Kambi ya Lowassa Inapumulia Mashine ndani ya CCM, Ndoto za Urais zazidi kuota mbawa

Le Grand Alexei

Senior Member
Nov 9, 2011
116
83
Katika hali ya kushtusha kambi ya mwanasiasa mkongwe, mashuhuri na maarufu sana mh Edward Lowassa imezidi kuzorota ndani ya chama hicho kikongwe kilichojaa mizengwe na makundi makubwa ya kuwania urais 2015.

Kuzorota huko kumetokana na mambo mengi yakiwemo wasiwasi uliotanda ndani ya kambi hiyo kuwa waziri mkuu huyo mstaafu ana matatizo makubwa ya kiafya na hivyo kufifiza matumaini ya kuwa mgombea muafaka wa kambi hiyo. Hili linazidi kuwa kikwazo kwa kambi hiyo kwa kuwa Lowassa hapendi kuona mtu mwingine yeyote katika kambi hiyo anatamani kuwa rais zaidi ya yeye tu.

Habari za ndani ya kambi hiyo zinasema kuwa Lowassa alikorofishana na Emmanuel Nchimbi pale tu aliposema wawe na plan 'B' endapo itatokea kuwa yeye Lowassa ameshindwa kugombea Urais, na plan 'B' hiyo iwe kijana mwenye nguvu na afya bora kama Nchimbi! Toka aseme maneno hayo wakubwa hawa hawapatani tena kama zamani na kuna ushahidi kwamba Nchimbi haitwi tena kwenye vikao mbalimbali vya kambi hiyo.

Wasiwasi huo umeonekana ukisababisha uaminifu kwa kambi hiyo upungue nguvu sana na watu waanze kutazama fursa zilizopo kwenye makambi mengine yanayoibuka kila siku na kujikuta yakiwa na nguvu kubwa. wengi wanahisi anguko la Lowassa 2015 lisije kuwa anguko lao pia, wanaanza sasa kuchukua chao mapema.

Pamoja na sababu hiyo, nyingine kubwa inayotajwa kuisambaratisha kambi hiyo ni maamuzi magumu na yaliyoonekana kutoiunga mkono kambi hiyo yaliyofanywa na vikao mbalimbali vya maamuzi katika chama mfano maamuzi ya kuyafyeka majina ya watu walioonekana vinara wa siasa za kundi hilo kama akina Hussein Bashe, ambaye anaonekana kuwa ni nguzo muhimu ndani ya kambi hiyo yenye ufuasi kwa Lowassa, pia kuna vijana wengine ndani ya UVCCM waliokatwa majina yao bila sababu za msingi kujulikana - hapa mfano mzuri ni Naibu katibu mkuu wa UVCCM Zanzibar Jamal Kassim, aliyekuwa akigombea Uenyekiti wa Taifa wa UVCCM na aliyekuwa anapewa nafasi kubwa ya kushinda kama jina lake lingeteuliwa na NEC ya CCM, pia Sango Kasela ambaye aligombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti UVCCM

Sababu kubwa ya tatu ya kuanguka kwa kambi hii ni kushindwa kwa makada wa chama hicho kwenye chaguzi za ndani ya chama zinazoendelea - mfano mzuri ni Makongoro Mahanga, mbunge wa segerea na naibu waziri wa kazi, na kaka yake Didas Massaburi (Mzee wa kufikiria kwa kutumia makalio) ambaye pia ni mayor wa Dar es salaam, ambao walishindwa kwenye nafasi ya NEC japokuwa walitumia pesa nyingi.

Pia kuanguka kwa wafuasi wa kambi hiyo mkoani tabora - jambo linaloashiria kuanguka kwa ngome ya Rostam Azizi (mshirika mkubwa wa Lowassa) na kupotea kwa umuhimu wa Hussein Bashe aliyeonekana kutaka kurithi nafasi ya king maker Rostam. Mkoani Tabora hakuna wilaya hata moja iliyopata mwenyekiti wa chama mwenye mlengo wa kambi hiyo ya watu wenye pesa. Pia wajumbe wa Nec Nzega, Igunga (Peter Kafumu aliyemshinda mlinzi wa jimbo la Rostam Azizi na mwenye kiti wa halmashauri hiyo Mh Abubakari Shabani) hawapo katika kundi hilo. Je hii inamanisha Samwel Sita anajipanga ama ni matokeo tu?
 
makund ndan ya ccm yaendelee tu mana utengano n udhaifu il cdm wapete kilain mbeye ya magamba
 
Habari za ndani ya kambi hiyo zinasema kuwa Lowassa alikorofishana na Emmanuel Nchimbi pale tu aliposema wawe na plan 'B' endapo itatokea kuwa yeye Lowassa ameshindwa kugombea Urais, na plan 'B' hiyo iwe kijana mwenye nguvu na afya bora kama Nchimbi! Toka aseme maneno hayo wakubwa hawa hawapatani tena kama zamani na kuna ushahidi kwamba Nchimbi haitwi tena kwenye vikao mbalimbali vya kambi hiyo.

