Kangi Lugola Alphaxard, Mhe

Kintiku

JF-Expert Member
Feb 3, 2011
617
319
Wadau,
Mhe. huyo amekuwa mojawapo ya wabunge ambao wamekuwa wazungumzaji sana ndani na nje ya Bunge.

Nimejaribu sana kufuatilia michango yake kuelewa msimamo wake hasa lakini nimeshindwa kumuelewa anasimamia nini?.

Naona yeye ni kama Zantel- Twanga kokote....nahisi pia alishakuwa kuwa au ni Mchungaji wa makanisa ya Kipentecoste maana flow yake ni kama ya mtu ambaye huwa anasimama madhabahuni kuhubiri.

Halafu nikiangalia katika Televisheni huwa nashindwa kuelewa huwa amesimama au sijui anakaaje anapochangia michango yake. Lugola wewe ni vuguvugu Bwana atakutapika
 
Wadau,
Mhe. huyo amekuwa mojawapo ya wabunge ambao wamekuwa wazungumzaji sana ndani na nje ya Bunge. NImejaribu sana kufuatilia michango yake kuelewa msimamo wake hasa lakini nimeshindwa kumuelewa anasimamia nini?. Naona yeye ni kama Zantel- Twanga kokote....nahisi pia alshakuwa kuwa au ni Mchungaji wa makanisa ya Kipentecoste maana flow yake ni kama ya mtu ambaye huwa anasimama madhabahuni kuhubiri. Halafu nikiangalia katika Televisheni huwa nashindwa kuelewa huwa amesimama au sijui anakaaje anapochangia michango yake. Lugola wewe ni vuguvugu Bwana atakutapika

La kutapikwa na bwana tumwachie bwana mwenyewe.ila lugola ni miongoni mwa wabunge wachache wazuri walioko ccm.
 
nilitaka kugombea jimbo la mwibara,lakni hakuna haja tayari jembe letu kangi ndege lugola anatosha kutuongoza tena kwa mwaka 2015 kama atakwenda na moto huo huo,
 
Kangi Lugola a.k.a Nati ya Kirumi namkubali siyo mnafiki.Ni mojawapo ya majembe ya mkoa wa Mara. Mkoa wa Mara kuna vichwa eti eh!
 
Kangi Lugola mimi kabla sija pata kumfahamu nilifili bonge la mzalendo, kumbe jamaa ni mganga njaa tu, kelele za bure hana uzalendo wowote ndani yake!.
 
Hata mie katika awamu yake ya kwanza bungeni nilidhani ni pande la mpapule, mzalendo wa kweli hasa alipokuwa akiingia bungeni na marundo ya vitabu, magazeti, akivaa kininja n.k

Katika awamu hii ndio nimegundua Lugora ni bonge la bomu na mpenda mlungula wa nguvu.

Nashangaa sana kuendelea kuhudhuria vikao vya bunge, si wamfukuze au kanuni za bunge na sheria za kawaida zinasemaje kuhusu mbunge kufikishwa mahakamani.
 
Hii Kashfa ya Juzi ya Kuomba Rushwa imempunguzia haiba yake Kisiasa.
 
Lugola na Lisu, Msigwa ,Mbowe, Msigwa kazi kupayuka , hawana chembe ya uzalendo ,kwao kupayuka ndio jambo la maana sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom