Kampuni ya TIGO inaelekea kufa!!??

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213
Kampuni ya simu za mkononi ya tiGO ambayo imejizolea wateja wengi kuanzia mwaka 2005 baada ya kuanza kushusha garama za kupiga simu iko katika hali mbaya na huenda muda wowote ikafa na kuacha kampuni za voda na zain/airtel zikiendelea kutamba. Taarifa zaidi zinaeleza kua kampuni hiyo (tiGO) ambayo imetamba kwa muda mrefu na kuzipiga bao kampuni nyingine za simu za mkononi hapa nchini kwa kua na garama nafuu zaidi kwa kipindi kirefu hivi sasa imeshindwa kuendana na kasi ya ajabu ya kampuni mbili za vodacom na airtel ambazo nazo zimeamua kupunguza garama na kusababisha wateja wengi waliokua ama wameasi au wamepunguza kasi kutumia mitandao hiyo kurejea kundini kwa kishindo na kuanza kuuponda mtandao wa tigo. Inasemekana kampuni ya voda imekua ikikusanya fungu kubwa la pesa kupitia huduma ya M-PESA ambayo imesambaa zaidi vijijini tofauti na huduma ya tigo pesa ambayo iko zaidi maeneo ya mijini. Kitendo cha voda kuzindua huduma ya kupiga simu kwa garama ya nusu shilingi kwa sekunde kuanzia dakika ya kwanza kwa muda wa masaa 24 kumeishtua kampuni ya tigo ambayo inatoa huduma ya kupiga simu kwa nusu shilingi baada ya dakika ya kwanza tena kwa muda wa masaa 20. Wadau wa mitaani wanasema nusu shilingi ya tigo ina mipaka mingi kwa sababu inambana mtu kujiachia kuanzia mida ya sa 11jioni hadi sa 4 usiku vilevile haithamini mazungumzo ambayo hayazidi dakika moja. Wanasema tigo imeshagundua kwamba imeanza kukimbiwa na wateja ndo maa imebandika mabango yanayosomeka "usiache mbachao kwa msaala upitao". Taarifa nyingine zisizo rasmi zinadai tigo wameuza minara mingi na hivi sasa wanatumia garama nyingi sana kukodi minara hiyo kitu ambacho kitaharakisha kuanguka kwa tiGO... Source: habari za street...
 
Hii ni habari mbaya kwa mtu yeyote anayetumia mtandao wowote, na si mteja wa tigo tu...The thing is, ushindani ni nyenzo muhimu sana katika biashara ndani ya soko huria, maana unasaidia ku'regulate huduma in many ways, ukiachilia mbali bei.
I personally dislike this!...Mungu saidia isiwe hivyo!
 
mmh kaka matangazo yanalipiwa...umeilipa jf?
una strateg nzuri ya matangazo ...gud!!!!!!
wamekulipa sh ngap
 
Kampuni ya simu za mkononi ya tiGO ambayo imejizolea wateja wengi kuanzia mwaka 2005 baada ya kuanza kushusha garama za kupiga simu iko katika hali mbaya na huenda muda wowote ikafa na kuacha kampuni za voda na zain/airtel zikiendelea kutamba. Taarifa zaidi zinaeleza kua kampuni hiyo (tiGO) ambayo imetamba kwa muda mrefu na kuzipiga bao kampuni nyingine za simu za mkononi hapa nchini kwa kua na garama nafuu zaidi kwa kipindi kirefu hivi sasa imeshindwa kuendana na kasi ya ajabu ya kampuni mbili za vodacom na airtel ambazo nazo zimeamua kupunguza garama na kusababisha wateja wengi waliokua ama wameasi au wamepunguza kasi kutumia mitandao hiyo kurejea kundini kwa kishindo na kuanza kuuponda mtandao wa tigo. Inasemekana kampuni ya voda imekua ikikusanya fungu kubwa la pesa kupitia huduma ya M-PESA ambayo imesambaa zaidi vijijini tofauti na huduma ya tigo pesa ambayo iko zaidi maeneo ya mijini. Kitendo cha voda kuzindua huduma ya kupiga simu kwa garama ya nusu shilingi kwa sekunde kuanzia dakika ya kwanza kwa muda wa masaa 24 kumeishtua kampuni ya tigo ambayo inatoa huduma ya kupiga simu kwa nusu shilingi baada ya dakika ya kwanza tena kwa muda wa masaa 20. Wadau wa mitaani wanasema nusu shilingi ya tigo ina mipaka mingi kwa sababu inambana mtu kujiachia kuanzia mida ya sa 11jioni hadi sa 4 usiku vilevile haithamini mazungumzo ambayo hayazidi dakika moja. Wanasema tigo imeshagundua kwamba imeanza kukimbiwa na wateja ndo maa imebandika mabango yanayosomeka "usiache mbachao kwa msaala upitao". Taarifa nyingine zisizo rasmi zinadai tigo wameuza minara mingi na hivi sasa wanatumia garama nyingi sana kukodi minara hiyo kitu ambacho kitaharakisha kuanguka kwa tiGO... Source: habari za street...

