Kampeni ya Kuirudisha UDA mikononi mwa wananchi; Haja ya Mfumo Bora wa Usafiri Dar

Mikononi mwa serikali?mimi nilijua hapa tunakampeni na mashirika mengi zaidi wapewe wazalendo wayaendeshe? kama kuipeleka UDA serikalini mimi siafiki waungwana. Naona nyie mmesahau maneno ya wanafalsafa kuhusu Private V public property. UDA kuwa ya serikali Hellllll NOOOOOOO!!!

Umesoma wapi tumesema irudishwe mikononi mwa serikali tu kama ilivyo?
 
Nakubaliana nawe kuwa wamiliki wa dala dala ndio wasimamizi washeria na ndio wavunja sheria.
Kuondoa vipanya na coaster hakuhitaji msuli, ikiwepo huduma nzuri na ya kisasa zitakufa kifo cha asili.
Kwamba dala dala zinapunguza vibaka,sijui ni takwimu gani zimetumika kujua kuwa wakati wa UDA kulikuwa na vibaka wengi kuliko sasa.

Shirika kama UDA liliajiri mamia ya watu kuanzia madereva wa shift, makondakta, wafanyakazi wa depot n.k idadi yao ni kubwa kuliko dei waka wa dala dala.Lakini mbona hujaongelea usalama wa abiria? Ni mara ngapi ulisikia UDA imeua au imekata watu miguu.

Kulipa kodi inategemea unaliangaliaje suala zima. Usafiri wa umma ni huduma ya jamii inayomwezesha mwananchi kutoka sehemu moja hadi nyingine iwe kwa shughuli za kijamii au kiuzalishaji. Inaweza kuwa huoni kodi inapatikana wapi lakini ni zaidi ya kodi za dala dala, ndio maana duniani kwenye miji mikubwa usafiri wa umma ni huduma ya lazima kama hospitali, ambulance n.k.

Kama inapunguza ufisadi tujiulize wamiliki ni wangapi? yaani ni bora kuwaonea huruma wamiliki 50 kwa gharama ya wanachi mamilioni wanaoishi jijini na wanaotembelea jiji. Na sheria za nchi ziliwekwa za nini kama tunaweza kudhibiti ufisadi kwa kuwaongezea mafisadi ufisadi.

Tunauwezo wa ku manage, UDA ipo tangu mwaka 1974 na ilifikia wakati utaratibu wake ulikuwa unaeleweka kuanzia muda,usalama n.k
Tatizo hatuangalii kwanini precision ifanye vizuri ATC ife, kwanini dala dala zifanye kazi kwa faida UDA ife!
Unapokuwa na mwenyekiti wa bodi mwenye historia chafu unategemea ufanisi utoke wapi.

Wamiliki wa dala dala na walafi kama wauza UDA usidhani wanaweza kufurahi UDA ikiimarika.

Nakubaliana nawe kuwa haikuwa sahihi kuuza UDA na kuanzisha 'UDA kwa jina la DART' lakini nadhani ipo hekima ya kuifanya UDA iwe mshiriki wa DART, je tumewekeza kiasi gani ili iwe mshiriki kamilifu?

Na mwisho, kwa miaka 25 iliyopita kipi kimefanywa na dala dala tunachoweza kujivunia zaidi ya vurugu, kukata ruti, usalama pungufu n.k.


Du mkuu moja ya mambo ambayo kamwe sitasahau kuhusu UDA ni kuwa ilikuwa na madereva wa kweli, ambo siku hizi hakuna kama wapo ni wachache sana. Tatizo ni lile alilosema Nyerere tunatupa vizuri tunakumbatia vibaya, system ya madereva wa UDA ilitakiwa kuendelea.
 
Mwanakijiji,
Nadhani unatambua malalamiko yangu kwako wakati wote, kwamba umebeba agenda nyingi sana at pa.
hofu yangu ni kwamba sina hakika kama na wewe agenda zoooote hizi umezielekeza kufikia lengo moja
sababu hofu hii kwa watanzania wengine (common tanzanians) ni obvious.

Sina shaka na makubaliano ya kimsingi yaliyo hapa Jamvini kwamba serikali inayoongozwa na chama
cha mapinduzi ni bogus governement, haina uwezo wa kusimamia jambo lolote likapendeza, ndio maana
hata baada ya yenyewe kujiona kwamba haiwezi kusimamia mashirika ya kibiashara yaliyo chini yake,
ikaamua kuyabinafsisha, wonderfully hata hilo zoezi la ubinafsishaji wameliendesha na wanaendelea kuliendesha
kibogus zaidi.

Hoja yangu ni kwamba, Mashirika haya yasibinafsishwe badala yake tuiondoe serikali iliyopo madarakani,
tuweke serikali imara ambayo inaweza kusimamia mashirika haya kwa ufanisi, na hata ikiamua kuendelea
na ubinafsishaji basi iufanye kwa ufanisi, kwa maana ya kwamba kwa faida kubwa zaidi kwa uma wa watanzania.

Kwa hiyo kilio changu ni kwamba, tuelekeze agenda zoote hizi kwenye regime change.

Asante kwa kunisoma
 
tayari sekta "binafsi" inaendesha asilimia 90 ya usafiri wa watu jijini dar.. kuna ufanisi? kwanini kwa karibu miaka thelathini hatujaona hicho kinachoitwa ufanisi wa sekta binafsi ambao tuliambiwa ungekuja kutokea kwa sababu ya ushindani wa soko huru?

Mkuu unadhani hakuna anyejua hilo? Tatizo ni uroho, wizi, na ubadhilifu. Hizi ni dhambi zinatutafuna, zitae4ndelea kututafuna sana!! Hakuna ndani ya serikali ya CCM asiyejua kuwa railway ni moja ya stimulant ya kukua kwa uchumi, lakini huwezi amini, ni hao hao ndo wanaochichea kufa kwa TRL ili magari yao ya mizigo yapete...

Shime wana JF, ukisoma kampeni ya MKJJ, mwisho kuna barua ya kutuma kwa wabunge wetu, shime tufanye hivyo ili lengo la kwanza tulitimize, turudishe UDA mikononi mwetu!!!!

Naunga mkono hoja ila, ubinafsishaji wa UDA ufanywe kwa uwazi lili wadau na wamiliki wote wake tununue kwa uwazi!!! Si haya ya fedha kuwekwa kwa account ya mtu binafsi kwa kisingizio cha overdraft....my foot!!!
 
Watanzania inabidi ifike wakati tuangalie na kufikiria mbali na tujiulize haya yafuatayo then tusonge mbele.Tuangalie tatizo ni nini kama ni management au Serikali.Na kama ni Serikali tufanyeje kama ni management tufnyeje.Suala sio kubinafsisha suala ni kuangalia chanzo cha matatizo ni nini.Kwa hali iliyopo unaweza kuwpa watu ambao ni wahujumu wa nchi mfano mzuri ni kisena
 
Kuna watu wanajua sana kukwepa miamba. Wanafuata tifutifu tu. Ardhi ni mchanganyiko wa udongo, mchanga, mawe, masalia, hewa, maji, n.k. Hiyo tifutifu ina ukomo
 
Kuna watu bado wanazungumzia mambo ya UDA; mwenzenu sijui kwanini najisikia kuboreka..
 
Tatizo la HOJA YAKO MMJ ni kwamba mnapendekeza kumuadhibu SIMON GROUP kwa makosa yaliyofanywa na Viongozi wa Serikali/JIJI la DSM kwa kumuuzia UDA bila kufuata utaratibu. Kama kweli Simon Group ataamua to PLAY A HARD BALL I mean kulipeleka hili suala mahakamani, itawachukuwa sio chini ya miaka 5 mradi wa mabus yaendayo kwa kasi kuanza Dar! There is a lot of water has passed through the bridge between Simon Group and the Government of URT and Dar City Council. If history has anything to go by, the Government will be defeated in the court of law and Simon group will be rewarded a hefty billions of money as a compensation. Kama serikali inataka KUFICHA AIBU yake ni kulimaliza suala hili nje ya mahakama. That means lazima makubaliano kati ya Serikali/City Council na Simon Group on the other hand.
 
Nakuunga mkono irudi nakumbuka siku ambayo Simon group imenunua hisa za serikali kinyemela wa andishi walikwenda pale UDA siku hiyo awakupewa ushirikiano wowote kilichofanyika no pesa zilitembea na waandishi wakaondoka bila kupata taarifa yeyote. Yani kisena name masaburihawa ni watu hhatari.
Nakumbuka mpaka bujugu alikosana na masaburi na mpaka kutishiwa maisha na wanaojiona kuwa wana akili kuliko watanzania wote
 
This is a good movement! Ila wasiwasi wangu ni kama wa mchangiaji Bishop Hiluka kuhusu watu watakaopewa dhamana ya kulisimamia hilo shirika.Nadhani watakuwa ni wale wale ambao wamelifikisha hapo lilipo.

