Kandoro asitisha wizi wa gari la serikali

huu nchezo hupo na pale polisi , magari yanayokamatwa na magendo, au kesi za wizi wanayaweka muda mreku alafu gari la milion 20 wanajiuzia laki nane bila kutangaza mnada
 
yaweza kuwa kazi nzuri ya JF nadhani! Safari inaendelea
Hongera mkuu kwa kazi nzuri iliyookoa mali iliyonunuliwa kwa kodi wa walalahoi. wazalendo na wenye uchungu na nchi hii tufichue vitendo vyote viovu vinavyofanywa na mafisadi kuhujumu mali ya umma
 
yaweza kuwa kazi nzuri ya JF nadhani! Safari inaendelea

ni sahihi, kwani katika kulalamika alisema ameandikwa hadi mtandaoni. ukienda kwenye google ukaandika kandoro, inakuja thread ile ilyotoa taarifa za njama zake hizo za kutaka kuwahujumu walipa kodi
 
Nimepita pale ofini kwao leo, nimelikuta limepaki. Nitalilinda na nawaomba wenzangu mliopo Mwanza, tulilinde wote.
Ni ujumbe kutoka kwa mwanajavi akinitaarifu kuliona gari.
 
Kazi nzuri ntamaholo..

kazi nzuri pia kwa michango yako iliyofanikisha kuliokoa gari hilo. tuendelea kulinda mali za walipakodi. halafu ile tabia ya bosi kwenda kulewa na gari la serikali inanikera kweli
 
huu nchezo hupo na pale polisi , magari yanayokamatwa na magendo, au kesi za wizi wanayaweka muda mreku alafu gari la milion 20 wanajiuzia laki nane bila kutangaza mnada

Kuna mdau yupo kikosini alinidokeza kuwa kuna aliyewahi kuwa RPC arusha, alijiuzia kitu wanaita found property, gari landcruiser kwa Tsh. 50,000/=. baada ya watu kulalama, alichofanyiwa ilikuwa kuhamishwa na kupelekwa mkoa mwingine lakini bado aliendelea kumiliki gari lile. upuuzi kama huu tusiuvumilie kwani kuna hospitali ngapi zinakosa gari la kubeba wagonjwa? found property zikipelekwa hospitalini zitasaidia wangapi?

tuwe macho wandugu kuhkikisha mambo haya tunayatokomeza
 
kwa mjibu wa marxist school of thout, kila kitu ndani ya jamii, ni matokea ya jamii husika. this simply means, ikiwa kuna wizi wa mali za umma, basi jamii hiyo imeridhia, ikiwa kuna ujambazi, basi jamii hiyo imeridhia, ikiwa kuna maendeleo basi jamii hiyo imeridhia. hakuna kipatikanacho kiko nje ya social interaction, jamii ikisema ndiyo, itakuwa ndiyo, na ikisema hapana, itakuwa hapana
 
Back
Top Bottom