Kampeni ya Kuirudisha UDA mikononi mwa wananchi; Haja ya Mfumo Bora wa Usafiri Dar

<br />
<br />
hata sijaisoma. Nimetazama mdahalo nikapata picha ya kutosha. Kawajibu vya kutosha. Tumeshaambiwa kuwa uda ilianza kufa pale biashara huria iliposhika kasi. Kuna mashirika ya kuhodhi kama tanesco n.k. Sio hili . Labda mseme likisharudi serikalini nini kitabadilika. Huu usanii wa mikataba mmeufahamia uda? Ilianzia kwa chief mangungu. Sio kama napenda usanii ila kwa nini uda? Au la uda ni rahisi ku deal nalo kuliko tics, migodi, n.k. Mbaya zaidi kiwira ilichukuliwa na wazalendo. Uda nayo wazalendo. Kwa nini kampeni kwa mashirika na makampuni yaliyochukuliwa na wazalendo? Nasema tena siafiki ubadhirifu kufanywa na mzawa. Kwa nini kampeni dhidi ya wazawa? Niko huru kukosolewa pia

Sio kampeni dhidi ya mzawa, hoja iliyoo hapa ni kuwa Kisena kauziwa nyumba na asiye mmiliki wa nyumba husika. Hivyo umiliki wake una utata. Toka lini Bodi ya wakurgenzi iliyowekwa na wanahisa kusimamia shirika kama UDA ikawa na madaraka ya kuuza hisa za Shirika husika?
 
Basically Mimi binafsi naiangalia Dar katika Public transport na kuona kuna kitu kinatakiwa kifanyike lakini bado hakijafanyika!! Sijajua ni nani anatakiwa asimamie Hiki!! Hii yote inatokana na kuwa na taasisi nyingi ambazo hazijui Majukumu yake kuhusu kuboresha masuala ya public transport na mwishowe kuwa ni full Confusion (Nasikitika) Ili Kufanya maboresho haya naona serekali haitakiwi kujitenga na Hili!! kwani hili suala linahitaji planning , implementation , monitoring and transfer to private ownership by shares!!
Sasa unakuta Tanroads inasema hii barabara ipo katika Himaya yangu!! That is fine!! Ila je itakapojengwa itahusisha Planning ya all stake Holders? Hasa kwa jiji la dar (Public transport Needs??????) Unakuta yote Hiyo haipo!! Unakuta manisipaa through Jiji ndio wamechoka na Hawana Any plans!! Sasa Tanroads wanajiamulia Kutokana na Matakwa Yao!! SASA NAJIULIZA NANI WA KULIKOMBOA HILI JIJI LA DAR? Halmashauri? Jiji? Sumatra? Tanroads? Private sector (Daladala?????) UDA (Kisena!!!!!) DART?? AU NANI SASA? Just I can say is full confusion
NAPENDA SEREKALI IANZISHE KITU KINAITWA (DAR ES SALAAM PUBLIC TRANSPORT NEEDS) NA WAPEWE MAJUKUMU YA KUSHUGHULIKIA USAFIRI WA PUBLIC KWA UJUMLA WAKE!!
 
Big up MMJ, na tunashukuru kwa kutujuza taarifa hizo na kwa kutupa way foward, Ila inasikitisha sana kuona nchi yetu inatafunwa kiasi hicho na WAHUNI wachache ambao tumewapatia dhamana ya kiuongozi na wao wamebadilika na kuwa MIUNGU watu.
 
Bongolander; inawezekana uko sahihi kweli na mimi siamini katika kurudisha UDA kwa watu hawa hawa na mtindo huu huu. Naamini ikirudishwa lazima uje mfumo mzuri wa kulisimamia na kuliendesha. Lakinin hili linahitaji uongozi na kiongozi mwenye maono. Yule Meya wa Bogota aliyeingiza hiyo public transportation alifanya kitu ambacho hakikudhaniwa kuwa kinawezekana.. tatizo sijaona bado kiongozi TZ mwenye maono na uwezo wa namna hiyo ; angalia tu wanavyosumbuka na suala la nishati ndio ujue tulivyo na kazi.

