Kampeni ya Kuirudisha UDA mikononi mwa wananchi; Haja ya Mfumo Bora wa Usafiri Dar

Kuna watu bado wanazungumzia mambo ya UDA; mwenzenu sijui kwanini najisikia kuboreka..

....hahah....though natambua unachomaanisha....lakini kwa jinsi neno hilo linavyojaribiwa kutoholewa na wazungumzaji wengi wa siku hizi.....linaleta utata!....hivi tafsiri ya neno "bored" kwa neno sahihi la kiswahili ni "kukereka"?......wajuvi wa kiswahili......Please help....
 
watanzania nimejua ni washenzi sana, badaya kumuunga mkono mtanzania mwenzetu tunaanza kumpiga ngwara. dowan ilipigiwa kelele kaja yule cia mstaafu wote kimya ananyonya kiulaini huku bili za umeme zikizidi kushamiri! nmb yuko mholanzi hatuulizi tena, kikwete muuzie obama hili kampuni tumalize uswahili.
 
You are right!.......unajua nimesoma hiyo statement yako...na kujiuliza maswali kadhaa.....sijui ujasiri wa kuonyesha ghadhabu kama tunao.....sisi ni waoga sana.....kwa jinsi tulivyo wabongo Polisi mmoja anaweza kutuliza au kutetemesha kundi kubwa sana la watu au hata kufanya vitendo vya uonevu huku wengine tukiangalia bila kufanya lolote.....kwa mfano Polisi kupiga makofi watu, au kumpiga "mtama" mtu.......au kusakiziwa kesi/kidhibiti....Polisi wetu wanatufanyia hivi vitu kwa sana tu....tena mchana kweupe lakini sisi tulio wengi tunabaki kuangalia tu......

Juzi juzi kule Zimbabwe kuna kikundi fulani kimewashughulikia Polisi mpaka basi....Polisi walikuwa wanatoka mbio hakuna mfano.......Well.....while I do not condone the act.....the fact remains ni Utu, sheria na haki kwa kila mwananchi.....si sahihi kunyanyasa wananchi......na shughuli zao.....matumizi ya nguvu za Kipolisi inabidi yawe defined kw awananchi na yawe very clear...sio kupiga tu...kama anavyosema Mh Pinda.....ambaye tutapambana naye mahakamani kwa mambo kadhaa.....kutokana na kauli zake......

Tukirudi kwenye somo la Mada....kusema ukweli uuzwaji wa UDA...wananchi tumenyimwa/tumeibiwa/tumefisadiwa haki yetu.......
Mkuu kinacho kosekana ni coordination tu! Imagine UKAWA plus wabunge wa Dar es Salaam wakiamua kuitisha Mkutano wa hadhara kwa kuongoza maandamano kuelekea Ikulu! ... Lazima tutambue kuwa haki ya kuandamana na kufanya mikutano iko kisheria kwa vyama vya siasa, kwanini hawa take full advantage? mimi sielewi mpaka kesho...
 
ulichelewa sana ulikuwa wapi enzi za simba shirika likiwa na mabasi 5 na madeni lukuki? hapo ndo ungeonyesha uwezo wako na uzalendo.sasa ni kucheza ngoma usiyoijuwa watu wamekaa vikao vya kuuza na posho wakatia mfukoni leo wanajiita watoto wa dar wanaitaka uda yao nyie mnatoa macho, waulizeni kwanza kwanini waliuza?
 
UDA UDA UDA naona dart watu wameanza kuivutia kasi sasa, hakuna kitu hapa mwanakijiji kesha pata fungu lake anakula taratibu halafu anakuja kujaza hasira wanainchi, kama kweli mwanakiji angekuwa na uchungu na hii tanzania kwa nini akaishi nje ya Tanzania? Acha kutupotezea muda wetu bana na stori zako, kama kweli kama unamachungu na nchi mbona kuna mambo mengi tu, kwa nini UDA?
 
Utangulizi
Tulipoanza kampeni ya kurudisha kampuni ya Kiwira mikononi mwa serikali watu hawakuamini kama inawezekana. Kwa wanaokumbuka kampuni hiyo ya makaa ya mawe ambayo kuendelezwa kwake kungesaidia sana kupunguza tatizo la nishati ya umeme nchini iliuzwa kinyemela kwa viongozi wa serikali miongoni mwao ni familia ya Rais Benjamin Mkapa na aliyekuwa Waziri mwenye dhamana ya Nishati na Madini Bw. Daniel Yona.

Tulipoanza kampeni ya kuidai Kiwira irudishwe watu wengi wanafikiri tulikuwa tunafanya utani. Tulianza kampeni hiyo mwaka 2007 na niliandika makala kwenye gazeti la Kulikoni wakati ule isemanyo Mkapa, Yona wanyanganywe Kiwira. Hii ilikuwa ni kabla wabunge hawajaanza kupigia kelele Bungeni kutaka Kiwira irudishwe serikalini. Ilituchukua muda na wengine walidhani tunafanya utani au ilikuwa ni jitihada ya bure lakini pole pole watu walianza kuamini tunachogombania siyo utajiri wa Mkapa au Yona bali urithi wetu na ule wa watoto wetu. Hatukutaka kuona mali ya wananchi wa Tanzania inapigwa rehani.

Kutokana na suala hilo tulijifunza vitu kadha wa kadha mojawapo ni kuwa sera yao ya ubinafsishaji wa mashirika ya umma japo kinadharia ilikuwa nzuri lakini imetengeneza mabepari waporaji ambao hawataki kuingiza uwezo na fedha zao katika kuanzisha miradi yao bali wako tayari kama kupe kudandia miradi ya watanzania! Tulitambua kuwa ubepari ambao tuliukataa toka mwanzo wa taifa letu umerudi kwa nguvu kwa jina la uwekezaji na safari hii siyo kutoka kwa watu kutoka ngambo bali kutoka kwa watu wetu wenyewe!

Tukagundua kuwa bila kuwakataliwa watawala wetu wanaweza kuuza kitu chochote na kwa sababu yoyote. Na ndio maana naamini kuwa endapo Watanzania wataamua kukaa pembeni na kupiga makofi tu bila kuhoji au hata kukataa wanaweza kujikuta wanaamka siku moja kama waliokuwa kwenye usingizi mzito wakiulizana ni lini taifa lao liliuzwa jumla?

Sakata la UDA ni suala la namna hiyo. Bila ya mgogoro wa fedha uliojitokeza kati ya wahusika na mchakato, UDA ingeuzwa kinyemela na wananchi wasingejua zaidi ya kusikia tu shirikia limebinafsishwa. Hakuna wa kuhoji hakuna wa kulalamika. Kama wahenga walivyosema mchawi hawi mchawi hadi mtoto wa kwake aliwe! Baada ya wahusika kuanza kuzungukana ndio tumegundua kuwa wachawi wengine hawatoki nje, ni sisi wenyewe.

Hivyo basi, kampeni hii ina kusudio moja tu la kwanza nalo ni kurudisha UDA mikononi mwa wananchi na kutoka hapo kufikiria namna gani shirika hilo na lile la Mabasi Yaendayo kasi yataweza kuunganishwa ili kutengeneza mfumo wa kisasa wa usafiri wa mabasi ya umma jijini Dar na yawezekana kuigwa katika mikoa mingine vile vile.

Kwa wengine wameona kuna habari kubwa kama vile ni mpya... kumbe tulishakuwepo hapa ni marudio tu.. swali siyo lile unaloweza kulituhumu bali lile unaloweza kulithibitisha...
 
Back
Top Bottom