Mkuu hapo kwenye red bold, unadhani kweli wanaweza korofishana hawa, wametoka mbali sana, na EN anajulikana kuwa loyal kwa EL!!!

How credible this is!! Nachokubaliana na wewe ni kuwa EL kweli afya inayumba, ingawa hatumuombei mabaya!!
 
Kwenye siasa kuna assets na liabilities, you can only turn asset into a liabilitie but you can't turn a liability into asset!.

Mwanzo nilidhani EL ni asset ya CCM, kwa survivor ya 2015!, baada ya kuosoma mahali kuhusu "safety net" ya Billioni 400, then nime reach conclusssion 2015, ni CCM tena, with or without EL!.

He was once an asset, now he is a liability jiust like ZZK kwa Chadema.

Namna pekee ya turning liabilities into assets ni disposal off and salvage whatever is left na kuitop up kwenye re-investiment scheme!.
 
Ni kawaida yako kugeuka!
Mwanzo nilidhani EL ni asset ya CCM, kwa survivor ya 2015!, baada ya kuosoma mahali kuhusu "safety net" ya Billioni 400, then nime reach conclusssion 2015, ni CCM tena, with or without EL!
 
Mkuu hapo kwenye red bold, unadhani kweli wanaweza korofishana hawa, wametoka mbali sana, na EN anajulikana kuwa loyal kwa EL!!!

How credible this is!! Nachokubaliana na wewe ni kuwa EL kweli afya inayumba, ingawa hatumuombei mabaya!!

Nchimbi has always been close to mkweree na sio Lowassa!! He can afford to lose manvi but not mkweree for obvious reasons!!!
 
Pasco, unayosema ni kweli, lakini mwaka 2015 kunatisha?????
uchaguzi ukiwa objective, tunaweza kuona mengine
 
Kwenye siasa kuna assets na liabilities, you can only turn asset into a liabilitie but you can't turn a liability into asset!. Mwanzo nilidhani EL ni asset ya CCM, kwa survivor ya 2015!, baada ya kuosoma mahali kuhusu "safety net" ya Billioni 400, then nime reach conclusssion 2015, ni CCM tena, with or without EL!. He was once an asset, now he is a liability jiust like ZZK kwa Chadema. Namna pekee ya turning liabilities into assets ni disposal off and salvage whatever is left na kuitop up kwenye re-investiment scheme!.

Nashukuru kwani ukisharudi katk sense utagundu akuwa CCM ni liability long time nayo utaipiga chini.haupo mbali na
Kama kweli Mhe. EL alikubali kuwa kafara..basi sasa hivi anasubiri vinguvu vidogo kama Samsom.

Ama CCM iwe Liability,ama mgombea wake, ama wote kwa pamoja wawe liability na si vinginevyo.Subiri wakichagua yeyote kama atafika siku ya kuteuliwa na chama akiwa safi.Hata wa kuokota ambaye hakuwa katk system ataangushwa na chama.
 
Nchimbi has always been close to mkweree na sio Lowassa!! He can afford to lose manvi but not mkweree for obvious reasons!!!

Ndinani EN kuwa ndani ya serikali ya JK haina maana kuwa ni kijana wake!! Huna habari kuwa baada ya uchaguzi wa 2005, team yooote iliyoingia madarakani ilikuwa ya EL?!!! Kama huna habari uliza wanazi wa EL kama Pasco atakuhabarisha. EN na wengineo wengi tu ndani ya serikali ya JK ni loyalists wa EL, wanaishai na JK kinafiki tu!!!

Usidhani jina la king maker kwa El limekuja hivi hivi tu!! The guy sits around with really strategists, na ndo maana unamuona wameshindwa kumvua gamba pamoja na Chenge wake!!!!
 