Mwanakijiji mara nyingi tunapojadili issue zinazohusu nchi yetu huwa hatupigi nyoka kwenye kichwa. Tunajadili kama vile hatui tatizo ni nini, tatizo ni kuwa siasa ziko above evrything, tuneweka watu wasiostahili kwenye ofisi zetu, kuna walioingia kwenye nyadhifa kwa kupewa tu, na kuna wengine hata hawajui wapo kwenye nyadhifa zao kufanya nini. Wenye uwezo wanaadhibiwa kutokana na kufanya kazi kwa uwezo wao na taaluma inavyotaka [Tido Mhando should be the reference] As a result mfumo mzima wa uendeshaji wa kila kitu umekufa. We have serious structural problems in Tanzania, unless we address them (we are currently doing nothing we are doing more to make things worse) we are not going to change the status quo. Kama kungekuwa na working systems za kushughulikia mambo tunayoona ni matatizo u tungekuwa tunajaribu, ingekuwa rahisi sana kuendesha UDA, KAMATA, RETCO, KILTEX, TIPPER etc etc. Mpaka sasa TANESCO imetushinda kuiendesha, zamani tulikuwa tunasema mashirika yametushinda kuendesha, kwa sasa it even worse, hata wizara ya nishati na madini imetushinda (mifano ipo mingi tu) tukiibinafsisha itakuwa much better. Angalia mambo ya muhimu kabisa, umeme, maji, msongamano wa magari vimetushinda. What can we manage?

We should remember that privatization came under pretex of massive mismanagement, embezzlement of public funds which is still blessed by seniors. We unaona wazi kabisa civil servant anafanya kosa ambalo ni wazi kabisa kuwa ni kosa...rais anasema subirini nije kushughulikia mwenyewe. Don't we have a system in place to deal with this kind of issues? jibu ni kuwa we do not, if we had asingefanya hivyo. Unaona kabisa kuna wezi na kuna kila ushahidi wa kuwachukulia hatua, lakini hakuna kinachofanywa. How do we explain this? Tuna system mbaya, ambayo akija mtu mwenye akili, inakuwa system yenye akili akija mjinga system yote inakuwa ya kijinga, angalia awamu zetu zote nne za utawala in this context. Then utajua kuwa tatizo si Nyerere, Mwinyi, Mkapa au JK, it is much bigger than that. Bado hatuna watu wanaoweza kudischarge duties zao kama wanavyotakiwa, kwa kuwa waliingia kwenye nyadhifa hizo kwa sababu ya dini zao, jinsia zao, vyama vyao na urafiki na wa waliowateua, si iwezo wao.

Kuna wakati nilikuwa nasema usafiri Dar es salaam ni holela sana kama nchi yetu ni Somalia vile, lakini i changed my mind na kuona uholela uliopo unasaidia kupunguza wizi wa mali za umma, public transport Tanzania ingeendeshwa publicly ingekuwa kiliko kila siku. Tanzania ni kuwa hatuna uwezo wa kumanage public property, whether we like it or not, we must admit. I said before, i am saying it now and i will say again and again, BRT ni bomu, utakuwa ni wizi na ubabaishaji tu. Mfano wa Colombia ni mzuri sana lakini unatakiwa uangalie jamii ya Bogota inavyobehave, na uangalie local government sytems za Colombia zinavyofanya kazi, then ulinganishe na Dar. Tell me kama ulisikia wanatukanana kwenye media au hata out of media. Hapa unaweza kuona wazi kabisa kwanini BRT inaweza ku-work Bogota and it will never work in Dar.
 
Jamani nyie mnaodai shirika lirudi, je mipango gani hai ipo ya kufufua hili shirika???bajeti ya wizara husika imesomwa tayari je kuna nini jipya la kusaidia kuinua shirika hili??? ni kweli watanzania tunakwamishana wenyewe kwa wenyewe?? unasema shirika lirudi sawa lakini ungetoa mchanganuo yakinifu ukirudishwa then shirika litajiendeshaje! naomba utudokezee na hapo na capital ya kuweka kuinua shirika inatoka wapi??plesae ainisha!

unajua wawekezaji sio watu wa kuamini sababu anapoingiza pesa zake anatehemea returns out of it, ila sometimes, uwekekezaji umekuwa mwiba kwa taifa la tanzania kulingana na aina ya mikataba ambayo viongozi wetu wamekuwa wakisaini!ila kama mkataba ni mzuri na sheria zote zimefuatwa sidhani ka kuna matatizo! cha msingi wadau wanufaike na mkataba na si vinginevyo!
 
UDA ilishakuwa na mabasi makubwa ya trela yaitwayo IKARUS ,sijui yameishia wapi au wameyarudisha walikoyanunua,kama yamekufa si tungeona hata scrap zake? mbona hatuelezwi yako wapi.
 
uda -ni sehemu tuu ya ufisadi mkubwa uliopo ndani ya Taifa letu....kuna haja ya kushughulika na tatizo la msingi ili tuachane na kushughulika na tatizo moja moja . Ila ni kampeni nzuri naiunga mkono.
 
