Hili halina ukweli hata kidogo. Kwanza mfumo wetu wa maisha na ule wa kimagharibi ni tofauti kidogo. Mtu akiwa na mkewe/mumewe anakumbana na mengi kuanzia presha za extended family, kucheat nk. Lakini pia nikutolee mfano mdogo tu wa watu waliowahi kudivorce kutoka huko unakokuita kwenye maendeleo. Kuna Reagan (USA) na Sarkozy (France) achana na yule muhun wa Italy.
Hongera Ngongo umeleta hoja ya maana sana.
umesahau jambo moja muhimu sana kuhusu udhaifu wa batilda salha.kwanza kabadili dini ukubwani kwasababu ya mwanaume,huu nao udhaifu angekuwa na mtu wa msimamo asingebadili dini eti kwasababu ya kuolewa tu.Tumeshuhudia akina mama kibao wakiolewa na wakristo au waislam wakiendelea kuabudu dini zao.
batilda ameolewa na kuachika mara tatu.Huu nao ni udhaifu kuachwa mara tatu ni doa kubwa sana.
Batilda kaolewa Zanzibar ni kwanini asigombee huko alikoolewa au anataka kujifanya Anna kilango.
Batilda ana uhusiano wa karibu usikuwa wa kawaida na lowassa
Duh mkuu meza mate its better mjadili hoja sio watu jamani jadili uwezo wa mtu kwa elimu yake na muonekano wake ukirefer valid evidences kuacha au kuachwa, masuala ya dini upagani hayo ni maisha binafsi ya mtu.
Heshima kwako Sokomoko,
Mkuu CCM sikuhizi ukuitaja EPA wanakwambia umetukana.wanataka uzungumzie sere tu hawataki uzungumzie watu wataozitekeleza hizo sera amabo ni muhimu sana.Watu wa hovyo sirahisi kutekeleza sera hataziwe nzuri kiasi gani mkuu wangu.Hili limekuwa ni tatizo kubwa sana kwa nchi yetu ya Tanzania,tunakubali kuongozwa na watu wa hovyo wasiozingatia maadili hata chembe.huwezi kuwa kiongozi mzuri kwa taifa wakati uongozi wa familia yako umekushinda.
Mimi nadhani kuna mengi sana yanayomfanya mtu awe kiongozi bora bila kutizama ya kifamilia na dini.... hivi hujui kuwa kwa jinsi Hilter alivyokuwa akiogopewa lakini kwa mkewe alikuwa mboga kabisa? Au Rais fulani hukumbuki alipigwa na kitu na waifu wake mpaka akawa anatembelea mguu wa tatu? naheshimu ufaragha wa mtu na kiongozi bora sio lazima atoke chadema na cuf hata CCM wapo na naweza kuwataja.....ane kilango, samwel sitta etc etc sio wote wenye mawazo mgando wengine wanapambanunua na kujua pumba na mchele TAFAKARI
Ngongo, asante kwa uchambuzi yakinifu kuhusu kinyanganyiro cha ubunge Arusha. Ninachokiona hapo ni kwa TLP na Chadema kugawana kura za upinzani, hivyo CCM kupita kwa ulaini. Mikoa ya Kaskazini ni mikoa yenye vuguvugu la upinzani, watu hawauzi uhuru wao kwa shibe ya siku moja 'pilau', au kwa t-shirt na kofia, lakini inapotokea wapinzani kupingana, hivi ni vita vya panzi, faida kwa kunguru.
Uongozi ni kipaji na uwezo na sio elimu, japo elimu ni just an added advantage, kama mtu ana uwezo wa uongozi hata darasa la saba, atakuwa kiongozi bora, ndio maana kuna mababu zetu hawakusoma, lakini walikuwa viongozi wazuri tuu wenye busara. Wapinzani lazima waungane, vinginevyo Arusha hiyo...CCM!.
Heshima kwako HM Hafif,
Mkuu nilitegemea ungesoma hoja vizuri na ungekuja na majibu ya kukataa au kuunga mkono yote niliyoandika kuhusiana na Mama Batilda Buriani badala yake unakuja na viroja kwamba ni chaguo la wengi Arusha.Mkuu hata Lowassa pamoja na madudu yake kibao bado ni chaguo la wengi Monduli vivyo hivyo Rostam ni chaguo la wengi Igunga.
Asome hoja zikowapi zaidi ya propaganda zako......Nini madudu ya Batilda Burian?? Je Lema ana nini cha kumzidi Batilda?? Hivi Phd ya Batilda ni ya nini na Phd ya Lyimo ni ya nini na kutoka vyuo gani? Uzoefu wa Batilda upo wazi, nini uzoefu wa Lyimo ambao tutautumia kumpima?? Kama chama hivi kweli TLP kuna chma zaidi ya nafasi ya kisiasa ya LYATONGA MREMA?? Propaganda zako NGONGO/KABONDE zinaonyesha wazi mtazamo mgando ulio nao kuhusu wanawake ambao ndio unaotawala katika chama cha msimu cha TLP. No wonder katika wote waliopo huko mkampata Mr Cut and Paste Book Writer/Mission town Mtamwega kupeperusha bendera yenu ya Urais......
Mwacheni Batilda wa watu kabla hamjaamsha mnaodhani wamelala....
Omarilyas
Mwanaume anasema viti maalum viondolewe na wanawake wagombee na kupambana sawa na mgombea mwanaume.
Akijitokeza mwanaume kugombea ubunge ni sawa, akijitokeza mwanamke, ana jeuri ya mwanaume au watu kuuliza jeuri anaitoa wapi.
Mwanaume wakiwa na girlfriend 100, tena sometimes 10 at one time it is okay tena ni kidume cha mbegu. Akitokea mwanamke kaolewa mara 3, hana maadili.
Asante mke kwa kukubali kuolewa, asante Mama kwa kukubali kuzaa. Ikitokea siku moja hawa wanawake wanaodharauliwa na wanaume wakagoma kuolewa au kuzaa...... tutatafutana.
Tunajua Mama Batilda anauzoefu wa kuwazuia wabunge wasijadili hoja ya RICHMOND.Ukiniuliza sababu za Omarlyas kumtetea Mama Batilda nashindwa kuelewa na pengine hii ni sababu tosha ufisadi unaendelea kutamalaki Tanzania.
Mtu yuko tayari kumtetea fisadi kwasababu ni ndugu yake,rafiki yake,jirani yake,kabila lake,dini yake,shangazi yake au mjomba.baba au chama chake.Omarlyas anaangukia katika kundi moja wapo niliyoyataja.Sina haja ya kubishana / ligi ya kipuuzi.
Duh hili nalo neno.Hakuna mtu anaekataa mwanamke kugombea nafasi za kisiasa kinachogomba au ninachokiangalia ni uwezo wa mtu.kamwe hatuwezi kumchagua mtu kwasababu ni mwanume au mwanamke tunamchagua mtu kwakuwa ana uwezo na si vinginevyo.Hoja yangu kubwa kuhusu Mama Batilda ni uwezo wake unatia shaka shaka nyingi,nimejaribu kutaja mbili na nikaomba wengine wachangie wamekuja wakaongeza hilo la kuolewa mara tatu pia ikumbukwe mgombea wa CHADEMA kalisema hili Mama Batilda badala ya kujibu kakimbilia kushtaki kwa msimamizi wa uchaguzi kwamba katukanwa tunasubiri majibu ya msimamizi wa uchaguzi tujue kama ni matusi hayo ua vinginevyo.