Kampeni: Wito kususia biashara za mafisadi

Na unga mkono kususia bizaa za mafisadi papa
jamani tushirikiane tusikate tamaa
it will work very soon.
 
Nimeshatupa line ya voda nimenunua tigo dakika kumi zilizopita mm sisubiri hiyo tarehe 1/06/09
 
Mhh!!?? Train inataka kuingia barabarani nini??
Anyway cjui Tz na wa Tz wapi tunaelekea maana fisadi wa kiukweli ni nani hasa?maana mimi sasa naanza kuchoka kabisaaaa!!!!!

Mbona hueleweki? Kuwa wazi? Thread inajieleza.
 
Wewe MASATU kweli 'you are falling asleep'. Tunazungumzia mafisadi, nawe unaimba wimbo wa mafisadi akina RA kwa kumwita Mengi Nyangumi bila kuonesha unyangumi wake. Hebu amka toka usingizini ndugu yangu. Nchi inamalizwa hii. Sijui unaambulia nini kutoka kwa hawa mafisadi. Labda wewe ni houseboy wa RA, au shambaboy wa Jeetu Patel.
 
.
HAKUNA VITA YA UFISADI HAPA! NI CHUKI NA UBAGUZI TU! wasitiingize ktk mambo ya siotuhusu

Hii inayoitwa vita dhidi ya ufisadi, ninafananisha na mtu anyekuja msibani na kutaka kuwahamasisha waombolezaji kulipiza kisasi juu ya muuaji, eti yeye alifahamu tokea njama zilipokuwa zinapangwa. KWANINI USITUFAHAMISHE WAKATI NJAMA ZINAPANGWA NA KUOKOA MAISHA!!. Something behind this..!!!

Nafikiri tungefikiria tu kususia bidhaa zinazotoka nje na kukuza viwanda vyetu. Tuhamasishane kununua bidha MADE IN TZ, bila kuanza kubaguan wenyewe kwa wenyewe, mwisho tutakuta hata moja haifaii. Kwani kitu chochote unapokichunguza sana basi hutakosa kasoro zake.
 
Ninaomba kwa wale wenye majina ya products and services zinazotolewa na makampuni ya mafisadi papa na wale wengiine ambao hawakuitwa papa na angali ni mapapa japo wadogo basi mziorodheshe hapa ili tuwe tuna publicize hata kwa ndugu na marafiki wasizisogelee. Mimi tayari nimeshaanza kutosoma wala kugusa magazeti ya New Habari (2006) Limited. Tena kwa kuwa sasa magazeti haya hayana soko wafanyakazi wake wanapita kila ofisi muhimu kutafuta habari kwa kuwa hawana mengi ya kuandika siku hizi, yanaelekea kufa hasa baada ya Ms. Mwakitwange kuondoka na baadaye Hindi la Caspian likateuliwa kuwa CO mambo ni hovyo.

Kwa hakika walipofika ofisi nilipo na discounted Adverts Rates zao ili wapatiwe kazi niliwapokea tu as usual ila mara baada ya kuondoka mara moja niliagiza ofisa wangu asitoe wala tangazo la 500 ndani ya magazeti haya. I did it and I am happy with it!!!
Ukiamua kukataa kitu kataa with all your vains, usiwe vuguvugu. Aluta continua JF!
 
Nimeshatupa line ya voda nimenunua tigo dakika kumi zilizopita mm sisubiri hiyo tarehe 1/06/09



Makala!

I like your idea lakini bwana nasita na kusikitika kwamba hilo haliwezekani mafisadi wamejikita kila kona ya uchumi wa Tanzania. Na kwa kuwa watz ni waoga kupindukia infwact it is another day dreaming. Itabidi uache kila kitu na mwisho utakufa!! angalia usije tembea uchi!!

Bandari yaendeshwa na mafisadi;sukari ya mafisadi; umeme ,mafuta yaani kuanzia petroli mpaka korie inamilikiwa na mafisadi;unga wa kupikia sembe/kaunga na mchele wabebwa na magari hata ule wa KYELA kwa Mwakyembe utahitaji kulamba miguu ya mafisadi!
Serikali yote kuanzia Rais mpaka mwenyekiti wa mtaa wako pale thanks to ufisadi!

