Kampeni ya kumchafua Mengi imeanza!

Ni upuuzi mtupu. Mengi anaandamwa bure tu na mafisadi. In my opinion bora wawepo akina Mengi 100 hapa nchini kuliko akina Rostam au Manji watano.
 
Wakubwa, kwa uzoefu bwna mkubwa mengi amekuwa na utaratibu wa kukanusha maneno yanayosemwa juu yake, mf. ndoa, ufisadi nk nk hili la kuhusika na mauaji ya albino amekanusha sijasikia au hajakanusha au ndo nyepesi nyepesi kuwa inahusisha n aile imani yake ingine zina kaukweli?
 
"Nikipiga picha tanzania ya baadaye machozi yananitoka...." Mh, Simbachawene...
hakuna ukuta wa kujengwa na matope unaoweza kuzuia mvua ya masika. utabomoka tu. Na hivyo mafisadi hawataweza kujificha kwa njia hizi za kitoto. kumbe hawa ni washamba wanalindwa na dola yenye kutumia ubabe. Mawazo yao haya wanayoyatumia sasa ya kuchafuana, ndio tunapata picha kwamba hata mawazo yao ya kuleta maendeleo ni hafifu pia. We are going to remain poor if we left these fake pasters in power.
 
simon,
Kwanini Masha?huo ndo uongo ..
Mbona kuna vikao vya siri vilifanywa na mengi na kina ole sendeka hatukusema?mengi amejiingiza kwenye siasa za majungu mwenyewe na mwisho wake ndio huu..asilalamike kabisa
 
Kwa mawazo yangu hii ni 'concoction' tuu, haina ukweli wowote.
Siungi mkono kampeni yoyote ya kumchafua Mh. Mengi.
Mengi ni mwema, anasaidia sana watu wenye shida mbalimbali na taasisi za kijamii zikiwemo zile za walemavu.
Ametoa ajira na mishahara minono kwa maelfu ya waTanzania kupitia familia yake IPP.
Sasa ameanzisha kamtindo ka kuwafadhili wabunge wote wa CCM walio mstari wa mbele kwenye vita dhidi ya ufisadi.

Nikiendelea kuorodhesha mema yote ya Mengi, hata JF yote haitoshi. Haya yote ni upande mmoja wa shilingi ambao ndio huwa unamulikwa kwa kupata priority media covarage, kwa kuimbiwa nyimbo za sifa na mapambio.

Kwa vile Mengi ni binadamu na sio malaika, lazima na yeye huwa anafanya makosa ambayo hayamulikwi. Wako watu wamepata manyanyaso ambayo hayaeleziki, toka kwa huyu mheshimiwa. Kuna michezo michafu anaifanya ambayo haizungumziki ila tuu ile anayochezewa yeye.

Mengi ni mdhalilishaji wa kiaina. Zile picha kama za harusi, hazikuleak kwenye media, ni posed photos zilizopigwa kwa madhumuni fulani ya kuwadhalilisha watu fulani ili aonekane kidume.

Wako watu wengi wenye mahusiano ya nje ya ndoa, tabia ya mhe. Huyu kufanya mambo hadharani tangu enzi za Madam Bongo Star Search ni kumdhalilisha mkewe ni hivyo kutia mashaka kuhusu his motives behind.

Kwa watu wenye bahati ya kuposses 'esp' na kumwangalia Mengi kwa jicho la 'the sixth sense' one can see some evil deep inside his smilling eyes. Hii ni kwa kutumia 'intuition' ambayo hakuna anayethubutu kusema ni nini haswa because its can not be explained.

Kwa kutumia 'law of the karma', utafika wakati hizi painted colors za Mhe. Mengi, zitafade away slowly with time, and 'the true colors' zitakuwa visible with naked eyes. Its only time that will tell.

'I fear the Greeks, especially when they bring gifts'.
 
Hizo ni shutma ambazo hazina kichwa wala miguu. Naona hili gazeti la sema usikike linajitafutia umaarufu kwa staili ya ajabu sana.
 
hapa ndipo watz tutajua kuwa, kuwaondoa mafisadi si kazi rahisi, inahitaji kujitoa muhanga. wanazo nguvu, wanazo pesa, wanao mtandao. tusiposimama kidete, hii nchi haitakuja ikombolewe hata siku moja. wale watu wanaowapiga mafisadi ndio matageti wakubwa, na ndio watu wanaopata matatizo.

Bwana mengi kama uko humu, nakupongeza kwanza kutoa mchango mkubwa kuwaumbua mafisadi. pili, nakupongeza kuwa hata wewe ubavu unao, manake hata wakipitia njia gani wanashindwa. sisi watz wapenda maendeleo na wachukia ufisadi tuko pamoja na wewe, na vita hii tutashinda kwa nguvu za Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo. Amin.
 
Back
Top Bottom