Kampeni ya Ubunge Arusha Mjini - Batilda Burian Vs Lema

KATI YA BATILDA NA LEMA YUPI ATIBUKA KIDEDEA?

  • Total voters
    52
Hebu acha kampeni za kitoto...

Kwani nani haelewi kuwa Ngongo, Kabonde na Nguruvi3 wote mtu mmoja anajitahidi kuonyesha kuwa anaungwa mkono...

Sipendi mabishano yasiyo na tija, lakini napenda nikuhakikishie kuwa mimi siwajui M/S Ngongo au Kabonde zaidi ya kusoma kutoka JF. Kama tunauelekeo wa mawazo unaofanana that's fine. Simpigii mtu kampeni ila ungesoma vizuri habari ungejua kwanini nina encourage watu walete data. Article imejibu swali muhimu sana kuhusu Batilda! ''Nguvu ya kisiasa'' hasA ukizingatia kuwa nimeishi na kufanya kazi Arusha nazijua siasa za pale. Sasa kama wagombea wa CUF na Chadema wana credentials zao ziwekwe tuwajue!. Hoja ni kuwajua wagombea.
 
Uchambuzi ni mzuri ambao uko balanced hata kama upande mmoja wa mizani umeelemewa kwa fact. Mama Burhani ana elimu nzuri na ya uhakika, lakini ana mapungufu mengi sana kama kiongozi. Lema hana elimu kabisa ingawa anaweza kuwa na uwezo wa kuongoza. Ni vigumu kubadili facts
 
Ka TLP nako kameamua kupaza kasauti na kenyewe kaonekane kamo, endelezeni mayowe msikike - Lyatonga Augustino Mrema awahitaji.
 
Itakuwa mara ya kwanza jimbo la Arusha kuongozwa na mwanamke. Ikitokea basi, bila shaka Waarusha atakuwa wamebadili mila na desturi zao.

........hili nalo neno si la kupuuzwa .....mkoa wa arusha na kilimanjaro ukiondoa mama kilango na mama nagu sikumbuki mbunge mwanamke wa kuchaguliwa kwa kura tangu miaka ya 70 hadi sasa ......kama atashinda dada burian ni kweli atahitaji pongezi kwa kuvunja rekodi!!!!
Tena bora wapare wana msimamo wa wastani..lakini wachagga na wamasai....wana mfumo dume sana sana...ndio maana mkoa kama Kilimanjaro umepata kuwa na wanawake maarufu na hodari kama Lucy Lameck,Zakia Meghji etc Lakini hawakupata kuchaguliwa na wapiga kura...hata kinamama wengine ni wachagga wanachaguliwa na wapiga kura mikoa mingine lakini kilimanjaro hawadhubutu kugombea!!!!....kabla mama salome mbatia hajafariki ndie kidogo walikuwa wanamfikira kumpa ubunge......,hata mdogo wake mama mkapa huwa anashindwa na mzee ndesa sometimes kwa ajili ya mfumo dume ....lakini kwa mfano uchaguzi wa mwaka 2005...ccm wangeweka mtu imara waneweza kumuangusha ndesa!!!
Pamoja na mapungufu yake .....battilda atakuwa anapigania kuvunja mwiko.....na anaweza kushinda hasa ukizingatia udhaifu wa wagombea wa upinzani waliowekwa Arusha.....!!!
 
Sipendi mabishano yasiyo na tija, lakini napenda nikuhakikishie kuwa mimi siwajui M/S Ngongo au Kabonde zaidi ya kusoma kutoka JF. Kama tunauelekeo wa mawazo unaofanana that's fine. Simpigii mtu kampeni ila ungesoma vizuri habari ungejua kwanini nina encourage watu walete data. Article imejibu swali muhimu sana kuhusu Batilda! ''Nguvu ya kisiasa'' hasA ukizingatia kuwa nimeishi na kufanya kazi Arusha nazijua siasa za pale. Sasa kama wagombea wa CUF na Chadema wana credentials zao ziwekwe tuwajue!. Hoja ni kuwajua wagombea.

Heshima kwako Nguvu3.

Mkuu usiangaike kuumiza kichwa JF mavuvuzela wanapenda majungu badala ya kujibu hoja ambazo zinaweza kutusaidia kupata viongozi bora.Naomba tena na tena wenye data za wagombea ubunge wa jimbo la Arusha mjini wamwage hapa jamvini tuzijadili kwa kina hatimae tuwasaidie wapiga kura kufanya maamuzi ya maana.
 