Ndo inabidi tutoe solution ya nani akabidhiwe hasa
 
Unataka kuleta mambo ya Ujamaa tatizi halio UDA ni viongozi wetu wanavyogawa hizo tenda. Tuliona siku za nyuma wananchi walipewa mpaka maduka ya kuuza nyama sasa ni wakati wa ushindani wa kibiashara, ila sema tuna tatizo sasa katika kila secta ya uongozi Tanzania ikiwemo polisi, wafanya biashara wanaachwa wafanye wanayotaka kwasababu baadhi vyombo vya usafiri vinamilikiwa na viongozi wa serikali kwahiyo wao wakivunja sheria wengine wanafuata na wanaona kawaida.
 
Polesana ndugu nadhani hukumsikiliza Malima Vizuri, Mimi nilimsikia na Nikastuka sana na inaonekana wengi hawakustukia ile kauli pengine ilimtoka bahati mbaya. Malima alisisitiza kuwa Simion hajanunua Hisa za Serekali na kwamba walimuita halete ushahidi na ushahidi alikuwa hana. Na pia aksema kuwa soon baraza la mawaziri litakaa na kupitisha/kuidhinisha uuzaji wa hizo hisa za serekali kwa mwekezaji mwenye uwezo. Na hapo nyuma alishasema kuwa serekali haito anaglia kama ni mzawa au wa nje, as long as anauwezo basi atapewa hizo hisa. Je unategemea Simion atazikosa hizo hisa?
 
Unataka kuleta mambo ya Ujamaa tatizi halio UDA ni viongozi wetu wanavyogawa hizo tenda. Tuliona siku za nyuma wananchi walipewa mpaka maduka ya kuuza nyama sasa ni wakati wa ushindani wa kibiashara, ila sema tuna tatizo sasa katika kila secta ya uongozi Tanzania ikiwemo polisi, wafanya biashara wanaachwa wafanye wanayotaka kwasababu baadhi vyombo vya usafiri vinamilikiwa na viongozi wa serikali kwahiyo wao wakivunja sheria wengine wanafuata na wanaona kawaida.

Unaonaje Mfumo wa NMB Bank ? Serekali iliuza hisa kwa Mwekezaji na zingine zikabaki mikononi mwake na mwisho wa siku zikauzwa kwa wananchi na mpaka leo bado serekali ina hisa 10%, Hivi unajua karibu mabenki yote makubwa nchini yanahisa NMB zisizopungua kila mmoja 5%. Kwanini Simion apewe asilimia 100 ? Si tayari ana 51% za Halmashahuri? Anashindwa nini kuendelea na kuwekeza huku akigawa salio na gawio kwa serekali ?
 
Hizo hisa 49% zimerudishwa kuondoa matatizo mbeleni kwa mwekezaji, bazara la mawaziri litahalalisha Aljeezera watapewa chao kilichobakia.
 
watu wameichukuwa kwa million mia mbili then wakaipiga mnada kwa billion 13
 
ni wazo zuri lakini jaribu kuangalia kama kuna urahisi wakurudisha vinginevyo kampeni itakuwa ni kupoteza muda wa kutafuta ada za wanao
 
Only Ghadhabu za wananchi ndizo zitakazorejesha UDA ....

You are right!.......unajua nimesoma hiyo statement yako...na kujiuliza maswali kadhaa.....sijui ujasiri wa kuonyesha ghadhabu kama tunao.....sisi ni waoga sana.....kwa jinsi tulivyo wabongo Polisi mmoja anaweza kutuliza au kutetemesha kundi kubwa sana la watu au hata kufanya vitendo vya uonevu huku wengine tukiangalia bila kufanya lolote.....kwa mfano Polisi kupiga makofi watu, au kumpiga "mtama" mtu.......au kusakiziwa kesi/kidhibiti....Polisi wetu wanatufanyia hivi vitu kwa sana tu....tena mchana kweupe lakini sisi tulio wengi tunabaki kuangalia tu......

Juzi juzi kule Zimbabwe kuna kikundi fulani kimewashughulikia Polisi mpaka basi....Polisi walikuwa wanatoka mbio hakuna mfano.......Well.....while I do not condone the act.....the fact remains ni Utu, sheria na haki kwa kila mwananchi.....si sahihi kunyanyasa wananchi......na shughuli zao.....matumizi ya nguvu za Kipolisi inabidi yawe defined kw awananchi na yawe very clear...sio kupiga tu...kama anavyosema Mh Pinda.....ambaye tutapambana naye mahakamani kwa mambo kadhaa.....kutokana na kauli zake......

Tukirudi kwenye somo la Mada....kusema ukweli uuzwaji wa UDA...wananchi tumenyimwa/tumeibiwa/tumefisadiwa haki yetu.......
 
Back
Top Bottom