Kampeni za Mafanikio na elimi ya msingi-watoto waendelea kukaa chini!

kmp

Member
Jun 18, 2009
39
0
02.jpg
03.jpg


Shule ya Msingi Nduli, ni kilomita takribani 20 kutoka Iringa mjini kwenye jimbo la uchaguzi la Isimani. Pichani ni wanafunzi 120 wa darasa la kwanza chini ya mwalimu Daniela. Mazingira hayo ni magumu, wanahitaji kusaidiwa. Shule ina wanafunzi 670 na walimu 13.

MMEM imefanya kazi gani jamani kama hali yenyewe ndio hii?

Na mawaziri wanakuja kutueleza mafanikio katika uongozi wao, ni mafanikio yapi kama hali ndio hii katika shule zetu.

Hii ni mjini, je vijijini kuna hali gani?


Mweeeee jamani!!!


Source:mjengwa.blogspot.com
 
Yaani "SIRIKALI" ya CCM imewafanya wa-Tanzania waamini kuwa shule ni vyumba vya madarasa...hahahah!
Kwa wananchi wanapojengewa vyumba vya madarasa basi wanaviita shule...jamani shule ina mambo mengi
jamani.Kwanza kwa miaka hii "SIRIKALI" haina shule hata moja...yaani hata ambazo tuliachiwa na wakoloni
tumeshindwa kuziendeleza na hazina tofauti na maboma au vyumba vya madarasa ambavyo tumeendelea
kuvijenga kupitia kwa wahisani au kwa kutembeza bakuli!
 
Back
Top Bottom