Kwa mtaji huo mwanangu nachelea kukuunga mkono! But we have the power!! 2010 TUKAPIGE KURA YA HAPANA KWA CCM na kama wakiiba kura tuwatoe mkuku kwa staili ya madagascar apewe hata chizi atutoe kwenye huu mtambo wa mavi then kitaeleweka down the road tutamgeuka as usual!!

CCM has lost the mandate to fight ufisadi na VASCO DAGAMA who is now in a show biz huko USA Anazidi kuchefua kama rais anafikiri hao wakimbizi cowards who are in the state ni watu wa kutegemewa au kuna maisha mazuri kuliko hapa Tanzania this president is not serious!!

Badala ya kuwaambia warudi kuishi maisha bora ya bongo anaota ndoto kwamba wanaishi vizuri who told him basi na yeye akimbilie huko pambaf!!!
 
WANA jf KWA mtazamo wangu tafsiri ya fisadi imepotea na watanzania,wana jf,wanahabari wameipoteza,lakini kwa kuwa mtoa mada ana nia njema na kwa uelewa wangu nimemuelewa kuwa tususie bidhaa za wanao hujumu uchumi wa nchii hii naomba nianze kutaja kampuni na bidahaa husika.
a; IPP MEDIA GROUP
BIDHAA ZAKE.
1; ITV 2;NIPASHE 3;ALASIRI 4;GUARDIAN 5;KULIKONI 6;THIS DAY 7; SEMA USIKIKE, 8; TAIFA LEO. 9;EATV 10; CAPITAL TV;
B; KWANZA BOTTLERS,NA BONIT BOTTLER
BIDHAA, SODA ZOTE ZA AINA YA COCA COLA UKIONA HUPA IMEAANDIKWA COCA ACHA. 2;MAJI YA KILIMANJARO 3;MAJI YA DASANI;
C;CRDB BANK
MENGI ANA SHARES CRDB KWAHIYO WENYE ACCOUNT HUKO WAKAFUNGE NA MIKOPO WARUDISHE.
D;NICO LTD
MENGI ANA HISA NICO NA NI MUANZILISHI WAMEPATA MTAJI KUPITIA SISI PAMOJA NA HISA ZA NICO KUSHUKA NA SHAURI TUUZE HISA ZETU TUCHUKUE PESA ZETU.

KWANINI NAMTAJA MENGI,AMEFANYA UPORAJI NBC NA KUKIMBIA KULIPA DENI NI MMOJA WA WALIOFILISI BANK YETU,PIA MENGI NI FISADI KWA TAFSIRI YA MAANDIKO YA BIBILIA KWANI AMEPORA MKE WA MTU NA ANAISHI NAE,ILA KWA MASLAHI YA TAIFA ANAHUSIKA NA UKWEPAJI WA KODI,NA KUTOLIPA MADENI YA MA BANK,NA IMPORT SUPPORT NA KUAJIRI WATU KAMA VIBARUA KWA MIAKA KUMI ILI AKWEPE KODI
 
Neno BUSANDA ni muunganiko wa maneno mawili BU (Mahali) na SANDA (wote mnajua, ni ile inayotumika kuzikia). Sasa basi Uchaguzi mdogo unafanyika BU-SANDA, na maana yake ni kwamba CCM ITAZIKWA rasmi BU-BUSANDA. Zomea zomea inayoendelea maana yake ni kwamba sasa Watanzania WAMEIKATAA rasmi CCM (Chama Cha Mafisadi).

Kuhusu kususia bidhaa za mafisadi mie mwenzenu pamoja na familia yangu tulianza siku nyingi kwa kutupilia mbali 'chip' za Vodacom baada ya kugundua kuwa ndani yake kuna maafisadi wengi. Nasubiri kwa hamu orodha ya bidhaa nyingine mnazozifahamu za hawa FISI MAJI ili tuanze kuzisusia rasmi. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
It really gets on my nerves when I realize that there are still some fools in here who are trying to protect the real fisadis. Wewe unayeshupalia bidhaa za IPP kama sio Lowassa ni Rostam Aziz, na kama sio basi ni Sophia Simba au George Mkuchika au yule jamaa mwenye mdomo mpana wa TBC1 - jina nimelisahau.
Hapa tunazungumzia mafisadi ambao tuhuma za zinajulikana waziwazi na sio wazalendo wanaopakaziwa ufisadi na hawa mafisadi papa -- kisa: wameumbuliwa.
 
kweli tususie hakuna kunywa dasani...hakuna kunywa coca cola na fanta na sprite....hakuna kutangaza itv...hakuna kusoma nipashe na guardian....
 
