Elections 2010 Kampeni chafu zaendelea dhidi ya CHADEMA

Heshima kwako Malaria sugu,

Hakuna habari za namna hii hapa Arusha magari ya vyama vyote yanapita kutangaza wagombea wao watahutubu sehemu gani ya jiji la Arusha.CHADEMA watakuwa na mkutano wao Kijenge,TLP watakuwa na mkutano Krokoni eneo maharufu sana kwa kuuza mitumba.Godbless Lema anjua kutumia propaganda ili kuvuruga mkutano wa Lyimo hii si mara ya kwanza.

Kwa hiyo unataka kusem Lyimo wanachuana vikali na Bwana Lema?

Alfu Batilda yupo ICU?
 
Heshima kwako Craswise,

Acha uzushi Godbless Lema hawezi kupokelewa TLP hata kwa dakika moja anajulikana ni mfanyabiashara mzuri ndiyo maana aliuza ubunge na diwani wa upinzani mwaka 2005.
CHADEMA kuitwa wazushi,waongo, waropokaji, walalamikaji siyo maneno mageni kwetu, ungetaka ukweli nenda pale Police Station maana najua uko Arusha hata hivyo utapata ukweli kwa wanafiki wenzako TBC kama watatangaza na Lema ni Mfanyabishara mzuri kama ulivyo kubari hapo juu kama ndiyo kwanini unamzalilisha kweli mfanyabisha mzuri auze ubunge kwa mil 30 badala ya zadi ya Mil 600 ambazo angezipata kwa miaka 5, acha kutufanya wajinga, huna jipya zaidi ya unafiki na chuki dhidi ya Lema,
 
Huyo Ngongo nadhani ndiye mgombea mwenyewe wa TLP. At one time alitoa post humu kuhusiana na Lema (I completely don't know the guy) kwamba ni tapeli, shule ndogo, visionless. Later on nikaja kugundua thruj himself kwamba Lema ni tishio kwenye hicho kinyang'anyiro kiasi kwamba wote CCM an TLP wanakosa usingizi.
 
niko arusha, yanayozungumwa kuhusu tukio la leo, na kuhusu bendera za chadema kugeuka tanzanite ni kweli kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
CHADEMA kuitwa wazushi,waongo, waropokaji, walalamikaji siyo maneno mageni kwetu, ungetaka ukweli nenda pale Police Station maana najua uko Arusha hata hivyo utapata ukweli kwa wanafiki wenzako TBC kama watatangaza na Lema ni Mfanyabishara mzuri kama ulivyo kubari hapo juu kama ndiyo kwanini unamzalilisha kweli mfanyabisha mzuri auze ubunge kwa mil 30 badala ya zadi ya Mil 600 ambazo angezipata kwa miaka 5, acha kutufanya wajinga, huna jipya zaidi ya unafiki na chuki dhidi ya Lema,

Heshima kwako Crashwise,

Mkuu kwanza samahani sikujuwa kulikuwa na tafrani baina ya mgombea ubunge wa CHADEMA Bwana Godbless Lema dhidi ya watangaji[wanachama wa TLP.Ilinibidi nipige simu kwa wadau wa TLP,CHADEMA na polisi wilaya ya Arusha ili kupata ukweli wa mambo ulivyokuwa.Mkuu natumaini umenisamehe kwa kukataa kwamba hapakuwepo na purukushani uliyoileta hapa jamvini bahati mbaya hukujuwa wapo wadau waliotayari kufuatilia jambo hata kwa gharamani kiasi gani.

TLP walikuwa na maadamano makubwa kata ya Levolosi maandamano hayo yaliambatana na kuvunja tawi la CHADEMA lililozinduliwa na Bwana Lema siku za karibuni na kuripotiwa na gazeti la Mwananchi[wamebaki wanachama wasiozidi kumi,wengine 80 wamejiunga rasmi na TLP].Leo gari la matangazo la TLP lilikuwa likitangaza mkutano mwingine eneo la krokoni na kuujulisha umma juu TLP kusomba wanachama wa CHADEMA.Lema alipopelekewa habari akasomba wahuni wenzake wakiongozwa na mgombea udiwani kata ya Kaloleni rasta wakavamia gari la matangazo na kuwapiga vibaya watangazaji.Kesi ikeenda polisi kila mmoja akatoa maelezo yake ambayo yamepelekea Lema na kundi la wahuni kufunguliwa kesi ya kujeruhi,kusababisha uvunjifu wa amani na uharibifu wa vifaa mali [vifaa vya matangazo na gari la matangazo].