Jamani nyie mnaodai shirika lirudi, je mipango gani hai ipo ya kufufua hili shirika???bajeti ya wizara husika imesomwa tayari je kuna nini jipya la kusaidia kuinua shirika hili??? ni kweli watanzania tunakwamishana wenyewe kwa wenyewe?? unasema shirika lirudi sawa lakini ungetoa mchanganuo yakinifu ukirudishwa then shirika litajiendeshaje! naomba utudokezee na hapo na capital ya kuweka kuinua shirika inatoka wapi??plesae ainisha!

vizuri sana; lakini na wewe si una uwezo wa kufikiria ndugu yangu? unafikiri tunaweza vipi kuliendesha UDA kama shirika la Umma?
 
vizuri sana; lakini na wewe si una uwezo wa kufikiria ndugu yangu? unafikiri tunaweza vipi kuliendesha UDA kama shirika la Umma?
Mkuu wangu sijui kama unakumbuka.. Mwaka 2001 niliwahi kuzungumzia kurudishwa kwa UDA nilipigwa vita vibaya sana ktk janvi la jamboforums au bcstimes... wakisema hawataki kurudi nyuma ktk matumizi ya UDA wakati daladala zinawatosheleza. Nikaeleza uzuri wa UDA as a system ya kileo kabisa ktk usafiri kwa sababu inatumika hadi nchi zilizoendeelea.. Wapi wadanganyika wakalia na Daladala kumbe wamewekeza mitaji yao ktk hizo daladala..

Tatizo la Watanzania ni kwamba pale penye UZEMBE wao huadhibu shirika ambalo halina makosa kabisa!.. Sisi ndio tuna lack uwezo wa kuongoza kunakosa kuwa responsible na accountable tunalihukumu shirika ambalo watu wale wale walioshindwa kutokana na Ufisadi wao ndio tunawapa mamalaka ya kuuza au kulinunua..

Sasa Leo mji wa dar umefurika magari Usafiri shida na hizo daladala bado hazitoshi ndio wanaona faida ya kuwepo public transportation..Gari moja kama IKARUS lilikuwa na uwezo wa kuchukua watu zaidi ya 70 sawa na daladala nne au tano wakati bus la kawaida linachuku mara mbili ya daldala..Kifupi Tungepunguza Nusu ya magari yaendeshwayo barabarani leo hii kutokana na kuwepo usafiri wa UDA. Lakini maadam ni mradi wa kutokea watu wanaupigia mahesabu mapyaaa!.
 
Mkandara, Meya wa Jiji la Bogota Colombia aliamua kutengeneza mfumo huu wa mabasi ya umma ya kisasa kwenye jiji lilikuwa na daladala kama za kwetu na ndani ya miaka michache tu daladalal kama 9000 hivi zimeondolewa na sasa mabasi ya kisasa yanaranda kwenye hilo jiji. Mzee katika hili ulikuwa mbele sana ya wakati na bado unaona miaka kumi baadaye magenius wetu wameamua kuliuza kabisa.
 
Tena kweli ebu unaweza nipa hesabu ya daladala ktk jiji zima la Dar zinaweza fika ngapi?
 
Sheria zote zinazohusu udhibiti wa daladala Tanzania zinavunjwa na watunga sheria au wasimamiaji wa sheria,kwa kuwa wao ndio wamiliki na wenye uwezo wa kupindisha sheria bila kuchukuliwa hatua. Kuondoa vipanya na macoaster si jambo gumu kama sheria zikifuatwa, lakini kamwe hazifuatwi. Ukiangalia kwa undani unaweza kuona daladala kwa Dar is political issue, inapunguza vibaka, wanalipa considerble amount ya kodi kwa serikali, inapunguza unemployement na kwa kuwa sehemu kubwa ya wamiliki ni wazito naweza kusema inapunguza hata ufusadi.

Once DART ikiwa operational inabidi ujiandae ku-deal na unrest itakayotokana na kuviondoa vipanya. I.e wizi mkubwa kwenye DART yenyewe, uhalifu,kupungua kwa kodi and somekind of political unrest.

Tunatakiwa kwanza tuoneshe uwezo wa kumanage hizi daladala tulizonazo barabarani sasa. Tusiwe new project mania halafu tukashindwa. tunarudi kule kule tuweke mfumo mpya wa kumanage mambo yetu.
 
Tena kweli ebu unaweza nipa hesabu ya daladala ktk jiji zima la Dar zinaweza fika ngapi?

ziko kama 9000 hivi kati ya hizo ni zaidi kidogo ya 3000 ndizo zimesajiliwa na SUMATRA.. na kati ya hizo zote 90% zina umri wa zaidi ya miaka 10 barabarani!
 
ziko kama 9000 hivi kati ya hizo ni zaidi kidogo ya 3000 ndizo zimesajiliwa na SUMATRA.. na kati ya hizo zote 90% zina umri wa zaidi ya miaka 10 barabarani!
Damn ama kweli tanzania nchi ya Mitumba. Ndio maana Zitto alitetea sana mitumba wakati fulani akijua hali halisi ya Matanzania..
Hakika, Nyerere was a Gunius!..
 
