we hujui tu..jiite jacky au monica au sheila uone kama vigeregere havijarindima asa ivi

na wewe umpendiiiii monikaaa sio ndio wale wale aijiite hayo mengine mwaya tena jana nikamwombea kweli nikamwota usiku amekumbatiwa na msungu mnene ana hela kweliiiiiii huku jf members tunanywesha gin n tonic bill kwa muzeeee
 
Ms
anatafuta mke wa pili utamweza nikuunganishie ...ten percent atanilipa mungu ikiita ndoa nakusikiliza
 
Huyu jamaa bado ananipenda na me pia nampenda sas mapenzi yetu si yanaweza athir ndoa yake?

We unajali ndoa yake?
Basi achana na huko unakodai una'mpenda' maana ungekua unampenda usingemwambia akaoe mwingine. Kinachokusumbua sasa hivi ni wivu tu kwa huyo aliyeolewa na kinachomsumbua huyo jamaa ni tamaa.

Na wewe tafuta wako kila mtu aende na njia zake.
 
Huyu jamaa bado ananipenda na me pia nampenda sas mapenzi yetu si yanaweza athir ndoa yake?
angekupenda asingeoa mrembo mwingine, anakudanganya tu ngoja apewe mapenzi motomoto na laazizi nyongo mlalia ini uone kama atahangaika nawewe.
 
ulikuwa unampenda lakini bado hukuwa na uwamuzi.

Sasa mwenzako ameoa unaumia roho. Basi tena kama unampenda kwa dhati usimuharibie ndoa yake. Piga moyo konde uendelee mbele na maisha yako.

mpwa hayo majina ayajui kupiga moyo yanakupiga wewe ulieamua kumuacha unafikiri amelogwa akakimbilia huko..ukimuuliza mke jina lake utasikia malafyale mwambulukutu,,mwantunu,mwasimbekele..oohh
 
Kuna makuzi mengine balaa sana...hizi familia nyingine bwana zinatisha.Yaani yeye kwake kitendo cha kuwa na uhusiano mume wa mtu sio ishu kabisa,kinachomsumbua ni atapataje wasaa wa kujivinjari nae.Uso mkavu.

Kuna binti mmoja nimeambiwa juzi kaenda Moshi na boyfriend wake (mume wa mtu) kwenye msiba wa baba yake mdogo halafu akalala na mshikaji guest jirani halafu asubuhi jamaa anakuja kuoga home kwao.So sad.

Nakushauri badilika tu.
 
we unajali ndoa yake?
Basi achana na huko unakodai una'mpenda' maana ungekua unampenda usingemwambia akaoe mwingine. Kinachokusumbua sasa hivi ni wivu tu kwa huyo aliyeolewa na kinachomsumbua huyo jamaa ni tamaa.

Na wewe tafuta wako kila mtu aende na njia zake.



lizzy kama ajakuelewa basi aende kujiuza pale afrika sana atapata bwana .,,mbona wanaume wa kuoa wako wengi tu na wana upendo wa agape jamani nini dada kakupa huyo mume wa mtu sasahivi embu msikilize binti mwezio basi hapo juu umuelewe atii...
 
10 Farao alipokaribia, Waisraeli wakainua macho yao wakawaona Wamisri, wakija nyuma yao. Wakashikwa na hofu wakamlilia BWANA. 11Wakamwambia Mose, "Je, ni kwamba hayakuweko makaburi huko Misri hata umetuleta tufe huku jangwani?Umetufanyia nini kututoa Misri? 12 Hatukukuambia tulipokuwa huko Misri, tuache tuwatumikie Wamisri? Ingekuwa vema zaidi kwetu kuwatumikia Wamisri kuliko kufa jangwani!'' 13 Mose akawajibu Waisraeli, "Msiogope. Simameni imara, nanyi mtauona wokovu BWANA atakaowapatia leo. Hao Wamisri mnaowaona leo kamwe hamtawaona tena. 14 BWANA atawapigania ninyi, nanyi mnatakiwa
kutulia tu.'' 15 Ndipo BWANA akamwambia Mose, "Kwa nini wewe unanililia? Waambie Waisraeli waendelee mbele. Kutoka 14: 10-15

Mankaa pole sana, naelewa nafasi uliyopo kwa sasa kwani upo NEUTRAL ZONE huelewi hatima ya baadae. Kwanza naomba uelewe kwamba huu wakati unaopitia ni sehemu ya maisha, wote huwa tunajikuta tupo NEUTRAL ZONE katika mazingira tofauti. Nimekukumbusha kisa hiki cha wana wa Israeli walipokuwa wanatoka misri kwenda nchi ya ahadi kuna wakati walijikuta wako NEUTRAL ZONE, hawakuelewa hatima yao ya baadae. Lakini Mungu aliwaambie WASONGE MBELE japokuwa mbele yao kuna bahari. Naamini hata wewe unaona bahari mbele yako lakini nami nakushauri KUSONGA MBELE kwani kanani yako iko mbele.