Habari ndiyo hiyo tuache kutoa habari za kishabiki ili kufurahisha mashabiki.
 
hakuna haja ya kuniomba samahani wakati bado unaendelea na unafiki na chuki zako binafsi dhidi ya Lema, watu wanafatilia hivyo wanajua nani ni nani kati ya Lema na Lyimo...eti TLP imechukua wanachama 80 wa-CHADEMA!? yale yale ya CCM, wakati kuna watu walioko hapa Arusha hata hawajui kama TLP nayo imesimamisha mgombea ubunge hapa Arusha, nimesikia gari lenu la matangazo saa moja na nusu usiku linatangazo kesho mna mkutano vipi sheria inaruhusu maana tabia hii huwa naisikia kwa wezenu CCM wao ni siku nzima wana tupingia makelele, wambie wana tuboa sana, chadema tutashinda hata kama mtaunganisha nguvu TLP na CCM…tukutane tarehe 31-11-2010
 
Kweliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii
 
Kwa chama kinachoongozwa na mtu kama Lyatonga unategemea nini? Yuko tayari kukaa kwenye chama kibovu hata kama hakikubaliki mahala kokote ili muradi tu awe mwenyekiti wa chama.

TLP si kwamba wanatumiwa na CCM, ni kuwa wanajipendekeza wakidhani watapewa chochote na CCM. TLP ni madalali njaa wa siasa hapa nchini na ni chama cha kishenzi kama CCM. CCM ni mshenzi mkubwa na TLP ni mshenzi mdogo.

Hawa ndio wanasababisha wananchi wadhani wapinzani ni wahuni, kumbe ni vyama kama TLP vyenye mlengo wa ki CCM ndio vimejaa uhuni.
Kweli Mkuu lakini kuna haja ya kufatilia hizi habari za TLP kupewa pesa na CCM ili wapate nguvu na kura za upinzani zigawanwe huku wakimchafua Lema na Chama chake..
 
Waache waendelee na kampeni chafu sie tunaendelea kupeta. Mungu ni wa ajabu maana kawatia watu maarifa na wameshatambua kuwa yote anayozushiwa Dr ni uongo. Sasa wanawasikiliza na kuwabeza tuuuuuuuuuuuu. Chadema inaendelea kukata mbio haooooo
 
hapa Arusha Chadema na CCM hawa wengine wana sindikiza tu

Heshima kwako Crashwise,

Mkuu hii ni habari nimeinyofoa Tanzania Daima gazeti linalomilikiwa na Mwenyekiti wa CHADEMA taifa hebu soma bila ushabiki maandazi unaotaka kuuleta jamvini.Mkuu najua unapenda Godbless lakini anaendekeza upuuzi kwa namna ya ajabu kiasi kwamba baadhi ya wapenzi wake wameanza kumkimbia.Mgombea udiwani wa CHADEMA kata ya Themi Bwana Ngowi juzi alipata wakati mgumu kumtetea Godbless ofisi za TANESCO mkoa baada ya baadhi ya watu kumuuliza imekuwaje mtu kama yeye mwenye elimu nzuri kama yeye asigombee ubunge na kumwacha Lema mwenye elimu ya ndogo na uelewa mdogo akikidhalilisha chama.Kwa taarifa yako mpaka sasa Lema ana kesi kumi na moja nyingi ni za utapeli na kutishia watu maisha.

