Kampuni ya sasatel yafilisika rasmi.

Natasha Ismail

JF-Expert Member
Jul 14, 2008
747
640
Wapendwa,
Nimepata taarifa toka kwa mdogo wangu aliyepo sasatel kuwa hadi leo hii hawajalipwa mshahara wa mwezi wa saba na ule wa mwezi wa sita walipewa nusu tu.inasemekana kampuni imeuzwa kwa wasanii wa kitanzania ambao hata hawajui jinsi ya kuendesha kampuni.wafanya kazi wanahofia kudhulumiwa haki zao zote.
 
sasatel ipo kwenye market kitambo ila sales zao zimeshindwa kuhit kabisaa , waje tukaange mihogo huku kwa Alimaua B kwetu kuliko usanii
 
mambo Natasha Ismail
hata mimi kuna mshikaji yupo hapo miezi ya nyuma ashawahi nidokeza kuwa kampuni hiyo ina hali mbaya, sasa pengine huu ndio umekuwa mwanzo wa mwisho
 
Last edited by a moderator:
Wapendwa,
Nimepata taarifa toka kwa mdogo wangu aliyepo sasatel kuwa hadi leo hii hawajalipwa mshahara wa mwezi wa saba na ule wa mwezi wa sita walipewa nusu tu.inasemekana kampuni imeuzwa kwa wasanii wa kitanzania ambao hata hawajui jinsi ya kuendesha kampuni.wafanya kazi wanahofia kudhulumiwa haki zao zote.

kwa hiyo mshahara usipolipa kwa miezi 7 ndio unafilisika Rasmi?
 
Daaa inauma saana ukifikiria umo ndani ya kampuni na ajira imekata...waenda wapi?
 
sasatel ipo kwenye market kitambo ila sales zao zimeshindwa kuhit kabisaa , waje tukaange mihogo huku kwa Alimaua B kwetu kuliko usanii

I was wondering kwanini walikuja na technology ambayo ilikuwa obsolete. Ile technology ndio waliyoanza nayo Mobitel na Tritel. Wao walikuwa wame target soko gani?
 
Kampuni ya simu za mkononi ya SASATEL iko choka mbaya kiasi cha kushindwa kulipa mishahara ya wafanyakazi wake. Kwa muda sasa hali ya mambo ndani ya shirika hili si nzuri kiasi cha kufikia kulipa mishahara ya wafanyakazi wake kwa mafungu.

Wafanyakazi walilipwa nusu mshahara mwezi wa saba nusu iliyobaki hawajalipwa mpaka sasa. Wafanyakazi wana wasiwasi sana kuwa sasa wanaelekea mwisho wa mwezi wa nanae huku hawajalipwa nusu ya mwezi julai.

Huyu mwekezaji vipi?
 
Haya ndiyo madhira yanayowakumba wafanyakazi wa kampuni zinazoanzishwa mwishoni mwa mwaka (X-Mas time)
 
Walikuja na mbwembwe wakakutana na akina tigo wakashindwa wakaamua kuwekeza kwenye internet zaidi ambayo nayo ni bogus sasatel huwezi tumia mikoani kama airtel hiyo kampuni isipouzwa itafungwa mda wowote
 
Kampuni imeshindwa kabisa kukamata kipande cha soko, itabidi iuzwe au ife karibu sana, nakumbuka nilikuwa naangalia stats za makampuni ya simu Tanzania hawa jamaa wanatia huruma kusema ukweli na kama sikosei walipoteza jumla ya wateja mwaka huu wakati kila kampuni zote nyingine zimeongeza.
 
tumieni akili nyie, jiulize mtaani kwako kuna maduka mangapi wavocha za sasatel. modem, line nk

mmwambie mdogo wako aondoke haraka, aandike barua ya kuacha kazi ni muhimu,aende NSSf haraka akaangalie chake kiliwekezwa? afuatilie..kwanza afuatilie nssf, pili atafute kazi nyingine ndio atoke, ila kwa hali ya hapo akishajua haki zake zilipelekwa nssf na zipo, aondoke..its from experience..my take
 
Back
Top Bottom