Kambi za kujenga uzalendo zianzishwe haraka

mgen

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
22,631
8,417
wananchi tumefika sio pazuri kama taifa mshikamano haupo tena hivyo basi napendekeza yafuatayo;

Ziundwe kambi maalum za kufufua uzalendo na mshikamano kitaifa

Viongozi wote waandamizi wakiwamo wa siasa na dini zote wachanganywe na kunolewa na wakufunzi wa Jeshi

Waandishi wa habari na watangazaji wa radio wote wahudhurie mafunzo hayo ya uzalendo.

Uwekwe utaratibu wa waliopitia mafunzo hayo kupewa kipaumbele kwanza kupata ajira!

wana jf naomba mchango wenu hali si shwari!
 
Tuanze kwanza na kambi za KUTIMIZA KWANZA HAKI, mambo mengine yatafuata. Uzalendo bila haki ni sawa ya maisha bila damu mwilini, sahau kabisa!
 
Yes indeed! And the new grooming points for future leaders. Our current system has failed us. Ndio maana tuna viongozi hawajui kama ni viongozi.
 
Kikwete, Makamba, Chiligati wote hawajapitia kwenye kambi hizo wakarudishwe tena ndio ufisadi ukome?
 
Tanzania kuna Tatizo kubwa sana??? Ajira kwa vijana. kuna maelfu ya vijana waume kwa wake hawana ajira.

Amani Tanzania yatoweka kwa ukosefu wa ajira.

Badala ya kubinafsisha mashamba, hawa vijana wangepewa mafunzo ya kilimo na kuanzisha kilimo.

Tanzania italipuka ,not so long
 
Tuanze kwanza na kambi za KUTIMIZA KWANZA HAKI, mambo mengine yatafuata. Uzalendo bila haki ni sawa ya maisha bila damu mwilini, sahau kabisa!

Kunguru kula kifaranga cha kuku anaona ni haki pia ndio sababu inabidi azomewe

Kutenda na kujua haki yako na ya wengine kunawakati hakuna budi ufundishwe kwa njia yeyote ikibidi hata kwa kuzomewa na bakoraaa!
 
Uzalendo utakuja automatically watu wakiridhika na uongozi na yanayoendelea!Wakiwa na ajira na uhakika wa kula kesho!!Sidhani kama mtu anaweza kua na mawazo ya kizalendo wakati hana kazi wala chakula na anaona serikali haimsaidii chochote zaidi ya kuzidi kumkandamiza!
 
Viongozi wakuu wa nchi sio wazalendo. Hao vijana nani atawajengea uzalendo? Wangeanza kwanza hao wakubwa kuwa wazalendo ndipo na sisis tufuate!
 
Back
Top Bottom