Kampuni ya simu ya TIGO ni WEZI

mtzd

Member
Jan 29, 2010
81
25
Kwema wana JF,
Hivi hawa wamiliki wa huu mtandao wa simu wana undugu na serikali yetu au? wana matatizo na ni wezi na hata tunapolalamika hawachukuliwi sheria yoyote na mamlaka husika. Jana niliweka salio kwenye simu yangu cha kustaajabisha nilipomaliza kuweka salio na mesegi ikaja kwamba nimeweka salio la kiasi cha vocha niliyonunua,baada tu ya kumaliza nikaangalia salio ,nakutaka wamenikata kama mia 400 hivi ,na sijawahi kuweka huduma ya kukopa wala nini,nikajaribu kuwapigia niwaulize kulikoni,mpaka ninapoandika uzi huu sijapata majibu yoyote kutoka kwao,,kuna yoyote ambaye ameshawahi kupatwa na hili? maanake sasa nadhani inawezekana wakawa wanatukata hela zetu bila sisi kujua,kama ningekua sijaangalia salio kabla ya kupiga nisingejua.Hivi huu wizi utaisha lini jamani.na kingine ni kufanya simu zetu kuwa kama za matangazo ,kwa sababu kila unapopiga simu kuna muda yanakuja maelezo mengi ,mara pata ofa,mara lipa kwa tigo pesa.Tafadhali wahusika jaribuni kutufikiria kwa hili.Huduma za kampuni hii zinatoboa kweli.
 
Tigo wanalalamikiwa sana.
Uki google utakuta lawama nyingi kwa tigo. Hata hapa JF watu wengi wameshalalamika.
Pia Tigo wana tabia ya kukata fedha za watu kupitia promosheni zao. Ukilalamika mpaka waondoe tayari umekatwa labda TShs 800. ambayo ikitokea kwa wastani wa wateja 1m ni sawa na 800m.
Ni wizi wa kawaida.
 
Naona hii sasa ni vita ya mitandao ya simu za mikononi humu JF.

Juzi uliletwa uzi ukidai Airtel money wanatuibia, mara Airtel yauzwa kinyemela? Sasa naona nao wameamua kujibu mapigo!!
 
Back
Top Bottom