Kampuni za Blandina Nyoni zinavyofanya ufisadi serikalini

Kumbe Duka la Mariedo ni la huyu mama? Mie nilikuwa najua ni la Mke wa Kimei boss wa CRDB...
 
Naifanyia kazi tetesi moja ya kutisha, inamuhusisha mama Nyoni na Rushwa kubwa ya kutoa kazi katika Kampuni ya SOFT-TECH Akiwa mhusabu mkuu wa Serikali na tenda za kupeleka semana zake za wahasibu pale Paradise hotel Bagamoyo kwa kamisheni maalumu. Na kwamba alitoa tenda moja ya Kununua majenereta ya Hazina makao makuu na Hazina ndogo zote Tanzania bara baada ya dili kuisha alikatiwa fungu na kufungiwa jenereta moja la kisasa kabisa pale kwake, nipo kwenye finishing ikikamilika hii ripoti nitaitoa kavukavu hapa Jamvini ila niombeeni si mnajua kuna kuuawa? maana watu wa kanda za huko wanatuma radi tuu imfikie mlengwa.


Bila kusahau kuwa alikuwa Board Chairman wa DAWASCO, alisababisha ulaji na uzembe wa utendaji wa DAWASCO mnaouona sasa.......did I mention aliyokuwa anataka kuyafanya kule jeshini ?
 
Huwezi kutuamnisha kwa kutaja majina tu, hilo sahau.

Tumeona madudu ya blandina yanaanikwa, tumeona madudu ya yule jamaa yenu wa TBS yameanikwa, hayo ndio tunataka, sio majina tu. Kuwa makini kidogo.
Jamaa yao kina nani?
 
Turudi kwenye mjadala jamani maana dada wa Kariakoo alitaka kutuyumbisha Kidogo. Haya madudu anayoyafanya Blandina na wenzake wengi walio serikalini ni kwa sababu sisi wenyewe tulikubali walioko serikalini wafanye biashara na serikali kwa kuondoa Azimio la Arusha.

Unategemea kitatokea nini kama Famasia wa Mkoa anamiliki duka la dawa mitaani, au Mhandisi wa TANROAD kumiliki Kampuni ya Kandarasi ya ujenzi wa Barabara? Hizi ni gharama tunazolipa kwa ujinga wetu wa kulikataa Azimio la Arusha
 
mama blandina .... mbona atajuta .. acha nibaki msomaji .

Mkiambiwa hii nchi imekwisha mnakuja na hoja zisizo na mbele wala nyuma. Mara ooooh! anaonewa kwa sababu ya imani yake, ooooh kwa sababu ya kabila lake, ..., ooooh! Ufisadi hauna dini, kabila, wala nini!
 
Kweli bwana!! Huyu mama ana tamaa sana kama Adam Malima na mwenzake Abasi Kandoro kwa kusaidiwa na Hawa Mavurugu!! Ukimjua mbwa jina lake hakusumbui.


Mkuu KG utamwacha atoke kwenye motion halafu ataharibu mtiririko wa habari !
 
Autopilot anataja hayo madudu yanayofanyika ingawa si kwa undani lakini at least anaweka majina ya maduka na kazi walizopewa. Wewe unaweka majina ya watu tu, huoni kuwa hiyo ni ufinyu wa akili na unaonekana hukijui ukisemacho?

Weka jina na kosa alilofanya tuchambuwe kama kweli au si kweli. Usitujaze ujinga.

Mimi nikisema kama Mbowe, kama Slaa kama Zitto, Jee, hapo nimetenda haki au naunganisha tu kuwapakazia , inabidi niseme, kama Mbowe amefanya hiki na haki na hiki. Hata wanaomtetea badala ya kuja na hoja watakuja na matusi kwani wanakuwa hawana cha kukitetea. Kuwa makini kidogo.

FF,

Ili kuondoa any misinformed perceptions, ulionaje pale JK alipowaita wafanyakazi MBAYUWAYU? Na je, unaonaje utendaji na performance yake kama kiongozi wa nchi kuhusiana na economic management?
 
