'KANGA MOKO' yatikisa BUNGENI!

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,610
Mchezo wa kanga moja maarufu kama kanga moko, umewatisha wabunge. Hali hiyo ilitokea bungeni jana wakati wabunge hao walipokuwa wakichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa mwaka wa fedha 2012/2013.

Akichangia ktk mjadala huo, Mbunge wa Viti Maalum, Dk. Getrude Lwakatare (CCM), alisema kuna haja Serikali kuangalia mwenendo wa muziki huo, kwa kuwa unakiuka maadili ya Kibongo.

"Hebu ngoja nizungumzie huu muziki wa kanga moja, huu ni mchezo mbaya sana, tena kanga inalowanishwa na maji halafu binti anaivaa.

"Baada ya kuivaa anaanza kufanya manenguo, hivi itakuwaje kama mwenye umbo nene akiivaa na kunengua, ni aibu tupu hapa.

"Kwa hiyo, naomba Serikali iangalie namna ya kudhibiti hii kanga moja kwa sababu inachezwa kinyume cha maadili," alisema Dk. Lwakatare.

Kwa upande wa Mbunge wa Viti Maalum, Mwanamrisho Taratibu Abama (CHADEMA)...alisema muziki huo unafaa kupigwa marufuku kwa kuwa unawadhalilishwa wachezaji.

"Huu muziki wa kanga moja haufai, nasikia mara nyingine wanauita kanga moko, huu ni udhalilishaji lazima upigwe marufuku.

"Pamoja na kwamba unakiuka maadili ya Kitanzania, wanaume wanaupenda sana kwa sababu kila unapochezwa wanajaa ukumbini, Serikali iupige marufuku huu," alisema Abama.

IMG_8495.jpg

IMG_8470.jpg

kanga_moja_chini.jpg_480_480_0_64000_0_1_0.jpg
 
​hebu niweke video yake

haya hiyo hapo video. hayo ndio mambo ya kanga moko ambay serikali inataka kuyapiga marufuku

[video=youtube_share;WY7NqyYiKZk]http://youtu.be/WY7NqyYiKZk[/video]
 
Akichangia ktk mjadala huo, Mbunge wa Viti Maalum, Dk. Getrude Lwakatare (CCM), alisema kuna haja Serikali kuangalia mwenendo wa muziki huo, kwa kuwa unakiuka maadili ya Kibongo.

"Hebu ngoja nizungumzie huu muziki wa kanga moja, huu ni mchezo mbaya sana, tena kanga inalowanishwa na maji halafu binti anaivaa.

"Baada ya kuivaa anaanza kufanya manenguo, hivi itakuwaje kama mwenye umbo nene akiivaa na kunengua, ni aibu tupu hapa.

"Kwa hiyo, naomba Serikali iangalie namna ya kudhibiti hii kanga moja kwa sababu inachezwa kinyume cha maadili," alisema Dk. Lwakatare.

Kwa upande wa Mbunge wa Viti Maalum, Mwanamrisho Taratibu Abama (CHADEMA)...alisema muziki huo unafaa kupigwa marufuku kwa kuwa unawadhalilishwa wachezaji.

"Huu muziki wa kanga moja haufai, nasikia mara nyingine wanauita kanga moko, huu ni udhalilishaji lazima upigwe marufuku.

"Pamoja na kwamba unakiuka maadili ya Kitanzania, wanaume wanaupenda sana kwa sababu kila unapochezwa wanajaa ukumbini, Serikali iupige marufuku huu," alisema Abama.

Kwanza maadili ya Kitanzania ndiyo yapi hayo?

Mbona hayo madanguro bubu aka ma 'guest houses' hawayashikii bango wakati ukweli wa mambo kwa asilimia kubwa sana yanatumika kama sehemu za watu kwenda kufanya ngono? Tena yamejaa kwenye sehemu za makazi ya watu....

Hayo ma gesti hayakiuki maadili ya Kitanzania? Hivi nyie wabunge mliteuliwa kwenda huko bungeni kuongea pumba?