Nchimbi has always been close to mkweree na sio Lowassa!! He can afford to lose manvi but not mkweree for obvious reasons!!!
Mtoa na mpokea rushwa WOTE MAZI GA NYANZA-by Nyerere wanahangaika kutafuta nani agombee Chadema wanapanga baraza la mawaziri la ukombozi na Uhuru......Lowasa wa Richmond,Nchimbi wa Mwangosi,Sitta wa Makinda,Membe wa Change ya Rada,Chenge wa Vijisenti,Bashe wa Somalia,Magufuli wakupiga mbizi kigamboni woteee Pumbaaaaaaaaavu kabisa na mkijifanya kukomaa na uraisi tunatia shaba tu hatulei mijizi sasahv
 
Ndinani EN kuwa ndani ya serikali ya JK haina maana kuwa ni kijana wake!! Huna habari kuwa baada ya uchaguzi wa 2005, team yooote iliyoingia madarakani ilikuwa ya EL?!!! Kama huna habari uliza wanazi wa EL kama Pasco atakuhabarisha. EN na wengineo wengi tu ndani ya serikali ya JK ni loyalists wa EL, wanaishai na JK kinafiki tu!!!

Usidhani jina la king maker kwa El limekuja hivi hivi tu!! The guy sits around with really strategists, na ndo maana unamuona wameshindwa kumvua gamba pamoja na Chenge wake!!!!

JK alikuwa nae ni wa EL.Kwani kupanda ndege wote hadi Dom Kifimbo akapiga chini ilikuwa mchezo.Dhaifu alibebwa tuu ili kuweka kampani kabla hajaona kuwa naye anaweza.
 
Ewe DHAIFU na wenzio muwekeni Lowasa hata kama ameinama kabisa ili nchi ibadilike bile ufisadi hatuna raisi 2015 kabisa.

Kwa kweli uwezekano wa CCM moja 2015 wuth EL candidate haupo! Dhaifu ndo atakayeibadili nchi hii, itakuwa kwa kuweka weak CCM au kwa kuleta katiba ya ukweli, tukose wote style!!
 
Mtoa na mpokea rushwa WOTE MAZI GA NYANZA-by Nyerere wanahangaika kutafuta nani agombee Chadema wanapanga baraza la mawaziri la ukombozi na Uhuru......Lowasa wa Richmond,Nchimbi wa Mwangosi,Sitta wa Makinda,Membe wa Change ya Rada,Chenge wa Vijisenti,Bashe wa Somalia,Magufuli wakupiga mbizi kigamboni woteee Pumbaaaaaaaaavu kabisa na mkijifanya kukomaa na uraisi tunatia shaba tu hatulei mijizi sasahv

Umemaliza mkuu
 
Katika hali ya kushtusha kambi ya mwanasiasa mkongwe, mashuhuri na maarufu sana mh Edward Lowassa imezidi kuzorota ndani ya chama hicho kikongwe kilichojaa mizengwe na makundi makubwa ya kuwania urais 2015.

Kuzorota huko kumetokana na mambo mengi yakiwemo wasiwasi uliotanda ndani ya kambi hiyo kuwa waziri mkuu huyo mstaafu ana matatizo makubwa ya kiafya na hivyo kufifiza matumaini ya kuwa mgombea muafaka wa kambi hiyo. Hili linazidi kuwa kikwazo kwa kambi hiyo kwa kuwa Lowassa hapendi kuona mtu mwingine yeyote katika kambi hiyo anatamani kuwa rais zaidi ya yeye tu....

Hujui unachoongea wewe..unamjua Lowassa au unamsikia?
 
Ni kawaida yako kugeuka!
Nafuata tuu principles of laws of motion na mambo ya genetics na mutatitions!. " Human being are not static!, they are dynamics and hence they change with time"!. My favourate ni EL, kwa vile with bilioni 400 za "safety net", EL now is a liability!, kwa sasa Membe ndie "asset"!, sisi tunacheza na timu ya washindi!.

"Kwenye politics, hakuna permanent friends or enemies, we only have a common interests!. Mimi interest yangu ni 2015, Taifa letu lipate ukombozi wa kweli wa pili wa Mtanzania!, nili bank on EL kuwa atatupatia ukombozi huo1, now he is a liability akisubiria disposal off, then, its my right not to sail with the sinking ship!. Kama hata Mzee Mwanakijiji anakutajia Membe!, the who are you kubisha!.
P.
 
Back
Top Bottom