Kambi ya Lowassa yaibuka kidedea UVCCM Arusha

Kinyang'anyiro cha kumsaka mjumbe wa baraza kuu la UVCCM Taifa kwa mkoa wa Arusha jana kimehitinishwa kwa ndugu BENSON MOLLEL kuibuka mshindi wa kishindo kwa kupata kura 326 na kumbwaga mpinzani wake vibaya ,Lightines Msemo aliyeambulia kura 40.ccm hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.
 
Naona Lowassa anazidi kupasua anga tu!
Umeona eeeh

Wakati wapinzani wake wakilialia(Sumaye), wakilalamika(Sitta), Wakiropoka(Nape) na Wakiroga(Membe), Lowassa mwenyewe anajipanga vizuri kuzidi kuwakamua tu.

Siasa za CCM wakati mwengine zina raha yake!!
 
Kinyang'anyiro cha kumsaka mjumbe wa baraza kuu la UVCCM Taifa kwa mkoa wa Arusha jana kimehitinishwa kwa ndugu BENSON MOLLEL kuibuka mshindi wa kishindo kwa kupata kura 326 na kumbwaga mpinzani wake vibaya ,Lightines Msemo aliyeambulia kura 40.ccm hoyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee.

Mkuu embu tuweke vizuri Mshindi anatoka kambi gani? Mshindwa naye anatoka kambi ipi?
Siku hizi ushindi unashangiliwa kufuatana na kambi za wagombea urais!!
 
Huyo Dr Harold Adamson amesomea political science? Kwa nini asitumie elimu kubwa aliyonayo kujenga nchi kupitia fani yake badala ya kukimbilia kwenye majukwa ya siasa?

huyu atakuwa medical doctor, tz huwezi kupata phd ukarudi kugombea umoja wa vijana. Lazima wakuzeeshe kwanza
 
lowasa hana mpinzan ndani ya magamba ana nguvu ya pesa na ushawishi ,membe hafui dafu kwa mamvi
 
Na sio arusha ni pamoja na mara,mwanza,shnyang,geita,simiyu,kigma,tbra,katavi,tanga,irng,mbeya,kilmnjaro,ruvma,njombe,lindi,manyara,sngida,dodma,kwa kifupi mikoa ya bara membe na riz1 wake wameshnda mikoa 3 tu dar,pwani na kagera cha ajabu membe mpaka kwake lindi mtu wa lowasa kashnd,walai nazidi kufurahi kuwa kwenye kambi hii chadema i wil see u when u get there 2015..
 
Na sio arusha tu ni pamoja na mikoa karibu yote bara Mara,Mwanza,Shinynga,Geita,Simyu,Kigoma,Tabora,Singida,Katavi,Lind,Irnga,Mbeya,Ruvuma,Mtwara,Kilimanjro,Arusha,Manyara,Dodoma yani Membe kambulia mikoa 3 tu Dar,Pwani,na Kagera mpaka home kwake Lindi kapigwa na mtu wa el.
 
Na sio arusha tu ni pamoja na mikoa karibu yote bara mara,mwanza,shnynga,geita,simyu,kgma,tbra,sngnda,katavi,lind,irnga,mbeya,rvuma,mtwara,kilmnjro,arusha,manyara.dodma yani membe kambulia mikoa 3 tu dar,pwani,na kagera mpaka home kwake lindi kapigwa na mtu wa el.

Umeona eeeh!!

Kuna tetesi pia kuwa baadhi ya hao watu wa Membe walioshinda mikoa ya pwani na kagera bado ni mapandikizi ya Lowassa kwa siri.

Kwa mkoa wa Dar sidhani kama washindi ni kambi ya Membe, kwani kambi ya Lowassa ina nguvu sana hata Dar, ngoja nifanye uchunguzi wangu zaidi kuwafahamu washindi ni nani.
 
Naapa mbele ya mwenyezi mungu, jinsi akili yangu inavyozidi kuimalika naona bora kambi ya Lowasa kuliko hizo nyingine.
 
Mafisadi ndani ya shishiem yataendelea kupenya kwani hata hao wanaowapinga wakionjeshwa wanatulia,dawa ya mafisadi waingie kwenye game na peoplessssssssssssssssssssssssssss!!!!!!!!!!
 
Kambi zipo nyingi lakini kwa sasa kambi kuu ni tatu tu, zingine ni sub-kambi ya hizi tatu (zipo Oppotunistic) na kadri siku zinavyokwenda zinanywea na kufungamana na hizi tatu. Kambi hizo kuu tatu ni;

1/UFISADI(Lowassa Group)
Hii ndio yenye nguvu zaidi na inaogopewa na kambi zingine zote.
Sifa yao kuu ni Rushwa.

2/USULTANI(Membe Group) Hii inaungwa mkono na mtawala, inapigiwa debe usiku na mchana na familia ya JK.
Sifa yao kuu ni Usanii.


3/ZILIPENDWA(Sitta Group)
Hii inajumuisha makada wengi waliowahi kuongoza au kupata umaarufu ndani ya CCM na serikalini lakini kwa sasa hawana nafasi kubwa. Sifa yao kuu ni Unafiki.