Huyo Batilda amezaa na ENL

Heshima kwako Mwanamilembe,

Binafsi hii habari ni mpya kidogo,uhusiano ninaouzungumzia ni wakisiasa zaidi mambo mengine ya faragha sina habari nayo pia nilazima tujaribu kuangalia maslahi ya taifa kuliko kuyatazama mambo binafsi.
 
........hili nalo neno si la kupuuzwa .....mkoa wa arusha na kilimanjaro ukiondoa mama kilango na mama nagu sikumbuki mbunge mwanamke wa kuchaguliwa kwa kura tangu miaka ya 70 hadi sasa ......kama atashinda dada burian ni kweli atahitaji pongezi kwa kuvunja rekodi!!!!
Tena bora wapare wana msimamo wa wastani..lakini wachagga na wamasai....wana mfumo dume sana sana...ndio maana mkoa kama Kilimanjaro umepata kuwa na wanawake maarufu na hodari kama Lucy Lameck,Zakia Meghji etc Lakini hawakupata kuchaguliwa na wapiga kura...hata kinamama wengine ni wachagga wanachaguliwa na wapiga kura mikoa mingine lakini kilimanjaro hawadhubutu kugombea!!!!....kabla mama salome mbatia hajafariki ndie kidogo walikuwa wanamfikira kumpa ubunge......,hata mdogo wake mama mkapa huwa anashindwa na mzee ndesa sometimes kwa ajili ya mfumo dume ....lakini kwa mfano uchaguzi wa mwaka 2005...ccm wangeweka mtu imara waneweza kumuangusha ndesa!!!
Pamoja na mapungufu yake .....battilda atakuwa anapigania kuvunja mwiko.....na anaweza kushinda hasa ukizingatia udhaifu wa wagombea wa upinzani waliowekwa Arusha.....!!!

Mkuu PM hapo kwenye nyekundu na bold naomba kutofautiana na wewe.Mgombea dhaifu upande wa upinzani ni G Lema wa Chadema.M Lyimo ni mgombea mzuri wa upinzani tena anauzika ukilinganisha na wapinzania wake mama Richmond na vuvuzela lema

Hongera Ngongo umeleta hoja ya maana sana.

umesahau jambo moja muhimu sana kuhusu udhaifu wa batilda salha.kwanza kabadili dini ukubwani kwasababu ya mwanaume,huu nao udhaifu angekuwa na mtu wa msimamo asingebadili dini eti kwasababu ya kuolewa tu.Tumeshuhudia akina mama kibao wakiolewa na wakristo au waislam wakiendelea kuabudu dini zao.

batilda ameolewa na kuachika mara tatu.Huu nao ni udhaifu kuachwa mara tatu ni doa kubwa sana.

Batilda kaolewa Zanzibar ni kwanini asigombee huko alikoolewa au anataka kujifanya Anna kilango.

Batilda ana uhusiano wa karibu usikuwa wa kawaida na lowassa

Acheni kuzunguka m-buyu sababu ni hiyo hapo, mnakerwa na uislamu wake. Hayo mengine ni blah blah tu
 
[/FONT] Mgombea Ubunge wa CHADEMA
Godbless Lema elimu yake haijulikani kabisa na ni moja ya mambo yaliyochangia kupunguza kura zake katika uchaguzi wa mwaka 2005.Anadai anacheti cha Computer lakini hatakia kutaja jina la chuo alichosoma wala mwaka aliomaliza.Anadai alimaliza kidato cha sita lakini hataki kutaja jina la shule aliyosoma wala mwaka na alama alizopata ??????????.
Godbless Lema haijulikani anafanyakazi gani haswa, mara nyingi anapenda kujiita mfanyabiasha za madini na wakati mwingine anadai kununua vitu mbali mbali Dubai & Japan.Hana ofisi ya biashara inayojulikana muda wake mwingi anapenda kukaa mitaani kuzungumzia mambo asiyoyajua vyema kwa kujidai anayajua kuliko mtu mwingine.

Godbless Lema ni dalali mzuri wa siasa za upinzani anajua kucheza karata zake vizuri sana huku akiyatanguliza maslahi yake binafsi.Bwana Lema anahusika bila shaka yoyote alifanikisha deal ya kumuondoa Diwani wa TLP Sombeti Bwana Mawazo na kumpeleka CCM kwa ujira wa pikipiki za mafisadi na kiwanja.Baada ya kutimuliwa TLP akakimbilia CHADEMA na amefanikwa kujinyanyua hadi akapitishwa kugombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA .wanamageuzi bado wanakumbuka jinsi alivyoiondoa kesi ya kupinga ushindi wa Mheshimiwa Felex Mrema mahakamani bila kuwashirikisha viongozi wa chama wakati chama kilitoa fedha za kugharamia kesi.Ilikuja kubainika Bwana Lema alipewa kitu kidogo ili kuiondoa kesi mahakamani.

Godbless Lema akifaniwa kuwa mbunge wa Arusha mjini ataongeza idadi wa viti vya wabunge wa upinzani jambo ambalo ni jema na afya kwa demokrasia ya Tanzania lakini hatakuwa na mchango wa maana bungeni kama akina Dr Slaa na Zitto Kabwe sana sana ataongeza idadi tu.
Godbless Lema anategemea zaidi umaarafu wa CHADEMA kuchaguliwa anatamani sana wapiga kura wasahau alivyorubuniwa na CCM mara mbili.
[1] Kumpeleka Mawazo CCM.
[2] Kufuta kesi ya kupinga ushindi wa Felex Mrema .
[3] Atapenda wapiga kura wasihoji elimu yake.
[4] Atapenda wapiga kura wasihoji kazi yake.
[5] Atapenda wapiga kura wampigie kura kwasababu ya umaarafu wa CHADEMA na Dr Slaa.

Naongezea Wasifu: Kuhusu Lema ni ukweli kabisa wala bwana/bibi Ngongo haujakosea, kwa kweli ni mtu wa bla bla, hapa Arusha kuna wakati alianzisha ki-organization sijui Positive kitu gani kinaendelea hapo mbele lakini sikumbuki vizuri hayo maneno mengine. Kwa kweli anaushawishi mkubwa sana kwani alifanikiwa kuwavuta vijana wengi wakiwemo wasomi, lakini baada ya muda kilichotokea hapo sijajuwa ni nini, hila chama kilisambaratika. Biashara yake nyingine anamiliki min-supermarket maeneo ya mianzini, arusha. Kwa sasa pia anajishughurisha na uandishi wa vitabu vya dini, sijui kama mnajua kwamba anajifanyaga mtu wa dini sana yaani kama mlokole flani hivi. Na mitaa ya kijiwe ni pale Sinka Hotel watu wa ARusha nadhani mnaifahamu hii mitaa ni ya mabroker wa mawe. Nawakilisha!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.

Kuhusu siasa: Yale mambo ya Sombetini yalitokea, ni kweli ana bla bala, lakini siasa si ndo bla bla jamani, kwani kuna uabaya gani? Kama anaweza kushawishi wapiga kura wakamchagua yeye na chama chetu ndivyo tunavyotaka kwani CCM tumeichoka. Mbona Jacob Zuma ana elimu ndogo na ni raisi tena wa nchi iliyoendelea kama South Africa, nini kuwa Mbunge wa jimbo la Arusha. Mbona aliyetoka ni msomi tena si msomi kidogo, mwanasheria aliyewahi kushika nyadhifa serikalini ametufanyia nini? Kwa miaka yote ambayo amekuwa Mbunge wa ARusha Mjini. Kwa hiyo kuwa karibu na wananchi/wapiga kura ni advantage kwa Lema na kwa chama chetu, angalau ana mambo ya kuwapelekea viongozi wa juu wa chama chetu(CHADEMA) yaani feedback kwa sababu yuko karibu hivyo cha msingi atashirikiana na kina Zitto na mpiganaji wetu Dr. Slaa wataleta maendeleo, maendeleo sio vyeti hata wasomi wanachemsha.
 
Heshima kwako Safina,

Mkuu safina kweli unamfahamu G Lema kuanzia tabia zake,elimu yake na makidai yake.

Inavyoelekea wewe ni muumini mzuri wa siasa za upinzani ?.Hivi nilazima tumchague Lema kwasababu tu anawakilisha upinzania ?.Hakuna wapinzani wengine au vyama vingine vya upinzani ?.Bwana / Bibi Safina inaelekea umeingia kwenye kale kaugonjwa ka chademaism.Mwl Nyerere aliwahi kumpigia kura mbunge wa upinzani mwaka 1995 kwasababu mgombea wa CCM wakati huo alikuwa ana kaharufu ka rushwa.Jiulize Nyerere alikuwa nani ndani ya chama cha mapinduzi na ni kwanini alikataa kuingia kwenye mtego wa kuabudu chama.Tafadhali Safina nakuomba utoke kwenye box la chama ambalo kwa muda mrefu limetufanya watanzania tuamini Tanzania hawezekani bila CCM.