Mimi naunga mkono hili swala mara dufu....na mimi pia ni mmoja wa watu wasiofahamu makampuni yote yanayomilikiwa na mafisadi.....Lakini.....So far....mbona orodha ya makampuni yaliyotolewa ni ya Mengi peke yake wakati orodha iliyotolewa wazi magazetini inaongozwa na Rostam Aziz na Jeetu Patel...nk....Makampuni ya Mengi yanafahamika na watu wengi kwasababu alianza kuyatangaza siku nyingi sana .....

Kwahiyo...naomba kama kuna anayeweza kuorodhesha makampuni ya Rostam na Jeetu afanye hivyo ili mimi na wengine kama mimi tuweze kuliunga mkono suala hili ipasavyo na pia tuweze kuisambaza orodha hiyo kwa ndugu na jamaa wasio wana JF.
 
tususie mara ngapi?

mimi maji ya Kilimanjaro situmiii

magazeti yake sinunui

redio yake sisikilizi

tv ndio kaisaa


In short situmiii product yoyote ya IPP

Hebu basi tueleze unavyotumia mkuu;

Je,
1. Nyumbani unalindwa na Ultimate Security ya Tanil Somaiya?
2. Unanunua magazeti ya New Habari Corp ya Rostam Aziz?
3. Unaangalia TBC1? na kusikiliza TBC Taifa hasa wakati wa habari za RA zikielezwa positively?
 
kususia biashara za mafisadi wanaojulikana, na wasiojulikana?? na waliosingiziwa??

tuanze na viwanda vilivyouzwa kifisadi, mabenki kama NBC, mpaka barabara zilizojengwa kifisadi tusisafirie!

Mpaka umeme wa kifisadi tusiwashe!

utakuta nchi nzima watu wana-stuck, maana mpaka bajaj nyingi ni za mafisadi , achilia mbali daladala, tex na mabasi!

au nyie kwenu mafisadi ni Mengi na RA??

Mtakaa na njaa shauri zenu, ngano ile je??
 
kususia biashara za mafisadi wanaojulikana, na wasiojulikana?? na waliosingiziwa??

tuanze na viwanda vilivyouzwa kifisadi, mabenki kama NBC, mpaka barabara zilizojengwa kifisadi tusisafirie!

Mpaka umeme wa kifisadi tusiwashe!

utakuta nchi nzima watu wana-stuck, maana mpaka bajaj nyingi ni za mafisadi , achilia mbali daladala, tex na mabasi!

au nyie kwenu mafisadi ni Mengi na RA??

Mtakaa na njaa shauri zenu, ngano ile je??

Yaani mkuu umenena,
Hapa Bongo hapatakalika tukiamua kususia bidhaa zote. Chukulia mfano huu kidogo

1. TANESCO- (Mafisadi: Songas, Aggreko, IPTL etc na Rostam ndo msambaji wa nguzo ndo maana hata bei ya nguzo imepanda sana). Haya wandugu ng'oeni mita za TANESCO wekeni solar

2. Nondo za kujengea- Jeetu Patel and co. (kiwanda kimewaka moto majuzi), kuna kiwanda kingine cha wahindi kule Kipawa na pia cha SITA stills pale Tabata along Mandeal road hivi sivijui vizuri.

3. Viwanda vya nguo vingi labda ukiondoa Urafiki vina mikono ya mafisadi

4. Treni- inamilikiwa na Wahindi mafisadi: Hakuna kupanda treni- ndugu zetu wa Kigoma, Mwanza, Tabora, Shinyanga, Kagera n.k kazi kwenu

5. Precision Air- Fisadi Mramba ana hisa huko - Hakuna kupanda Precision Air

6. Madini (Caspian ya Rostam ndo wachimbaji): kwahiyo wafanyakazi wote huko waache kazi

7. Bandarini- Kuna TICTS ya mafisadi. Kwahiyo hakuna kununua bidhaa yoyote inayotoka nje ya nchi inayopitia bandari ya DSM yakiwemo magari ili TICTS wakose kazi