Watu aina ya kina Idd Simba hawana msaada wowote kwa nchi yetu. It is time now they must go! Wafunguliwe mashitaka wahalifu wote wa sakata la uda bila kujari ni kina nani. Mambo yakiachwa yaende ende hivi, tunakaribisha hatari kubwa mbele yetu
 
Mkuu Tangawizi, Tanzania wanaofunguliwa mashataka ni wale wasio tatizo kwa nchi na design ya watu hao bado wanapeta.
 
Sheria zote zinazohusu udhibiti wa daladala Tanzania zinavunjwa na watunga sheria au wasimamiaji wa sheria,kwa kuwa wao ndio wamiliki na wenye uwezo wa kupindisha sheria bila kuchukuliwa hatua. Kuondoa vipanya na macoaster si jambo gumu kama sheria zikifuatwa, lakini kamwe hazifuatwi. Ukiangalia kwa undani unaweza kuona daladala kwa Dar is political issue, inapunguza vibaka, wanalipa considerble amount ya kodi kwa serikali, inapunguza unemployement na kwa kuwa sehemu kubwa ya wamiliki ni wazito naweza kusema inapunguza hata ufusadi.

Once DART ikiwa operational inabidi ujiandae ku-deal na unrest itakayotokana na kuviondoa vipanya. I.e wizi mkubwa kwenye DART yenyewe, uhalifu,kupungua kwa kodi and somekind of political unrest.

Tunatakiwa kwanza tuoneshe uwezo wa kumanage hizi daladala tulizonazo barabarani sasa. Tusiwe new project mania halafu tukashindwa. tunarudi kule kule tuweke mfumo mpya wa kumanage mambo yetu.
Nakubaliana nawe kuwa wamiliki wa dala dala ndio wasimamizi washeria na ndio wavunja sheria.
Kuondoa vipanya na coaster hakuhitaji msuli, ikiwepo huduma nzuri na ya kisasa zitakufa kifo cha asili.
Kwamba dala dala zinapunguza vibaka,sijui ni takwimu gani zimetumika kujua kuwa wakati wa UDA kulikuwa na vibaka wengi kuliko sasa.

Shirika kama UDA liliajiri mamia ya watu kuanzia madereva wa shift, makondakta, wafanyakazi wa depot n.k idadi yao ni kubwa kuliko dei waka wa dala dala.Lakini mbona hujaongelea usalama wa abiria? Ni mara ngapi ulisikia UDA imeua au imekata watu miguu.

Kulipa kodi inategemea unaliangaliaje suala zima. Usafiri wa umma ni huduma ya jamii inayomwezesha mwananchi kutoka sehemu moja hadi nyingine iwe kwa shughuli za kijamii au kiuzalishaji. Inaweza kuwa huoni kodi inapatikana wapi lakini ni zaidi ya kodi za dala dala, ndio maana duniani kwenye miji mikubwa usafiri wa umma ni huduma ya lazima kama hospitali, ambulance n.k.

Kama inapunguza ufisadi tujiulize wamiliki ni wangapi? yaani ni bora kuwaonea huruma wamiliki 50 kwa gharama ya wanachi mamilioni wanaoishi jijini na wanaotembelea jiji. Na sheria za nchi ziliwekwa za nini kama tunaweza kudhibiti ufisadi kwa kuwaongezea mafisadi ufisadi.

Tunauwezo wa ku manage, UDA ipo tangu mwaka 1974 na ilifikia wakati utaratibu wake ulikuwa unaeleweka kuanzia muda,usalama n.k
Tatizo hatuangalii kwanini precision ifanye vizuri ATC ife, kwanini dala dala zifanye kazi kwa faida UDA ife!
Unapokuwa na mwenyekiti wa bodi mwenye historia chafu unategemea ufanisi utoke wapi.
Wamiliki wa dala dala na walafi kama wauza UDA usidhani wanaweza kufurahi UDA ikiimarika.

Nakubaliana nawe kuwa haikuwa sahihi kuuza UDA na kuanzisha 'UDA kwa jina la DART' lakini nadhani ipo hekima ya kuifanya UDA iwe mshiriki wa DART, je tumewekeza kiasi gani ili iwe mshiriki kamilifu?

Na mwisho, kwa miaka 25 iliyopita kipi kimefanywa na dala dala tunachoweza kujivunia zaidi ya vurugu, kukata ruti, usalama pungufu n.k.
 
Mikononi mwa serikali?mimi nilijua hapa tunakampeni na mashirika mengi zaidi wapewe wazalendo wayaendeshe? kama kuipeleka UDA serikalini mimi siafiki waungwana. Naona nyie mmesahau maneno ya wanafalsafa kuhusu Private V public property. UDA kuwa ya serikali Hellllll NOOOOOOO!!!
 
Back
Top Bottom