Bwana / Bibi safina umetoa mfano wa Jacob Zuma wa S.Afrika.Kifupi sana Zuma si mfano bora wa viongozi wa Afrika amechaguliwa kwasababu ya historia yake ya kupinga ubaguzi.Uchafu wa Zuma wa kutembea na wanawake wengi tena wengine wenye ukimwi si mfano mzuri wa viongozi wa kizazi chetu.

Nashukuru umekiri ufisadi wa Sombetini ulivyoratibiwa na Bwana Lema.Safina bado tu unataka tumchague Lema ?????????????????.CHADEMA kiliendesha operesheni sangara kwa mafaniko makubwa mno sikutegemea wangekuja na wagombea wa hovyo kiasi hiki.Tazama wagombea wa vitu maalumu [wakina mama ]mkoa wa Arusha utashangaa mashangingi ya mjini yalivyojazana.CHADEMA kama kinataka kuongoza Tanzania lazima kiandae viongozi si kuokota viongozi barabarani.
 
Mimi ni mmoja kati watu wanaofahamu siasa za Arusha......Godbless Lema ni mmoja kati ya vijana wanao kubarika Arusha tena kwa lika zote...Huyu jamaa anajenga hoja ile mbaya huwezi kum-compare na akina Batilda Salha Buriani AU lyimo.
Jamaa anajenga hoja kama akina zitto,slaa,Mpendazoe na wengine wengi kama hao..nimeisoma post yako Ngongo umejitahidi kuwa neutral lakini ,upo upande wa Lyimo.....Kuhusu Elimu ya Lema hicho siyo Kigezo kwa sababu katiba inamtaka mbunge ajue kusoma na kuhesabu tu so hapa hoja ya elimu ingawa ni mhimu lakini haina mashiko.......kama tatizo ni elimu nenda RORYA uta mkuta mtu anaitwa AILO huyu jamaa ni STD seven na alikuwa anajitangaza mwenyewe lakini uliza kamfanya nini Profesa bingwa wa mifupa Tanzania na Duniani Prof.SALUNGI...so wana Arusha huu ndiyo wakati wao kumchagua tena kijana wao Lema..kuhusu Swala la Mawazo kuhamia CCM hayanaa ukweli kuwa ni Lema ndiyo aliye mwambia ahamie CCM..sababu ifahamike Lema huyu huyu ndiyo alishiriki kumuapisha mwalimu Mawazo mbele ya viongozi wa Dini kuwa hata hama chama hii ni baada ya CCM kuanza njama za kumununua mwl.Mawzo..kama angekuwa amempeleka mwazo CCM kwa nini yeye hajahamia CCM??? huu ni wakati wa uchaguzi tuwe wakweli jamani...
ukitaka kujua kuwa jamaa antisha uliza ARUSHA chaguo lao ni nani this yr......Lakini naungana na Ngongo kuwa kama uchaguzi utakuwa fair basi BURIANI hanan chake....
 
Labda kwa kuwa simfahamu Lyimo na sijawahi kuhudhulia mihadhara yake. Nitajaribu kumsikiliza na yeye. Lakini kwa Sasa mimi ubunge Lema, urais Slaa, nitashawishika na Lyimo baada ya kumsikiliza na nione kama atanishawishi vya kutosha kama huyu jamaa. Tatizo lingine naanza kupatwa na wasiwasi nisije nikampa kura yangu Lema halafu akifika bungeni huu ushawishi wake alionao sasa hivi akaenda kuwa domo zege. Mkuu hili la Zuma kuhusu wanawake sijawahi kusikia kashfa, jamaa ana mke wake anaitwa Neema na wamebarikiwa kupata watoto wawili. Naomba kuwakilisha samahani kama nimekukwaza.
 
