Elections 2010 Kampeni ya Dk. Slaa Karatu na Arusha Katika Picha

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
2a6s21z.jpg

Mchumba wa Dk. Slaa, Josephine, akisalimia wananchi wa Karatu mkutanoni, juzi Alhamisi.

b7z3na.jpg

Dk. Slaa hatumii shangingi. Hiki ndicho kipanya anachotumia katika ziara zake za kampeni. Katika picha hii, wananchi wa Arusha Mjini wanasukuma kipanya hicho kuondoka viwanja vya mkutano kuelekea hotelini jana Jumamosi jioni.

2zny2x2.jpg

Jina la shabiki huyu wa Dk. Slaa halikupatikana mara moja. Ni mkazi wa Arusha Mjini.

6f31bs.jpg

Dk. Willibrod Slaa, akimnadi mgombea wa ubunge katika jimbo la Karatu kupitia chama hicho, ambaye anatarajiwa kuwa mrithi wake wa ubunge jimboni humo, Mchungaji Israel Natse, wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Bwawani mjini Karatu jana Ijumaa

Dk. Slaa Katika Kampeni

Slaa+kumtambulisha.JPG

Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akimnadi mgombea wa ubunge katika jimbo la Karatu kupitia chama hicho, ambaye ni mridhi wake, Mchungaji Israel Natse, wakati wa mkutano wa hadhara wa kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Bwawani mjini Karatu jana

Slaa+kuhutubia+Karatu.JPG

Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Bwawani mjini Karatu leo.

168trmf.jpg

Dk. Willibrod Slaa, akizungumza na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Daudi Siasi, mara baada ya kuhutubia mkutano wa kampeni zake kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Bariadi juzi Alhamisi.

1z34cgz.jpg

Bendera za mashabiki Musoma Mjini: Dk. Slaa ni chaguo la vyama vyote

2vt8qhi.jpg

Wananchi Musoma: Dk Slaa ni Taa Mpya

Saturday, September 18, 2010

DR SLAA ALIVYOFUNIKA ARUSHA

2v98xdt.jpg

am42yv.jpg

ampelc.jpg

arusha4.jpg

arusha3.jpg

arusha2.jpg

arusha1.jpg
 
Big up dr.slaa.maajabu zaidi ni kwamba hawa watu hawajabebwa na maloli na kupewa t.shirt kanga au elfu 2
 
Asante mkuu, nilitamani nione hizo picha za Karatu na Arusha.

Nimesikitika Michuzi kamwonesha tu Dr. Slaa na Mgombea ubunge Karatu bila umati wa watu. Nadhani ndivyo walivyoelekezwa na Makamba, mbona za CCM anaonesha pia umati wa watu? Ina maana Slaa kwenye kampeni zake hakuna watu?

Huyu Michuzi ni mshabiki wa CCM tu hata kama wengine wakinipinga. Linganisha picha anazoleta za CCM na za wapinzani.
 
Mkuu Dopas,
kwa sababu hiyo, mimi hiyo blogu ya michuzi wala siifungui siku hizi, nimemshtikia anataka kutufanya wote ni malofa..
Actually, nime-delete toka kwenye favourites. To hell, kama kuna nyuuzi tutazipata tuu toka vyanzo vingine vingi ambapo ni wakweli!
 
hata mm nimemshiti michuzi, naona siku hizi amegeuka michuzi ya vibudu, BIG UP DR SLAA, KAZA BUTI, TUKO BEGA KWA BEGA, SIO NYUMA YAKO
 
These pictures made me cry, I am so moved angalia wananchi na taa zao mkononi kumulika mwanga wa matumaini. Dar zioneni picha hizo toa pembezoni mwa nchi hii, waungeni mkono. I nahuzunisha sana kuona Dar kwenye kila taarifa tunakosa wabunge wa upinzani na tunaenda kupata pembezoni kabisa, mpanda, kigoma, karatu

people let us work up, kuchagua upinzania siyo jinai
 
Dar jiji kubwa lakini chafu, viongozi walafi hawana muda wa kulifanya jiji liwe la kisasa. Watu wa Dar hawana muda wa kupiga kura wako busy kutafuta pesa zilizoibiwa na mafisadi. They are busy for nothing, I hate those people who say politics is out of their mind.
 
Mkuu Dopas,
kwa sababu hiyo, mimi hiyo blogu ya michuzi wala siifungui siku hizi, nimemshtikia anataka kutufanya wote ni malofa..
Actually, nime-delete toka kwenye favourites. To hell, kama kuna nyuuzi tutazipata tuu toka vyanzo vingine vingi ambapo ni wakweli!