Kampeni Arusha Mjini zapata moto

na David Frank, Arusha

amka2.gif
KAMPENI za kugombea ubunge jimbo la Arusha Mjini zimezidi kuchukua sura mpya kwa wagombea kujinadi kwa staili tofauti ikiwa ni pamoja na kupigana vikumbo misibani, huku wengine wakijinadi katika vijiwe vya kahawa na vibanda vya kung'arishia viatu. Hali hiyo inadhihirisha kuwa kampeni za majukwaani na zile za nyumba kwa nyumba bado hazitoshi kufuatia kuwepo na msuguano mkali baina ya wagombea kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), Tanzania Labour (TLP) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Tukio la aina yake lilitokea juzi katika msiba wa mfanyabiashara maarufu Naftal Mollel eneo la Kaloleni jijini hapa na baadaye mazishi kufanyika Kijenge ambapo mgombea ubunge kupitia CHADEMA, Godbless Lema, alishiriki katika mazishi hayo huku akionekana kutumia muda wake vizuri kwa kunadi sera zake.
Wakati mgombea huyo akiendelea kumwaga sera zake, ghafla mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian, aliingia katika mazishi hayo akiongozana na wapambe wake na mara msiba huo ukageuka kuwa furaha baada ya waombolezaji kufurahia ujio wake na kusahau majonzi ya ndugu yao.
Mgombea huyo alianza kuwapa mkono wa pole ambapo waombolezaji hao kwa upande wao walijikuta wakiimba ‘daada…daada….daada' na kufanya umma uliokuwa umefurika katika mazishi hayo kutaharuki.
Lakini wakati hayo yakitokea, mgombea kiti hicho kupitia TLP, Macmillan Lyimo, ambaye amepanda chati siku za hivi karibuni na kutishia nafasi za wagombea wengine, amekuwa akimwaga sera zake katika vijiwe mbalimbali jijini hapa vikiwemo vibanda vya kung'arishia viatu na vya kahawa.
Tanzania Daima ilishuhudia mgombea huyo akimwaga sera zake katika vibanda vya kung'arisha viatu karibu na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Jimbo la Mji Kati akiwaomba wang'arisha viatu kumpa kura ili alete mabadiliko na kulipatia jimbo la Arusha maendeleo ya kweli.
 
Kwa hiyo unataka kusem Lyimo wanachuana vikali na Bwana Lema?

Alfu Batilda yupo ICU?

Heshima kwako Fidel80,

Mkuu wagombea ubunge Arusha mjini wako watano kati ya hao wagombea watatu Lema,Lyimo na Batilda yoyote anaweza kuibuka mshindi.zimebaki siku kumi na tano kila mgombea ana base yake anayoitegemea Lema anategemea kupata kura nyingi za vijana wenye umri kati ya miaka 20 mpaka 25.Mama Batilda anategemea kura za wanachama wengi wa CCM ambao si rahisi kubadili msimamo pia anategemea nguvu ya chama amabyo siku za karibu imeongezeka sana.Lyimo anategemea kupata kura nyingi za watu wa makamo na watu wanaofanya maamuzi baada ya kumsikiliza mgombea.
 
Huyo Ngongo nadhani ndiye mgombea mwenyewe wa TLP. At one time alitoa post humu kuhusiana na Lema (I completely don't know the guy) kwamba ni tapeli, shule ndogo, visionless. Later on nikaja kugundua thruj himself kwamba Lema ni tishio kwenye hicho kinyang'anyiro kiasi kwamba wote CCM an TLP wanakosa usingizi.

Heshima kwako Nyambala,

Mkuu jaribu kufikiri kidogo kabla ya kukimbilia kupost.

Mkuu Lowasa ni maarufu sana monduli pamoja na madudu kibao aliyowahi kufanya [RICHMOND],Bariadi Chenge ni maarufu sana pamoja na kuficha mabilioni ya fedha nje,Rombo wapo watu wanamwona Mramba mungu mdogo pamoja na kulitia taifa hasara kubwa achilia mbali kesi iko mahakani.
Lema ana kesi ya kumtapeli Mama Maimuna Rashid lakini wapo watu wanaona hiyo kesi haina maana sana wanadhani wakimpeleka mjengoni atapunguza utapeli kwakuwa wabunge wanalipwa vizuri binafsi nimewahi kukutana na vioja vya namna hii usishangae hii ni Tanzania kila mara jambo jipya linaanza Tanzania wengine wanafuata.

Mkuu mimi na wewe tunashangaa Lowasa,Mramba na Chenge wanawezaje kuchaguliwa na wananchi ? pengine unatakiwa kuacha kushangaa Lema pamoja na kuwa na mapungufu kibao bado anao watu wanomshabikia.

Mkuu mimi si mgombea wala sina interest ya kugombea nafasi yoyote ya kisiasa ila napenda kushiriki mijadala ya kisiasa bila kufungamana na chama chochote.Wewe si mtu wa kwanza kudai mimi ni mgombea wa TLP wapo wengine wamewahi kunituhumu mimi ni mgombea wa CCM.Mara nyingi hapa jamvini kuna habari zinazopendwa na wengi bahati mbaya sipendi kufuata mkumbo nina misimamo yangu.
 
Back
Top Bottom