8. Makampuni ya simu: (a). VodaCom- Kuna RA (share holder 35 %), Somaiya (Shivacom -super dealer ), Lowasa - Alphatel (dealer)
(b). Zain (wameifisadi TTCL hadi ikabinafsishwa na wameingia TZ kwa wizi na utapeli mkubwa)
(c). Tigo (wamekuwa wakibadili majina kila baada ya miaka 5 kukwepa kodi: 2001 from Mobitel to Buzz, 2006 from Buzz to Tigo) na ukifuatilia tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993 ikishirikiana na shirika la posta na simu wakati huo mpaka sasa ime-undergo several dubious contracts na serikali. Mpaka sasa kampuni inamilikiwa na Millicom ya Luxemburg kwa asilimia 100 % kinyume na sheria za nchi
(d). TTCL - hii nayo imebinafsishwa kwa Wa-Kanada kifisadi kupita kawaida na bila shaka mafisadi wana share huko. Kwahiyo tunatupa simu zote na kufunga landline zetu zote tuwasiliane kwa internet na barua.

Mpo hapo WaTZ wenzangu? Shughuli ipo. Ndugu zangu kila mahali tumezungukwa na ufisadi na kama hutaki kabisa bidhaa hata moja inayotokana na kazi yoyote ya mafisadi inabidi uondoke katika hii dunia.

The best way let us vote CCM out next year (2010) yaweza kutusaidia sana angalau kupunguza wizi wa mali za umma kwa maendeleo ya taifa letu.
 
Last edited:
La Mgambo Limelia.


Wote Spana Chini.


Kuanzia Tarehe 01-06-2009 Wapinga Ufisadi wote waliuokuwa Wanatumia Vodacom wahamie mitandao mingine.


Sasa tunakomaa nao.


Leteni bidhaa za makampuni mengine pia ya kifisadi. No jokes.
 
La Mgambo Limelia.


Wote Spana Chini.


Kuanzia Tarehe 01-06-2009 Wapinga Ufisadi wote waliuokuwa Wanatumia Vodacom wahamie mitandao mingine.


Sasa tunakomaa nao.


Leteni bidhaa za makampuni mengine pia ya kifisadi. No jokes.

Soma Post 55 hapo juu
 
Soma Post 55 hapo juu

Mkuu;

Charity begins at home and u must start somewhere.

Kama leo hii uchukue hatua kwa sababu yoyote ile, wajukuu zako wana hatari ya kuja kukuta nchi hii haina kitu kwa wazalendo.

You decide now, politics or reality. The choice is yours!

Tulio na uchungu wa thati tumeshatoa ujumbe na tunatenda.

I am done with this.
 
Wandugu tumekuwa sana tukija na data za kuwahusisha wale nugu yetu hosea anasema washika uchumi wa nchi...(MAFISADI).Wengi wametoa maoni yao ..wamejaribu kutoa mawazo yao...nafikiri imefika sasa badala ya kuakaa na kuanza kuandika tuanze kufanya vitendo kwa kuukataa ufisadi wao......BASIL MRAMBA ;ROSTAM AZIZ
wamekuwa na mali nyingi sana ambazo kwa masikitiko wengine tumeendelea kuzikimbilia na hata wengine kuhakikisha wanasionga mbele;;

Pdidy

KATAA UFISADI-- KATAA BASIL MRAMBA-- KATAA PRECISSION AIR

BASIL MRAMBA amkuwa na share nyingi sana pale precission air.najua watanzania wengine watashangaa ila kwa mtazamo wangu kama tunashabikia kufikishwa mahakamani mramba na huku Tunaendelea kupanda PRECISSION AIR;tunajiumiza vichwa wenyewe.....
PESA tunazopigia kelele ndizo zimeleta ndege za precission kuwepo pale..sasa kama ni hilo ningeomba tumsaport na kijana wetu apo chini

KATAA UFISADI-- MKATAE ROSTAM AZIZ--
KATAA KUTUMIA VODACOM


It is too late now but not too late enough.. kama uko kwenye mapambano dhidi ya ufisadi na hauko tayari kusalimu amri, nakushauri kuachilia namba za simu za Vodacom ASAP. As a matter of fact, hamia "kwingine" within the next 72 hours (beginning Monday). Do it or be ready to live with the consequences.

Nilikuwepo.

M.M.
 
Back
Top Bottom