Kuna wakati niliandika huyo Michuzi aache kutuletea matukio ya Chadema kama hawezi kuleta bila upendeleo. Lakini bado anajipendekeza kutuletea vipande vya picha, akimulika hasa eneo lisilo na watu wengi. Yote ni kwa ajili ya hela. Ameuza uhuru wake. Hana maana yoyote tena.
 
Je hakuna wafurukutwa wengine ambao wanaweza kusaidia kuanzisha Blogu (Mtungo) unaonyesha matukio na picha za mikutano ya Dr. Slaa ili kuweza kuleta taswira halisi ya mikutano yake. Kama mnavyoelewa picha huzungumza zaidi ya maneno elfu moja. Vilevile kama ingewezekana kuweka vpande vya video (video clips) za hotuba zake mbalimbali. Baada ya hapo vitu hivyo vitumwe kwa watu kwa njia ya simu. Naomba kutoa hoja.
 
Yaani mimi mwenzenu nahisi raha sana na kusisimka mwili mzima nionapo umati mkubwa wa wananchi katika mikutano ya Dr. Slaa, ama kweli huyu ni Nyerere mpya mkombozi wa watanzania mwenye uchungu na nchi yake. Mwaka huu lazima kieleweke hakuna kuiba kura na wala hakuna kudanganyikaaaaa. wananchi wamaechoka, wananchi wanahasira, wananchi wanauchu na kiu ya mabadiliko. Watanzania wenzangu tafadhali tujitahidi kumpigia kampeni za kutosha Dr. Slaa na wala tusiiachie CHADEMA pekee, mabadiliko ni kwa faida yetu wenyewe na wala siyo CHADEMA AMA DR. SLAA. Shime watanzania tujitahidi pia kuelimishana juu ya umuhimi wa kupiga kura na tarehe 31 october tujitokeze kwa wingi kutiwahamasisha na wengine kwenda kupiga kura, kumbuka kura yako moja inathamani kubwa sanaaa na wala usitegemee kuwa kun mtu atapiga kura kuchagua rais kwa niaba yako, tuache ushabiki wa maneno matupu bali tufanye kwa vitenda sasa.
 
Kusema ukweli machozi yamenitoka kwa jinsi picha zilivyo nigusa hii inaonyesha ni jinsi gani wananchi wamechoshwa na ukoloni wa ccm!

Kwanini nasema UKOLONI WA CCM??? Tulitawaliwa na wakoloni walitumyonya wakatunyanyasa na kutudhalilisha sasa tunawakoloni wa ndani ambao ni watanzania wenzetu wasio na huruma wala kujali maendeleo ya nchi yetu, wanajinufaisha wao wenyewe na familia zao hawajali kuwa rasilimali wazitumiazo ni mali ya taifa, wameuza madini yetu kwa manufaa yao rasilimali za nchi zimepotea kwa maslai yao binafsi, wanauwa tembo wanasafirisha meno yao kwa maslai yao wenyewe sasa watu wa kundi hili tuwaiteje kama sio WAKOLONI WA NDANI AMA WAKOLONI WA CCM!
Kiongozi wa nchi anatunyonya akatumaliza akaulizwa kwanini Nchi yako ni MASKINI wakati ina kila aina ya UTAJIRI bila ya AIBU WALA HAYA TENA KWA KUJIAMINI AKATUKANA MBELE YA ULIMWENGU KUWA HUJI NI KWASABABU GANI SIE WATANZANIANA NI MASKINI HUKU AKIJUA WAZI KUWA WAO NDIO WANAZIDI KUDIDIMIZA TAIFA LETU.

31-10-2010 tuamke alfajiri na mapema kwenda kupiga kura hata kama nitashinda kutwa nzima kwenye foleni nitahakikisha kura yangu naitowa kwa CHADEMA ili kuungoa huu UKOLONI wa CCM
 
Mwaka huu Slaa yetu ni Dr. Slaa. Kanyaga twende.
 
Michuzi hajui iyo blog tunaifungua ni wale wenye access ya mtandao na ambao hawadanganyiki.
Unazani mtu wa lupembe,makete,kantalamba,pawaga,tenende anawatch iyo blog yako.
Jaribu kuwa objective kwa wateja wako wote
 
Wakuu, mmenikumbusha mbali sana, unajuwa blog ya michuzi niliacha rasmi wiki mbili zilizopita nilikuwa nime-comment kitu flani ambacho kilinipotezea nusu saa nzima kukidaijesti ukweli lakini alivyo waajabu hakupost tatizo kubwa kilikuwa kina zungumzia ccm ambayo anaitumikia yeye.
 
Back
Top Bottom