Mnapokea mishahara ya bure kabisa. Hamstahili kulipwa hata shilingi moja. Na ingekuwa ni juu yangu mimi ningefutilia mbali huo ubunge wa aina yenu.

Yaani mnasimama bungeni mnajadili khanga moko ndembendembe laki si pesa milioni chenji? Halafu mnadiriki kusema khanga moko zipigwe marufuku?

Msitake kutuharibia watu starehe zetu bana, ebo!!!
 
Kuna mambo mengi sana ambayo yatakiwa kufutwa zaidi ya hiyo kanga moko,wamesahau night club zoote wadada wanavaa nusu uchi hapo je?madanguro je,?wacheza show wa bendi zetu je?hakuna cha kinyume na utamadiuni,waje na sera mbadala kupambana na utandawazi wa dunia kijiji ,kuanzia mashindano urembo hadi vipindi vya TV....majumba kulala wageni na uthibiti wake,Bar na Grosary zilizojaa kila mtaa na muda wa kuuuza na kunywa pombe....yako mengi sana!!waje na hoja mbadala wa mfumo mzima
 
....wanaacha kujadili mambo ya maana wanajadili kanga moko. wawaache kwani ndo mtaji wao wenyewe....
 
inaonekana waheshimiwa nao memba wa kuangalia kanga moko ndembendembe laki si pesa million..... huh huh huh huh
 
Kila mtu na starehe zake.. Watuachie starehe zetu!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Kanga moko na bongo fleva zote zipigwe marufuku Tanzania, ila kuhusu maadili ya Tanzania hilo sijuwi. lnachekesha kuona ni wabunge wanawake tu wanaopiga kelele kina baba kimyaaaa wanawaza watapata wapi starehe kama hii. Wabunge wetu hawa, basi tu!
 
khaaaaaaaa kumbe na ww ni muumin wa dini hii?

Kwanza maadili ya Kitanzania ndiyo yapi hayo?

Mbona hayo madanguro bubu aka ma 'guest houses' hawayashikii bango wakati ukweli wa mambo kwa asilimia kubwa sana yanatumika kama sehemu za watu kwenda kufanya ngono? Tena yamejaa kwenye sehemu za makazi ya watu....

Hayo ma gesti hayakiuki maadili ya Kitanzania? Hivi nyie wabunge mliteuliwa kwenda huko bungeni kuongea pumba?

Mnapokea mishahara ya bure kabisa. Hamstahili kulipwa hata shilingi moja. Na ingekuwa ni juu yangu mimi ningefutilia mbali huo ubunge wa aina yenu.

Yaani mnasimama bungeni mnajadili khanga moko ndembendembe laki si pesa milioni chenji? Halafu mnadiriki kusema khanga moko zipigwe marufuku?

Msitake kutuharibia watu starehe zetu bana, ebo!!!
 
Kuna mambo mengi sana ambayo yatakiwa kufutwa zaidi ya hiyo kanga moko,wamesahau night club zoote wadada wanavaa nusu uchi hapo je?madanguro je,?wacheza show wa bendi zetu je?hakuna cha kinyume na utamadiuni,waje na sera mbadala kupambana na utandawazi wa dunia kijiji ,kuanzia mashindano urembo hadi vipindi vya TV....majumba kulala wageni na uthibiti wake,Bar na Grosary zilizojaa kila mtaa na muda wa kuuuza na kunywa pombe....yako mengi sana!!waje na hoja mbadala wa mfumo mzima
Nakubaliana nawe asilimia moja (100%).
 
Kanga moko na bongo
fleva zote zipigwe marufuku Tanzania, ila kuhusu maadili ya Tanzania
hilo sijuwi. lnachekesha kuona ni wabunge wanawake tu wanaopiga kelele
kina baba kimyaaaa wanawaza watapata wapi starehe kama hii. Wabunge wetu
hawa, basi tu!

kuna mbunge mwanamke aliwahi kuonyesha hofu ya wao 'kukosa soko' kama wanaume wataruhusiwa kuoana!
 
