Kampeni Jimbo La Uzini: CCM Yaelemewa na Kasi ya CHADEMA, yaanza vitisho kama Igunga

Wakuu heshima mbele,

Taarifa za uhakika kutoka Uzini zinaarifu kuwa CHADEMA imeliteka jimbo hilo,makundi ya watu kuanzia watoto,vijana,akina mama na wazee wanaunga mkono cdm,alama za V na neno pipooos vimetawala na wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kwenye mikutano.CCM imebanwa na imeanza vitisho,ikiwamo kuorodhesha majina ya wakaazi wote wanaotoka bara nakuwatishia kuwa cdm ikishinda watafukuzwa Zanzibar ikumbukwe kuwa jimbo la uzini linamchaganyiko wa makabila kadhaa toka bara kama wasukuma,wanyamwezi nk na zoez hili linafanywa na mashea ambao kwa bara ni sawa na watendaji wa kata na wanaheshimika sana kule visiwani,wamekuwa wakiingia kwenye miji ya watu na kuwaamuru watoe vitambulisho vyao vya kupigia kura wananchi kutoka maeneo kadhaa kama GHANA na MIWANI wamekuwa wakienda kulalamikia hali hii kwa viongozi wa cdm,shea mmoja toka eneo la miwani alikiri kupata maelekezo ya kukusanya shahadda toka kwa viongozi wa juu wa ccm baada ya kufuatwa na makamanda baada kumpoka raia mmoja kitambulisho ajabu shea huyo alitoa pia utetezi ambao uliwaacha midomo wazi makamanda kuwa kamnyanga'nya kitambulisho yule raia kwakuwa ni MLEVI.Taarifa zaidi za kiintelejensia zinaarifu kuwa kuwa tayari kikosi kimoja cha usalama kimepewa maelekezo kuwakamata na kuwaweka ndani wanaounga mkono mabadiliko ili wasiweze kupiga kura siku ya uchaguzi.

Nawasilisha.

CDM hawawezi shinda uzini, watu wanamkubali RAZA kwa uzalendo wake kwa wazanzibari. Na wao wanasema Raza atawaletea maendeleo kwa pesa zake hata km serikali itakuwa haina kitu. Je CDM mgombea wenu analiweza hilo ?

 
..kwa hapo ZNZ panatakiwa kipatikane chama kingine/vingine zaidi ya CCM[asp] na CUF[hizbu].

..hiyo itasaidia kuongeza uwigo wa demokrasia, na kuleta mawazo mapya na mbadala ktk siasa za Zanzibar.

..hata Wamarekani nao wameanza kuchoshwa na siasa za Republican vs Democrats, kiasi kwamba wameibuka wapambanaji wa Tea Party.
 
Back
Top Bottom