Mama Nyoni aliwahi kusema hahitaji kufanya kazi serikalini ili kuwa na pesa

sasa anafanya nini huko serikalini?

Kule JWTZ alijaribu lakini si mnajua serikali ya wale jamaa ilimshinda so ikabidi atulize ball

Hana tofauti sana na IMELDA MARCOS

imelda_marcos_intro.jpg



 
Mkiambiwa hii nchi imekwisha mnakuja na hoja zisizo na mbele wala nyuma. Mara ooooh! anaonewa kwa sababu ya imani yake, ooooh kwa sababu ya kabila lake, ..., ooooh! Ufisadi hauna dini, kabila, wala nini!
Hakuna mtu aliyemtetea Blandina kwamba anaonewa kwa sababu ya dini yake, bali watu tulikuwa tuna deal na FF kwa sababu tunamjua na lazima ujue wengine huwa tunatumia Bold ya Kijani kwenye kuonyesha msisitizo kwenye hoja za FF kwa sababu tunajua anatumiwa na CCM kueneza udini na si Uislam.
 
Jana ulimzungumzia Juma pinto kule kwingine na nikakujibu na leo sina haja ya kusema mengi

In short JUMA PINTO HANA UNDUGU WOWOTE NA MKUU WALA MAMA SALMA!

Mindhali hii thread ni ya kuwekana sawa nashauri uanzishe thread inayomhusu Juma Pinto kisha tumwage mboga Chadema Style

Kwanza Juma Pinto hana undugu wowote na Mama Salma. Hivi unajua huyo Pinto alisoma wapi na elimu yake aliishia wapi?

Pinto alikuwa mwandishi wa habari za michezo wa kuunganisha kuunganisha na 1995 ndipo akajidai kutaka kumjua kwa saana JK na kuwa na mahasira Dodoma baada ya JK kufanyiwa uhuni na Nyerere na Pinto alikuwa mmoja kati ya waandishi waliokuwa na hasira kuwa wakirudi Dar wanakuja kumwaga radhi mpaka JK akamwambia aache munkar na baada ya pale akaulizwa anataka nini akaomba apewe safari ya kwenda Ulaya ambako alioza (hakuwahi kupata passport)

Pinto hana undugu hata wa kwa mbali na Mama Salma sema mambo yake ya kujipendekeza ndio yamemfikisha hapo alipo na ukitaka habari zake mtafute hasim wake na patna wake wa zamani jamaa mwenye TZUK anaitwa abuu faraji

Hivi inawezekana vipi ndugu yake mama Salma ajitangazie BARICK kuwa ni mfanyakazi wa Ikulu wakati sio? Au huna habari alifoji letterhead ya ikulu kwenda kuwatisha wale jamaa wampe tenda?

Ingia google kisha search Juma Pinto utapata habari zake zote. Angekuwa ndugu yake mama angekuwa anadaiwa na akina Chale Mtawali magari aliyochukua pale?

Pinto alisaidiwa kuanzisha gazeti la Jambo leo lakini majibu yake yakawa ni kumtukana JK kila kukuchavyo kwenye vichwa vya habari za gazeti lake.

Kazi kwenda kuwapakazia wenzie aonekana ana maana wakati ukweli hana maana hata kidogo.


Ukitaka kufaidi anzisha thread ya Pinto tukupe vitu.


Ukweli mtupu!
 
CORRECTION;
Maths: Vitanda 3,000 kwa bei ya 1,000,000 kwa kila kitanda,
Otherwise upo ok,....

lakini pia tusisahu kuwa:
Idara za procurements katika irada za wizara zote anazopita blandina huwa anakuwa influence ya ajabu

Mfano wizara ya Afya, wizara ambayo inatakiwa na matumizi makini ya fedha lakini huyu mama hakuona taabu kupitisha bajeti ya ya zaidi ya bilioni 6 kwa ajili ya maonyesho ya 77 na 88

Mfano mdogo mmoja ni STAFF UNIFORMS ambazo mama Nyoni alilazimisha wizra ya afya kuwanunulia washiriki wapatao 1,000 suti jozi 6,ambazo thamani yake ni BILIONI 3..................!

