Kampeni zikiwa mbichi polisi waliolewa wajeruhi kwa risasi

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
VURUGU zilizoambatana na ufyatuaji risasi zimetokea katika machimbo ya madini ya rubi ya Winza, Mtakanini, Mpwapwa mkoani Dodoma ambako watu kadhaa wamejeruhiwa kwa risasi akiwamo mwanamke mmoja.

Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zimeeleza kwamba tukio hilo kwa kiasi kikubwa zimesababishwa na polisi waliofika eneo hilo wakiwa na silaha huku wamelewa pombe kiasi cha kukosa maelewano na wachimbaji wadogo wanaotakiwa kuondoka eneo hilo.

Katika tukio hilo polisi walitumia risasi za moto ambapo mama mmoja alipigwa risasi ya kichwa na imemparaza upande wa sikio.

Mtoa habari wetu anasema, "Chanzo cha vurugu ni baada ya polisi 10 wakiwa na OSS wa Mpwapa na afisa madini kanda ya kati Singida."

Tatizo la awali linaelezwa na mtoa habari wa JF kuwa ni ugomvi wa kugombea eneo hilo baada ya kutolewa amri ya kuwaondoa wachimbaji wadogo.

"Polisi hao walipopewa kitabu cha kusaini kama wageni wakakataa na kuanza kumpiga aliyewapa kitabu hicho na kuanza kupiga watu ovyo na ndipo vurugu zikaanza na watu kukimbia.

"Wakamkamata alowapelekea kitabu hicho na kuanza kuwakamata watu na kutembeza risasi. Wakawapa masaa mawili kusiwe na watu maeneo hayo.

"Wamevunja maduka, wakamwaga vyakula na vinywaji lakini walikuja wakiwa wamelewa hata askari polisi," anasema.

Maandalizi ya kuwashambulia wachimbaji wadogo yanaelezwa kuwa yalianza tangu jana Jumanne Agosti 24, 2010 baada ya polisi hao kulala eneo la jirani na mgodi walikokesha wakilewa.

"Hawa jamaa walipewa leseni lakini zilifutwa, mkuu wa Wilaya aliwambia kuwa wachimbaji wadogo walitangulia hivyo walitakiwa kuwaacha.Hawa tayari walikuwa wana maeneo mengine hivyo wamewaingilia," anaeleza mtoa habari.

Watu wafuatao ndio wanaodaiwa kuwaongoza polisi eneo hilo; Aboubakar Mtuluchile, Johnson Kamala pamoja na Shao, Leloo, Mussa Mansour, Hamad Msuya, Pazi na Moses Mnuo.

More to come soon;
 
DUh, polisi waliolewa kufyatua risasi, imekosa mvuto!!!!! hawa watu waliahidiwa maziwa na asali na watu wa CCM sasa wanatimiliwa hata kabla ya uchaguzi na utashangaa MBUNGE na DIWANI wa eneo hilo atatoka CCM
 
Tuwahurumie WATANZANIA wenzetu kwa kuukubali utimwa wa kujitakia
 
CCm inawapa hawa watu jeuri sana maana hakuna uwajibikaji kuanzia kwa mdogo mpaka mkubwa. ni kulindana tu,
 
Back
Top Bottom