........hili nalo neno si la kupuuzwa .....mkoa wa arusha na kilimanjaro ukiondoa mama kilango na mama nagu sikumbuki mbunge mwanamke wa kuchaguliwa kwa kura tangu miaka ya 70 hadi sasa ......kama atashinda dada burian ni kweli atahitaji pongezi kwa kuvunja rekodi!!!!
Tena bora wapare wana msimamo wa wastani..lakini wachagga na wamasai....wana mfumo dume sana sana...ndio maana mkoa kama Kilimanjaro umepata kuwa na wanawake maarufu na hodari kama Lucy Lameck,Zakia Meghji etc Lakini hawakupata kuchaguliwa na wapiga kura...hata kinamama wengine ni wachagga wanachaguliwa na wapiga kura mikoa mingine lakini kilimanjaro hawadhubutu kugombea!!!!....kabla mama salome mbatia hajafariki ndie kidogo walikuwa wanamfikira kumpa ubunge......,hata mdogo wake mama mkapa huwa anashindwa na mzee ndesa sometimes kwa ajili ya mfumo dume ....lakini kwa mfano uchaguzi wa mwaka 2005...ccm wangeweka mtu imara waneweza kumuangusha ndesa!!!
Pamoja na mapungufu yake .....battilda atakuwa anapigania kuvunja mwiko.....na anaweza kushinda hasa ukizingatia udhaifu wa wagombea wa upinzani waliowekwa Arusha.....!!!

Mimi nadhani ni muda mufaka wa kujua kuwa Arusha si ya Waarusha peke yao. NI mji mkubwa sana wenye mix kubwa sana. Umekuwa mji mkubwa sana na uliochanganyika sana sana. Kwa mfano, ukienda Sombetini, Kwa Idd, Ngulelo, mpaka katikati ya mji mchanganyiko ni mkubwa sana. Wamasai wa mjini (waarusha) wamebakia wenyewe kwa wingi maeneo ya Sanawari ni vitongoji vya karibu yake.

Huko Uchagani (Moshi) sina cha kuchangia. Hao mangi bila shule hapa Tanzania kuanzia huko kwao sijui ingekuwaje leo!
 
Mimi ni mmoja kati watu wanaofahamu siasa za Arusha......Godbless Lema ni mmoja kati ya vijana wanao kubarika Arusha tena kwa lika zote...Huyu jamaa anajenga hoja ile mbaya huwezi kum-compare na akina Batilda Salha Buriani AU lyimo.
Jamaa anajenga hoja kama akina zitto,slaa,Mpendazoe na wengine wengi kama hao..nimeisoma post yako Ngongo umejitahidi kuwa neutral lakini ,upo upande wa Lyimo.....Kuhusu Elimu ya Lema hicho siyo Kigezo kwa sababu katiba inamtaka mbunge ajue kusoma na kuhesabu tu so hapa hoja ya elimu ingawa ni mhimu lakini haina mashiko.......kama tatizo ni elimu nenda RORYA uta mkuta mtu anaitwa AILO huyu jamaa ni STD seven na alikuwa anajitangaza mwenyewe lakini uliza kamfanya nini Profesa bingwa wa mifupa Tanzania na Duniani Prof.SALUNGI...so wana Arusha huu ndiyo wakati wao kumchagua tena kijana wao Lema..kuhusu Swala la Mawazo kuhamia CCM hayanaa ukweli kuwa ni Lema ndiyo aliye mwambia ahamie CCM..sababu ifahamike Lema huyu huyu ndiyo alishiriki kumuapisha mwalimu Mawazo mbele ya viongozi wa Dini kuwa hata hama chama hii ni baada ya CCM kuanza njama za kumununua mwl.Mawzo..kama angekuwa amempeleka mwazo CCM kwa nini yeye hajahamia CCM??? huu ni wakati wa uchaguzi tuwe wakweli jamani...
ukitaka kujua kuwa jamaa antisha uliza ARUSHA chaguo lao ni nani this yr......Lakini naungana na Ngongo kuwa kama uchaguzi utakuwa fair basi BURIANI hanan chake....

Heshima kwako Bandorajr.

Nadhani ulikuwa umesafiri nje ya mkoa wa Arusha muda mrefu kwasababu unatetea vitu usivyovijua kabisa anyway siwezi kubishana na wewe kuhusiana na swala la Bwana Mawazo.

kuhusu elimu huwezi kuifananisha Rorya na Arusha hata kidogo,Arusha ni makao makuu ya EAC sitegemei iwakilishwe na mbunge mwenye elimu ndogo kama ya G Lema.Arusha licha ya kuwa makao makuu ya EAC pia ni kitovu cha utalii Tanzanaia,ni mji ambao mikutano ya kimataifa inafanyika kila wakati usisahau mahakama ya UNICTR na mahakama ya Afrika zote ziko ndani ya jiji la Arusha.Ukisoma post zangu zote bila kuruka utakubaliana na mimi CHADEMA imechemka kumsimamisha Lema ambae hata udiwani bado ni mkubwa sana kwake.
 
Back
Top Bottom