kanga kwa wanaume yana sasa matusi

Hadi najisikia maumivu moyoni ninapo ona wa Tanzania wenzangu wanapo iuza haki yao na vizazi vyao kwa kipande ya kanga tena iliyo andikwa HALI MPYA YA MAUMIVU ZAIDI ,NGUVU MPYA ZA KUWAIBIA ZAIDI, NA KASI MPYA YA MANYANYASO ZAIDI ZAIDI.Watanzania wenzangu mlio wavumilivu na shida,Manyanyaso na dhuluma tunayo tendewa na hawa manyang'au tulio dhani ni msaada kwetu tusikate tamaa tuendelee kuipigania haki yetu hata ikitugharimu uhai lakini siku moja itafika na naamini watakosa pori la kujificha.
 
Tena hata ukiangalia sura ya Nape inadhihirisha dharau kwao kabisa yani dah........
 
afu mbona kama anawadolishia,sio kwamba anawagawia?unakumbuka ukiwa na pipi yako afu washkaji wanangojea uwamegee kwa meno?maskini wababa wa watu...
 
hawa wote ni std seven leaver nina uhakik KAMA MTU ALIYEMALIZA FORM IV shule za kata hawezi kukaa hapo
hence: i love shule za kata
 
mama watoto hajapata nguo mpya tokea uchaguzi upite kwanini nisiende kugombania kanga za ccm.
 
Yaani wanagombania khanga.....na jamaa anawatazama kwa dharau!!
 
Yaani wanagombania khanga.....na jamaa anawatazama kwa dharau!!

na nyuma yake kuna land cruiser v8 matata sana ambalo thamani yake inazidi thamani ya majengo yote katika eneo lao vikiwemo shule na zahanati (kama wanayo) na pengine thamani yake inazidi jumla ya fedha zote halmashauri yao inazopata toka serilkalini kwa ajili ya maendeleo!!

whaaat a joke!!!
 
afu mbona kama anawadolishia,sio kwamba anawagawia?unakumbuka ukiwa na pipi yako afu washkaji wanangojea uwamegee kwa meno?maskini wababa wa watu...


Hahahahahahaaaaa King'ast hapo kwenye blue umenikumbusha mbali sana........kuna jamaaa yangu yupo wizara flani nyeti nilie soma nae tangu primary niliwahi kumdorishia ndizi ya kuchoma na parachichi aisee ilimuuma sana hadi leo iktokea nahitaji kitu flani lazima anikumbushie ile issue vile nilimfanyia hahahahha......sio mbaya wacha tu hawa wanao dorishiwa labda na wao siku moja watawadorishia wanao wadorishia .......
 
Hii ndio inayotuvurungia kura kila mwaka! watu wanadanganywa na sare za chama.....CCM wame-capitalise kwenye umaskini wa watanzania...huu umaskini ni CCM made for CCM survival!
 
Back
Top Bottom