Kampeni ya kumchafua Mengi imeanza!

Superman

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
5,695
1,696
Wana JF;

Katika matangazo ya ITV leo asubuhi, tumetaarifiwa kuwa katika toleo la sasa la SEMA USIKIKE, pamoja na mambo mengine kuna habari zinazodai kuwa kumekuwa na vikao vya siri ambavyo vimeweka mkakati wa kusambaza habari katika Media kuwa Mengi anauhusika na kuwaua Maalbino na kutumia viungo vyao katika kufanikisha biashara zake.

Kuna chanzo kimoja kimenidokeza kuwa Mbunge wetu wa kuteuliwa Albino anazo taarifa hizo kuhusu mengi kuhusika na kuwa watu wake wa karibu wamemhakikishia.

Wadau hii imekaaje? Au ni katika muendelezo wa vita vya Ufisadi na kupakana matope kama SEMA USIKIKE linavyodai?
 
Last edited by a moderator:
Mzee Mengi naona umeandamwa kweli kweli je ni ishu gani umewakosea hawa haters?
Naona wamekuandama lakini ugomvi wa wanawake ndo iwa unakuwa hivi kama ni kweli tunayo yaskia kuwa unawaingilia vijana kwenye anga zao.
 
Mimi naona ni kama SIASA TU HIZO.HUwezi jua bwana pengine Mengi alitamani kuingia kwenye Siasa.Na akiingia huko huuyo ni PUBLIC FIGURE,lazima atahit sana
 
Proofs should be tabled for this allegation to Mr.Mengi
Mengi's is a victim to this so I could propose that for him to come up clean this mess.

Je viungo hivi anavitumiaje?Kwa kuviuza kama bidhaa au anatumia kwa njia za kishirikina?
We need to know about this too.
JE KUNA UKWELI KATIKA TUHUMA HIZI?
 
Uongo mtupu huu. Mnamwandama Mengi kwa nini?? Mafisadi mmekwisha. Mmeanzisha moto hamuwezi kuuzima. Tena msije mkamsingizia mbunge wetu issue kama hii. Unajua Mengi anaandamwa sana. Mafisadi wamo, vijana wamo, hasa wale aliowazidi kete kwenye ile ndoa na binti chawote iliyokanushwa vikali.
 
Siku hizi kuna watu wanalala wakiwaza kuchafuana, tutakuwa badala ya magazeti kutumika kuhamasisha maendeleo, yote yanatumika kwa minajili ya udaku. Sijui tunakoelekea, inachefua, hata kama ndio kukamiana kisiasa huku kumezidi, na sijui tunarithisha nini vizazi vyetu.
 
Unless ushahidi unatolewa, si busara kuichukulia hii issue kuwa ina uzito wowote. Mafahali wanapigana..wanachopigania kuna siku kitajulikana wazi.Ngoja tusubiri
 
Hii ni sawa na yaleyale ya kutaka kumflisi. kama kuna proof, kwa nini zisiwekwe mezani??
 
Uongo mtupu huu. Mnamwandama Mengi kwa nini?? Mafisadi mmekwisha. Mmeanzisha moto hamuwezi kuuzima. Tena msije mkamsingizia mbunge wetu issue kama hii.

Mbunge wa kuteuliwa na wananchi sio!?
 
Huyo mbunge umeongea nae au unataka kuja kujaza page za jamii?

Mengi anauzika kwenye forums, magazeti we endelea mzee wa watu ameapa hashindani na nguvu za giza tena! Kama pesa ni albino angeanza kuwa na mabillion waziri wako Masha

Lakini Mengi hawamuwezi jamani!
 
Wana JF;

Katika matangazo ya ITV leo asubuhi, tumetaarifiwa kuwa katika toleo la sasa la SEMA USIKIKE, pamoja na mambo mengine kuna habari zinazodai kuwa kumekuwa na vikao vya siri ambavyo vimeweka mkakati wa kusambaza habari katika Media kuwa Mengi anauhusika na kuwaua Maalbino na kutumia viungo vyao katika kufanikisha biashara zake.

Kuna chanzo kimoja kimenidokeza kuwa Mbunge wetu wa kuteuliwa Albino anazo taarifa hizo kuhusu mengi kuhusika na kuwa watu wake wa karibu wamemhakikishia.

Wadau hii imekaaje? Au ni katika muendelezo wa vita vya Ufisadi na kupakana matope kama SEMA USIKIKE linavyodai?

Brother, can you post that page please (SEMA USIKIKE)! Maana bila ya kuona hiyo siwezi kuchangia maada unless iondolewe kabisa hapa kwenye Forum
 
Brother, can you post that page please (SEMA USIKIKE)! Maana bila ya kuona hiyo siwezi kuchangia maada unless iondolewe kabisa hapa kwenye Forum

Wakulu msije mkanitoa roho . . . Mimi ni mjumbe tu wa kufikisha habari kama zilivyo na mjumbe hauwawi.

Kukata mzizi wa Fitina nimenunua gazeti na Ku-Scan. Here is a full Story:

MAFISADI WAPANGA KUMMALIZA MENGI

Source: Sema Usikike (Top Story), Jumatatu February 23, 2009 ISSN 0856 - 5414 No. 006 (Kama noma na iwe noma . . . !)

- Wafanya Vikao Usiku Kupanga Mikakati ya Kumchafua
- wapanga Kumhusisha na Mauaji ya Albino
- Wasambaza Vipeperushi Makanisani na Mashuleni
- Vitaandikwa kuwa Anafadhili Mtandao wa Madawa ya Kulevya Hapa Tanzania
- Kazi Hiyo Kuanza Hivi Karibuni
- Waandaa Vijana Watakaotoa Ushahidi wa Uongo
- Wadai Pia amemtoa Mwanawe Kafara Apate Utajiri

Mafisadi wapanga kummaliza Mengi

Katika ya kutaka kuzima kasi ya wenyekiti wa Makampuni ya IPP, Bw. Reginald Mengi ya kupiga vita ufisadi, baadhi ya mafisadi wamefanya kikao juzi usiku na kuamua kumchafua kwa kudai kuwa anahusika na mauaji ya Albino na kwamba amemuua mwanawe kwa - kumtoa kafara ili apate utajiri. -zilizopatikana katika kikao hicho, mafisadi hao wamepanga mikakati ya kuhakikisha wanammaliza Bw. Mengi na kumfanya anuke katika jamii.

“Lazima tuhakikishe kuwa tunammaliza na ananuka katika jamii. Si anajifanya mpiganaji wa wanyonge? Safari hii haponi”, akasema mwenyekiti wa kikao hicho ambaye jina lake linahifadhiwa.Kwa mujibu wa kikao hicho, mikakati inayoandaliwa ni kwamba mafisadi hao wamepanga kushirildana na baadhi ya waandishi wa habari kumuhusisha na mauaji ya albino hapa Tanzania iii kumchafua.

Taarifa zinasema kuwa mafisadi hao watasambaza vipeperushi mitaani hasa makanisani na mashuleni vildeleza jinsi Bw. Mengi anavyohusika na mauaji ya albino kwa sababu ya kutaka kupata utajiri zaidi.

Pia wamedai kuwa ili kummaliza Mengi vipeperushi hivyo pia vitaeleza jinsi alivyomuua mwanawe kama kutoa kafara ili utajiri wake uongezeke. Wamesema watafanya hivyo ili kuwaonyesha wananchi kuwa kama Mengi ameweza kumtoa mwanawe kafara, atashindwaje kuhusika na mauaji ya albino?

Uchunguzi Wa SEMA USIKIKE pia umepata taarifa za msiri wake aliyekuwa katika kikao hicho kuwa katika vipeperushi hivyo vitaandikwa jinsi Mengi anavyohusika na mtandao wa madawa ya kulevya na kwamba tayari mafisadi hao wamewarubuni vijana watakaotumika kutoa ushahidi wa nongo kumsingizia Bw. Mengi katika vyombo vya habari. Jnadaiwa kuwa vijana hao pia watatumika kumkandamiza Bw. Mengi kama suala hilo litapelekwa xnahakamani.

Kachero wa SEMA USIKIKE ambaye alikuwa katika kikao hicho amesema kuwa watu wote waliokuwa katika kikao hicho waliapishana kuwa atakayetoa ski ya mikakati inayoandaliwa atauawa kwa kupigwa risasi ama kusababishiwa ajali au kwa sumu.
 
Kumbe Mengi ni Mbunge wa kuteuliwa?..dang i didn't know that...

oops where is My cuzin Mzee mwanakijiji aje defend Mr Mengi here,kwi kwi kwi kwi.
 
Last edited:
mmh.. haya mapambano yanachukua sura mpya kila siku!

Mbona hawajasema kila kikao kinachodaiwa kufanyika ambapo mawazidi kadhaa wa JMT walikula njama kugawana mapato ya mradi wa vitambulisho? Au kile kikao kati ya Waziri Mkuu "wa zamani" na wafanyabiashara wa kiasia waliokutana kujadiliana juu ya kumuwezesha kurudi madarakani? Vipi kuhusu kikao kile kilichomhusisha mkuu wa nyumba na wasaidizi wake kuhusu kuuzima mjadala wa rada?

Wanajua kuna "vikao" vingapi vya siri.. ?
 
sawa sawa kabisa.....Mwanakijiji mzee mengi anaifatilia hii thread na anataka taarifa baadae....
 
Wana JF;

Katika matangazo ya ITV leo asubuhi, tumetaarifiwa kuwa katika toleo la sasa la SEMA USIKIKE, pamoja na mambo mengine kuna habari zinazodai kuwa kumekuwa na vikao vya siri ambavyo vimeweka mkakati wa kusambaza habari katika Media kuwa Mengi anauhusika na kuwaua Maalbino na kutumia viungo vyao katika kufanikisha biashara zake.

Kuna chanzo kimoja kimenidokeza kuwa Mbunge wetu wa kuteuliwa Albino anazo taarifa hizo kuhusu mengi kuhusika na kuwa watu wake wa karibu wamemhakikishia.

Wadau hii imekaaje? Au ni katika muendelezo wa vita vya Ufisadi na kupakana matope kama SEMA USIKIKE linavyodai?

Hamna mwenye uwakika kamili nadhani hii swala bado halijatulia kabisa.Na kwa nini awe mengi wasiwe wengine????Tuache mambo ya kupakaziana kuna wakubwa wangapi na wenye hela TANZANIA leo tuje tuseme MENGI ndio anahusika na hili swala kweli inakuja akilini hata wewe uliyeleta hii habari hapa jamvini unaona inakuja kweli?????
 
sawa sawa kabisa.....Mwanakijiji mzee mengi anaifatilia hii thread na anataka taarifa baadae....

true dat! si unajua lazima ripoti ifike mapema leo leo hazilali. Draft ya kwanza tayari nimeshamaliza. Lazima mzee afurahi.
 
Nashindwa kujua kama Taifa tunaelekea wapi,kila siku mambo yasiyokuwa na msingi,,,ni lini tutakuwa wazalendo wa kweli?pia tujue mambo yote yanapita ila utaifa wetu utabaki daima,tufike mahali tuwe na mijadala yenye maana na si ugomvi usiokuwa na misingi.Inawezekana kila mmoja atimize wajibu wake,,,,,,,,,,,
 
Back
Top Bottom