Ukweli ni kwamba huyo mtu hakuwa na mapenzi ya kweli kwako yaani hamkuwa na BALANCED LOVE nae alitambua hilo kwamba wewe unampenda zaidi kuliko yeye anavyokupenda inategemeana na tofauti zenu ambazo yeye aliona hawezi kuchukuliana nazo. Hii hutokea kwa wengi sio wewe tu. Ikitokea kwamba mapenzi hayako balanced ni kwamba mmoja wenu anakuwa mtumwa kwa mwingine (kuburuzana), hivyo basi isingekuwa tofauti na wana waisraeli walipotamani kuendelea kubaki utumwani.

MANKAA, naomba utambue kwamba wewe ni wa dhamani sana hapa duniani, hakuna mwingine kama wewe "YOU ARE ONLY ONE ON THIS WORLD" na kuna wengi duniani wanatamani kukutana na wewe. Hivyo basi nakushauri kuwa mtulivu katika kipindi hiki na kuweza kuchukua maamuzi sahihi ambayo hayataleta machungu katika maisha yako yote, naelewa wakati huu unapitia machungu, lakini haya ni ya muda mfupi sana ukilinganishi wakati wako mwingine wa maisha. Ilishawahi kutokea kwa binti mmoja habari kama hii, alikuwa akipatiwa ushauri na mama yangu katika kumfariji; lakini baadae yule binti alikuja kuolewa na mwanaume kutoka nje ya nchi (specifically alikuja kwa ajili yake) alimfahamu vipi, sikutaka kujua zaidi.

Vilevile naomba ufahamu kwamba bado kuna wengi wa dhamani ambao wanakupenda na kukujali wakiwemo wazazi, ndugu, jamaa na marafiki bila kusahau jamii yote ya JF, we real love you....!!!!

Nakushauri kutumia KANUNI YA SIKU 21:

http://www2.fiu.edu/~oea/InsightsFall2004/online_library/articles/daily%20activities%20to%20help%20change%20habits.htm

Watafiti waligundua kwamba mwanadamu anao uwezo wa kubadili tabia yeyote ile ndani ya siku 21, hivyo basi ndani ya siku 21 utamsahau kabisa na maisha yataendelea kama kawaida. Kwa sasa nakushauri ujitahidi kutokukutana nae ndani ya siku hizi 21, naelewa ni ngumu lakini ukiweka dhamira ya kweli yawezekana.

Kumbuka kwamba mahusiano yako na mwenza wako yana uhusiano mkubwa sana na maisha yako ya baadae; hivyo basi huu ndiyo wakati wako wa kujenga au kubomoa. Namshukuru Mungu kwa aliowapa maono ya kuanzisha JF kwani naamini kupitia jukwaa hili tunajifunza mengi.

Nakutakia kila la kheri!!!
 
upuuuzi mtupu.
Kongosho,wala sio upuuzi aisee,i have seen it again and again,mwanaume anaoa/mwanamke anaolewa na mtu ambaye for some reasons (economic/religious?)rohoni wala hayumo na baada ya harusi anaendelea kama kawa na mpenzi wake wa zamani,very common na sishangai kwa uzi huu,remember triangle ya lady diana,parker bowles na prince charles?
 
lizzy kama ajakuelewa basi aende kujiuza pale afrika sana atapata bwana .,,mbona wanaume wa kuoa wako wengi tu na wana upendo wa agape jamani nini dada kakupa huyo mume wa mtu sasahivi embu msikilize binti mwezio basi hapo juu umuelewe atii...
akajiuze afrika sana? Why?
 
Huyu jamaa bado ananipenda na me pia nampenda sas mapenzi yetu si yanaweza athir ndoa yake?
acha ujinga wewe, angekupenda angeoa mwingine wakati wewe bado upo available? angekupenda angebadili hivyo vitabia ambavyo wewe huvipendi ili ukubali kuolewa naye. tafakari, chukua hatua...................... utabaki kuwa kipozeo tu akiamua kubadilisha mboga.....................
 
Subiri Mr. Perfect aje akuoe wakati miaka inasonga mbele na mwenzako ameshapiga hatua ya ziada.

Tutajaribu kukuundia ambaye hana hivyo vitabia usivyovipenda.
 
Usijaribu kumruhusu u fanye naye yale mambo yetu,kwasababu tayari kashamilikiwa kihalali na mwanamke mwenzio,kwahyo utakachomfanyia mwenzio kumbuka na wewe utakujafanyiwa hvyo wakati wako ukifika..kwahyo kuwa muangalifu.
 
Manka,kwa vyovyote mabadiliko yanaweza kuanzia kwako...mwenzio keishaamua moja,hakuna sababu ya kuiweka ndoa yake shakani...umekiri mwenyewe nafasi ilikua yako ukatia kiburi...pole...vuta vumbi move on...maisha hayajakoma!
 
sina ushauri wowote wa kukupatia zaidi ya kukupa pole.btw inaonekana umetokea fb maana hata kiswahili chako kinaonyesha hivyo.next time tuandikie kiswahili kizuri cha kueleweka na sio kile cha fb kwa mfano sasa huandikwa xaxa.
Haahaaa napenda sana binadamu anaejali uzalendo na asili yake, watu wanavuruga lugha yao na kuwa kama Kirumi
 
Pole...maelezo yako yanajichanganya...kama hukutaka akuoe unasikitika nn sasa? Move on hunachako hapo tena
 
Back
Top Bottom