du habari serious kama hii unasema source :street...ilinishtua kidogo kwani kuondoa tigo sokoni kutafanya soko liwe monopolised na Voda....voda siku zote wamekuwa wakituvuna ..sana...na pesa yao wanaitumia kudhamini mafisadi.......tigo wamekuwa wakitumia low cost strategy .....kwa muda mrefu toka enzi za tritel na wameweza kudumu sokoni.....baada ya ushindani mkubwa voda ambao wamekuwa wamejibaza kwenye high rates..wameanza kuwafuata tigo huku chini...kibiashara wanaoumia ni voda kwani wanalazimisha kupunguza gharama wakati bado overheads zao zipo juu...hii maana yake ni kuwa hawataweza kudumu muda mrefu kucharge rate ndogo unless wanafanya tentative cost cuttings.......na itabidi wafanye hivyo kwani tigo inaongozwa na wa ASIA ambao ni champions wa low cost..sasa airtel nao imechukuliwa na indians so they will go for downsizing ..and to what i know tayari wameanza...,zantel pia wao ni low cost...so mtaelewa kuwa voda wanajaribu kuiga low cost...

Issue ya kukodi minara ..ni moja ya mbinu ya cost saving....wanaita OUTSOURCE STRATEGY...yaani inasaidia kampuni ku downsize interms of humanresource..wanabaki wafanyakazi wachache amabo wana deal na utawala,mauzo na mikakati.....makampuni yote makubwa yanafanya hivyo .....so kwa kampuni kama ya simu itakachofanya ni ku outsource towers operations,outsource call centres[CRM management]..,outsource some of marketing [mnaona makampuni yanapewa tenda za kufanya roadshows]....concentrate sales operations to wholesalers / distributors[ie planetel,alphatel etc]...basicallly makampuni haya yanabaki na watu muhimu tu kama administration,finance na network management.
 
It does not matter

- Tritel ilikufa
- MIC (T) aka mobitel ilikufa ikamrithisha mjukuu wake tIGO
- Celtel ilikufa na mtoto wake ZAIN kafa juzi juzi baada ya kumzaa Airtel
- Vodacom ipo ICU mrith wake ni vodafone

e.t.c:::

Life goes on - MAFISADI @ work!
 
Jamani TIGO haijafa na wala haijauzwa, MIC (T) Ltd ndio jina la kampuni mpaka muda huu.
kilichofanyika ni kubadili tu 'brand name' na si kampuni, nina influence za ndani juu ya hii kampuni hivyo si kweli kwamba eti tigo imeuzwa.

Kumekuwa na ushindani saana wa kisoko kwa kampuni za simu hapa nchini, kwa sababu zain & voda zimeuzwa...hivyo ili kulinda imani kwa wateja wao 'kisoko' ni lazima watumie propagations fulani katika kulinda maslahi fulani,,,bali pia kupunguza bei za kulonga kwa KUSHURUTISHWA na tigo.

NB: Kampuni za simu zilishindwa kukubaliana tangu awali katika suala la kushusha bei za simu tangu awali, ambapo iliyokuwa vodacom & zain waligoma kushusha bei ilhali zantel & tigo wakakubali bei zishushwe...what happened then..
Tigo walishusha bei na zantel wakashusha bei...ikapelekea wengine soko kuwa gumu, wameshurutishwa mpaka nao wameamua washushe bei.
AT LAST NI LAZIMA KAMPUNI ZA SIMU ZITAKAA MEZA MOJA NA KUWA NA GHARAMA SAWIA KWANI HAWATOKUWA NA FAIDA SOKONI...hii ni furaha kwa watumiaji.

Nawasilisha.
 
tigo wanatakiwa wajiimarishe mpaka vijijini,hata huku KUMSENGA kijijini tunahitaji huduma bora za tigo_OTHERWISE TIGO HAIWEZI KUFA,ni washindani halisi wa kibiashara.
 
Phillimone mikael naona umeamua kutumia lugha kitaalamu i gues wewe nph mwajiriwa wa tigo. Voda kupitia huduma ya M-PESA ambayo imesambaa hasa maeneo ya vijijini ambako hakuna benk wanapata faida kubwa sana ambayo inawaweyesha kumudu gharama rahisi. Usiache mbachao kwa msaala upitao.
 
Back
Top Bottom