Kampuni ya Six Telecom yafungiwa kwa kuisababishia Serikali hasara ya Sh. Bilioni 8

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Serikali ya Tanzania, Imeifungia Kampuni ya Six telecom kwa kuisababishia serikali hasara ya Billioni nane. Vilevile Kampuni hiyo, imekiuka taratibu za leseni za mawasiliano.

=================

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TRCA imeifungia kampuni Six Telecom kuendesha shughuli zake kwa tuhuma za kuikosesha Serikali mapato zaidi ya Shilingi Bilioni 7.6 kwa kutoza chini ya kiwango simu zinazotoka nje.

Ilikuwa majira ya saa nne asubuhi wakati maafisa wa TCRA wakiandamana na maafisa wa Polisi walipofika kwenye ofisi hizo na kuwakuta wafanyakazi wakiendelea na Shughuli zao na kuwataka kutoa Ushirikiano, ambapo afisa aliyekuwapo alionyesha kutotii agizo hilo mara moja.

Hata hivyo Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo Rashid Shamte ambaye aliingia kwa kujiamini katika ofisi hiyo alihoji uhalali wa maafisa hao kufika ofisini kwale kabla ya kuelezwa madhumuni na tuhuma zinazoikabili ofisi hiyo na hali ilikuwa hivi…

Baada ya kubanwa na maafisa hao na kutishiwa kutiwa pingu, hatimaye Mkurugenzi Mkuu huyo alikubali kutoa ushirikiano kwa maafisa hao huku akiendelea kulalamikia hatua hiyo.

Maafisa hao wa TCRA na Polisi walifanikiwa kufungua na kuchukua baadhi ya vifaa vinavyotumika kusambaza mfumo wa sauti na data na kuondoka navyo pamoja na mkurugenzi wa kampuni hiyo na wafanyakazi wengine watatu kwa ajili ya mahojiano zaidi…

Kampuni ya Six Telecom inahodhi makampuni mengine kadhaa ya mawasiliano hapa nchini

About Six Telecoms

Source: Google

Six Telecoms Company Limited operates primarily as a Tier-1 carriers-carrier headquartered in Dar es Salaam, Tanzania. While our business spans across sub-sectors and includes various products and services within the voice and data realm our function as an international gateway remains our focus, our core and our greatest strength.

Six Telecoms is the premier international gateway operating in Africa with aparticularly prominent presence in sub-Saharan Africa including East Africa, Southern Africa and West Africa.

Six Telecoms has pioneered the international gateway business through our investments and focus on network architecture and infrastructure.

Additionally, through strategic relationships with SEACOM, TEAMS and EASSy, the undersea fiber-optic cables straddling the East African coast, we have been able to establish excellent connectivity with Western Europe, Asia and the Middle East furthering our ability to provide quality access.

Six Telecoms degree of connectivity facilitates our interconnection with over 350 interconnect operators most of which are similarly tier-1 and tier-2 providers worldwide

===========================

UPDATE

Six Telecoms yafikishwa kortini

MKURUGENZI wa Kampuni ya Six Telecoms, Hafidh Shamte na wafanyakazi wengine watano, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka ya uhujumu uchumi kwa kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni nane.

Washitakiwa walifikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka mawili na mawakili kutoka Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), Jackline Nyantori na Johanes Kalungura wakisaidiwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Theophil Mutakyawa, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage.

Mbali na Shamte ambaye jina lake jingine ni Rashid, washitakiwa wengine ni Ofisa Mkuu wa kitengo cha Fedha, Raphael Hongo, Mha sibu Said Ally, Ofisa Masoko, Noel Chacha, Msimamizi wa mtandao, Tinisha Max na Mkuu wa takwimu za biashara, Vishno Konreddy.

Akisoma mashitaka, Jackline alidai, katika tarehe tofauti kati ya Mei 2010 na Januari mwaka huu, Dar es salaam, kwa lengo la kujipatia fedha, washitakiwa walitoza huduma za simu za kimataifa chini ya dola za kimarekani senti 25 kwa dakika.

Wakili Jackline, alidai jambo hilo lilisababisha washindwe kuilipa TCRA, mapato ya dola za Marekani milioni 3,836,861 zilizopatikana kutokana na huduma za simu za kimataifa zilizokuwa zinaingia.

Katika mashitaka mengine ilidaiwa, katika tarehe hizo, kutokana na kutoza chini ya dola za kimarekeni senti 25 kwa dakika na kushindwa kuilipa TCRA mapato yanayotokana na huduma hiyo, waliisababishia mamlaka hiyo hasara ya dola za kimarekani 3,836,861, sawa na Sh bilioni nane za kitanzania.

Wakili Jackline alidai, upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa. Awali, kabla washitakiwa hawajasomewa mashitaka, Hakimu Mwijage aliwaambia washitakiwa hawaruhusiwi kujibu mashitaka kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo isipokuwa Mahakama Kuu, au endapo Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) atatoa kibali kwa mahakama hiyo kusikiliza kesi hiyo.

Aidha alisema mahakama haiwezi kutoa dhamana, hivyo wapeleke maombi ya dhamana Mahakama Kuu. Washitakiwa walirudishwa rumande na kesi hiyo iliahirishwa hadi Janurai 28 mwaka huu itakapotajwa tena.