GUESS WHO SUPPLIES HIZO NGUO?

Yap you guessed it.......ni lile dula la MARIEDO BOUTIQUE ambao wao wanachokifanya ni kununua nguo kutoka China lakini wanaandika lebo za UK.

Jiulizeni kwa nini Mariedo hawakuwahi ku supply suti BENKI KUUU enzi za LIUMBA?


Sasa kumbukeni kuwa hizo BILIONI 3 zingenunua vitanda vingapi kwenye hospitali za wilaya ngapi Tanzania?

jibu ni rahisi.....tungeweza kununua vitanda 3,000 kwa bei ya shilingi 1,000 kwa kila kitanda! shemeji,wifi,wake ,mama,shangazi zetu wasingekuwa wanajifungulia chini sakafuni kama ilivyo sana lakini Blandina hayo yooote kwake sio muhimu...muhim MARIEDO wapewe tenda za staff Uniforms!

btw

I just wanna point out kuwa duka la huyu mama la Mariedo pamoja na kusupply vitu FEKI lakini pia tazameni mikataba yake ni endelevu kwenye kila idara ya serikali so unakuta Mariedo lina contract ya miaka mpaka 3 hata kama wanaleta bidhaa ambazo ni hafifu!

Now Mzee Luhanjo hayupo tena na as it is MTOTO WA MKULIMA hawezi kuendelea kumlinda huyu mama....at some point itabidi ajiuzulu nyadhifa zote inluding kule WAMA ambako aliingizwa na PHILEMON LUHANJO.................!

In short waingereza wanasema kuwa HER POSITION IS UNTENABLE
 
''alipokuwa board chair wa nssf uniform zikanunuliwa mariedo''chanzo kimebainisha

Hapa sasa jamani ndio mnajidhalilisha, kweli mama Nyoni aliwahi kuwa mwenyekiti wa NSSF lakini kazi ya kununua uniform haifanywi na board of Directors hufanywa na management!! Sasa was Blandina part of the management? No, she was no, mtu wa kuulizwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Nssf ambae nadhani wakati huo alikuwa Ramadhani Dau kwaninii walinunua uniform hukowalikonunua!!Kudhihilisha majungu yenu mnasema kuwa huyo Mariedo ana kontract endelevu katika idara zote serikalini , Je huko kwenye hizo idara zote serikalini mama Nyoni ndio anahusika na manunuzi?
 
aisee mambo makubwa haya -- hivi intelligensia na Takukuru yetu inaanzia wapi na kuishia wapi? nahisi intelligensia ni ile ya kunusa maandamano ya CUF na CDM yanafanyika lini, yataanzia wapi na yataishia wapi na kina nani wanayaongoza. nanukuu kwa hisani ya FaizaFoxy "na hawa wachache wenye tamaa kupitiliza ndiyo wanaofanya nchi hii isitawalike"

leo hii tunamchambua huyu mama ila wapo wengi sana wanaoitafuna inji hii bila huruma hata kidogo; naunga mkono mgomo wa madaktari asilimia mia.
 
Hapa sasa jamani ndio mnajidhalilisha, kweli mama Nyoni aliwahi kuwa mwenyekiti wa NSSF lakini kazi ya kununua uniform haifanywi na board of Directors hufanywa na management!! Sasa was Blandina part of the management? No, she was no, mtu wa kuulizwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Nssf ambae nadhani wakati huo alikuwa Ramadhani Dau kwaninii walinunua uniform huko walikonunua!!

Aisee wewe uko dunia gani? ati Mwenyekiti wa bodi hafanyi nini?
 
Pia kuna tender moja imepitishwa kihuni huni ya kufunga gps tracking system kwenye gari za wizara... utekelezaji wake unasuasua hadi leo, kampuni inayohusika na ufungaji wa hivyo vifaa ndugu (kaka) yake Jakaya na Salma (inasemekana Shangazi) wanauhusiano nayo
 
Back
Top Bottom