*NOTE (Majina ya hizo kambi siyo rasmi bali ni utunzi wangu katika kufanya uchambuzi, lakini yanashahabiana na mfumo wa sifa za kundi husika)

Duh! Kiongozi wa hii kambi ya Pili (Membe) licha ya kufanana kwa USANII na anayemuunga mkono, vile vile wanafanana kwa SURA. Je ni Ndugu au? First lady kwa kupigania mjumbe wa NEC ni maandalizi ya kumuingiza huyu SHEMEJI/HOMEBOY?
 

na Grace Macha, Arusha


WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa amezidi kuwatimulia vumbi wapinzani wake ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), kutokana na wajumbe wanaounga mkono kambi yake kuzidi kupeta katika uchaguzi. Katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha uliomalizika jana, kambi mbili zinazowaunga mkono Lowassa na Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe katika mbio za urais 2015, zilionekana kutifuana vikali.

Msuguano huo ulianza kujitokeza tangu juzi kwenye uchaguzi wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa huo, ambapo juhudi za Katibu wa Mkoa, Mary Chatanda kutaka kuihujumu kambi ya Lowassa, ziligonga mwamba na kunusurika kipigo.
Chatanda ambaye alikuwa akifanya juhudi za kuhakikisha mshindi anakuwa Dk. Harold Adamson, aliambulia patupu baada ya Robinson Meitinyiku anayedaiwa kuungwa mkono na Lowassa, kushinda kwa kura 247 dhidi ya 188 za mpinzani wake.

Katika mwendelezo huo huo wa msuguano wa kambi hizo mbil, jana Katibu huyo CCM Mkoa wa Arusha, Chatanda, alijikuta akiaibishwa na wajumbe wa mkutano Mkuu wa chama baada ya kujifanya amesahau kumtambulisha Lowassa. Chatanda aliufanya ukumbi mzima kupiga kelele kubwa wakisema bado! bado! Bado Eddo! Eddo! Eddo! Na ndipo kwa aibu kubwa, katibu huyo akameza mate na kumtambulisha Lowassa.

Hata hivyo, hatua hiyo ilitafsiriwa tofauti na baadhi ya wajumbe ambapo wengine walisema ni tukio la bahati mbaya, lakini wengi wao wakidai kuwa Chatanda alifanya makusudi kutokana na kundi analoliunga mkono kuanguka kwenye uchaguzi wa UVCCM. Katika mkutano huo mkuu wa mkoa uliohudhuriwa na wajumbe 833, nafasi ya Mwenyekiti ilirudi tena kwa Onesmo ole Nangole ambaye anadaiwa kuunga mkono na Lowassa, akiwaacha kwa mbali washindani wake wawili.

Nangole alijizolea kura 604 huku akifuatiwa kwa mbali na Adam Choro wakati Dk. Salash Toure aliyedondoshwa na Lowassa kwenye uchaguzi wa ujumbe wa NEC Taifa kupitia wilayani Monduli akiambulia kura 13. Akitangaza matokeo hayo, msaimamizi mkuu wa uchaguzi huo, Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe, alisema kura zilizopigwa ni 833 ambapo kura halali zilikuwa 830 na tatu ziliharibika.

Mapema akifungua mkutano huo kabla ya uchaguzi, Prof. Maghembe, aliwataka wajumbe kuacha kuzomea au kushangilia wagombea pindi watakapofika mbele yao kujinadi. Alisema lengo la uchaguzi huo ni kupata viongozi watakaojenga chama kwa kuhakikisha wanavunja makundi na kuwaunganisha wanachama wote ili kuvirejesha viti vya udiwani na ubunge walivyovipoteza mkoani humo.
"Msichague viongozi watakaobweteka na kutugawa, hawa hawatufai, tuepuke viongozi wa aina hii, tuchague watakaokisaidia chama," alisema Maghembe.

Naye Lowassa, akizungumza baada ya kuchaguliwa na wajumbe kuwa mwenyekiti wa muda wa mkutano huo, aliwashukuru wote kwa imani waliyompa huku akishangiliwa kwa kishindo. "Wajumbe nimewaelewa na sitawaangusha, nimewaelewa ndugu zangu sitawaangusha, nawashukuru kwa kunishangilia, ila sasa tusishangilie tusije kuharibu utaratibu," alisema Lowassa.

Akijinadi kwa wajumbe hao, Nangole aliwaomba wamchague ili aweze kusimamia dosari zilizopo na kushughulika na watu wote wanaoleta makundi ndani ya chama kwa mgawanyiko kuanzia wilayani mpaka Mkoa.

Naye Dk. Toure, aliwaomba wajumbe hao kuwa akichaguliwa, atamaliza makundi yaliyopo ambayo yamekiathiri chama hicho kwani wanachama wamegawanyika kila ngazi na kuwasihi wawabwage wagombea waliotumia fedha kuomba kura kwenye uchaguzi huo.
Mgawanyiko ndani ya chama ulionekana kuzungumzwa na kila mtu kwani hata Chora, naye aliwaomba wajumbe wamchague ili tatizo hilo alilodai kuwa limewapotezea majimbo.
 
Back
Top Bottom