Wakati huo huo, Mwanasheria Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Johanes Kalungura ametoa siku saba kwa Bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Six Telecoms Tanzania Limited, kuilipa mamlaka hiyo deni la Sh bilioni nane.

Kalungura alisema hayo jana, Dar es Salaam, akiwa nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kuwafikisha mahakamani wafanyakazi watano wa kampuni hiyo kwa kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni nane.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kalungura alisema “naomba wakurugenzi wote au bodi ya wakurugenzi walipe fedha za wananchi, shilingi bilioni nane ndani ya siku saba kuanzia leo (jana), wasipofanya hivyo sheria itachukua mkondo wake dhidi yao” .

Aidha aliwakumbusha wamiliki wa makampuni yote yanayotoa huduma za mawasiliano, ambao wanajua hawajalipa tozo za nchi, walipe haraka kwa sababu wasipolipa watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.


Chanzo: Habari Leo
 
Last edited by a moderator:
Serikali ya Tanzania, Imeifungia Kampuni ya Six telecom kwa kuisababishia serikali hasara ya Billioni nane. Vilevile Kampuni hiyo, imekiuka taratibu za leseni za mawasiliano.
Hakuna kukamata mali na kufilisi??? Hakuna kushtakiwa??? Wahusika walikuwa ni akina nani???
 
Yaaan hii nchi ni shamba la bibi.
Yaaan hata hawajashtakiwa wamefungiwa tu. Na wanaeza kwenda fungua company nyingne wakapga kazi kama kawa.
Shamba la bibi.
 
Amazing. ...

Bila kukomesha hiyo tabia, si watatafuta njia ya kurudi kivingine?
 
Kwa namna ya wanasheria wa taasisi za serikali wasivyokuwa makini mara nyingi hunipa wasiwasi wa kodi ya wananchi kuja kutumika kulipa fidia.

Kilichotokea leo, sidhani kama ni namna nzuri ya kufanya kwa makampuni yanayofanya biashara,tena ya mawasiliano.

Hii move isiishie leo tu,tunahitaji majibu na hizo zaidi ya 8 bn kama hasara kwa serikali zilipwe kweli msifanye siasa katika biashara.
wafungiwe milele.
 
Last edited by a moderator:
Ujeuri sio kwenye awamu hii ya 5. Wako rumande sasa hivi kwa kauli na jeuri zao.
Najiuliza Huyo kijana Shamte hiyo jeuri ameitoa wapi!?
 
Jamaa ana confidence mpaka maafisa wa serikali wakagwaya isipokuwa yule mmoja! Mimi naona alikuwa anatetea upande wake ... Sometimes, hupaswi kuwanyenyekea maafisa wa serikali ...

Wakikuona boya watakutesa sana, isitoshe walienda na waandishi wa kuuzia sura. Hamjawahi kukutanana nao hawa! Mimi jamaa nimemkubali, huo ndo uanaume. Mwanaume gani anapenda kudharilika mbele ya mke/watoto kwenye Tv?!!
 
Jamaa ana confidence mpaka maafisa wa serikali wakagwaya isipokuwa yule mmoja! Mimi naona alikuwa anatetea upande wake ... Sometimes, hupaswi kuwanyenyekea maafisa wa serikali ...

Wakikuona boya watakutesa sana, isitoshe walienda na waandishi wa kuuzia sura. Hamjawahi kukutanana nao hawa! Mimi jamaa nimemkubali, huo ndo uanaume. Mwanaume gani anapenda kudharilika mbele ya mke/watoto kwenye Tv?!!
Pamoja na ujeri wake mwisho wa siku alinywea na kukubali kosa yani walikuwa wanakwepa kodi kwa kisingizio hakuna ufatiliaji! Na mitambo yao ilizimwa!

Mimi nawapongeza TCRA kwa kuanza kuwafatilia watoa huduma za simu maana serikali inapoteza pesa nyingi!

Endeleeni kuwasifu lakini nyie ndio huwa mko mstari wa mbele kusema serikali haifanyi kazi....
 
Jamaa ana confidence mpaka maafisa wa serikali wakagwaya isipokuwa yule mmoja! Mimi naona alikuwa anatetea upande wake ... Sometimes, hupaswi kuwanyenyekea maafisa wa serikali ...

Wakikuona boya watakutesa sana, isitoshe walienda na waandishi wa kuuzia sura. Hamjawahi kukutanana nao hawa! Mimi jamaa nimemkubali, huo ndo uanaume. Mwanaume gani anapenda kudharilika mbele ya mke/watoto kwenye Tv?!!
Wanaume kwenye kuikosesha Serikali mapato sio!!?? Muulize yuko wapi jioni baada ya kuwa nyumbani na mkewe na watoto!? Shuwaini Kama wewe huwa naomba nikutane nao kwenye kazi zangu halafu uniletee hiyo jeuri.
 
Jamaa hajui serikali ya awamu ya 5 ilishaondoka nini, ngoja tusubiri mwisho wa ili sakata
 
Back
Top Bottom