Kila mtu na starehe zake.. Watuachie starehe zetu!
Ni kweli...na starehe za wabunge wetu ni hizi (kanga moko, ufuska, ulevi, kujirusha, utoro bungeni) na kutochangia mada muhimu kwenye vikao vya bunge. Sitashangaa akija mbunge na hoja ya kutaka kanga moko iwe vazi la taifa kwa kina mama. Ah Tanzania, nakusikitikia mama yangu!
 
Wavivu wa kufikiri,akili zao znaweza ku deal na vitu kama hivyo na wala sio mambo ya msingi. Simpleton represantatives!
 
Safi sana na imetulia.

Kelele za mpita njia,
Hazimtoi pangoni mwenyewe,
Wapi kanga moko huchezwa?
kama zi kwenye majumba ya starehe!

Huchezwa hadharani?
Au mbele ya watoto mashuleni,
Huchezwa stendi ya basi Ubungo?
Palipo wote na watoto pia?

Huko Kilabuni wacha ichezwe,
Acheni wanengue mpaka wakatike,
mikono mfukoni iwekwe,
mijengo isimame imara,
atazamaye kaipenda mwenyewe,
Kiingilio si bure ni ngawira,
Kanga moko wenyewe twaipenda,
Kama huipendi waifwatiani?

Mbunge alalama sauti juu apaza,
eti ipigwe mafuruku nchini kote,
mbona ujinga na ununda bungeni,
mwashindwa piga marufuku???
Matusi ruksa bungeni,
Mwatukana mpendwavyo,
Mangapi ya kuudhi bungeni twayasikia,
Lakini pingu mwaitia Kanga Moko?

Mwaendeleza ujinga wenu bungeni,
michango mwashindwa toa kwa kiswahili,
Ujumbe haufiki mpaka neno libane matusi,
mmekomaa mashavu ndimi za chuma,
Midomo yenu yanena ukengeufu,
Vichwa vyenu vimejaa mvi
Vichwani akili fupi kaa za makinda,
Bunge gani la misonyo na utusitusi JUU.

Msiiguse wala msiiseme vibaya kanga moko,
kanga moko siye yatuburudisha,
jadilini hoja maridhawa bungeni,
kanga moko ni upepo wapita,
Msiitaje kanga moko Bungeni,
Suala la Kanga Moko liko Mahakamani.

Msikomae na ulimbukeni komaeni na;
Uhaba wa maji safi,
Uovyo wa maji taka,
Wizi na ubadhirifu serikalini,
Ufisadi rushwa na ufuska,
foleni za magari ubungo,
Ndege mbovu TBS nyanya,
Mauti Kuzama kwa meli,
Mabilioni Iba ficha Uswiss,
CCM sheria chini wao JUU,
Watiwa mfukuko na mabilionea,
Rais kiguu na njia,
Muhimbili ife sie na APOLO,
Ritz! Milionea,
Kapata wapi kinda yule pochi????
Haya basi mgawie kidogo Willie!!!
 
Msalagambwe utarogwa. Wewe hujuwi wasifu wa wabunge wa Tanzania kuwa ni kuroga ili uogopwe? Haya yote uliyoyazungumza ni ya kweli na bahati mbaya watanzania hatupendi kuambiwa ukweli kwani ukiwa mkweli unaonekana adui. Mi nakuombea tu hawa wabunge wasije kuku Ulimboka (umafia aliowafanyiwa Dr. Ulimboka).
 
Last edited by a moderator:
Lakini jamani hivi hii kanga moko moko mambo ndembe ndembe laki si pesa million chenji unawakosesha wabunge amani???? kwanini wasikoseshwe amani ya hela ya NSSF wanayoikopa kwetu kiulazima? kwanini wasikoseshwe amani na mazingira mabaya watu tunayofanyia kazi?

hivi hii wizara ina mambo mangapi ya kudiscuss? hebu angalia mavipindi yaliyopo kwenye tv na redio yanayopata coverage kubwa may be tz yote yanaachwa tena yasiyokuwa na maadili istoshe gesti za uchochoroni ndo usiseme huku uswazi halafu wanaongelea haya yanayoonekana hapa dar tu tena kwa watu wachache sana ambao hawazidi hata 100 kwa mara moja?
 
Back
Top Bottom