Kambi rasmi za upinzani na uwaziri vivuli ni hasara au faida kwa wapinzani?

WATANABE

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
1,092
466
Nianze thread yangu kwa kukumbusha kuwa katika Bunge lililopita 2005-10 chama cha CUF kilikuwa ndio kilikuwa na wabunge wengi na hivyo kuunda Kambi rasmi ya upinzani na kuteua mawaziri vivuli. Katika uchaguzi Mkuu wa 2010 watanzania bara wakaamua kuchagua wabunge wengi wa upinzani toka chama cha CDM. Hii moja kwa moja ni kutokana na kutoridhishwa na utendaji wa chama na wabunge wa CUF.


Nimeanza na utangulizi huu nikiwa na nia ya kuwafikirisha wasomaji wangu ambao ni wapenzi wa Upinzani hapa nchini kuufanyia utafiti uelewa wa watanzania kuhusu mfumo wa Bunge letu wa kuwa na Kambi Rasmi ya Upinzani na Mawaziri Vivuli, na jinsi watanzania wanavyoonyesha kuutumia katika vigezo vya kuwapima wabunge wanaofaa kuchaguliwa tena.

Nikizingatia ukweli kuwa watanzania wenye uwezo wa kupata fursa ya kusikilzia hotuba za Mawaziri Vivuli katika runinga, tena moja tu ya TBC, tena katika masaa ya kazi ambapo watanzani walio wengi wako katika harakati mbali mbali za kuhakikisha wanapata fedha za kununua mahitaji ya siku husika. Ni dhahiri kuwa wanaopata fursa hiyo ni wachache sana, na hata hao wanaopata hawawezi kuwa na utulivu wa kuelewa kwa kina mantii nzima ya hotuba husika.

Aidha kwa kuwa hotuba hizo huchapwa katika magazeti mbali mbali, ushahidi unaonyesha kuwa watanzania wenye “hobby” ya kujisomea ni wachache sana kiasi cha kuathri sekta nzima ya uchapishaji kiuchumi; hivyo upungufu huu pia utakuwa na atahari kubwa katika usomwaji wa hotuba za Mawaziri Vivuli.

Kutokana na hayo ni mtazamo wangu kuwa haishangazi idadi kubwa ya watanzania wengi kupuuza kazi nzito inayofanywa na mfumo wa kamabi Rasmi ya Upinzania pamoja na Mawaziri Vivuli inayohusisha kufuatilia utendaji wa wizara husika, kutafuta ushahidi wa mapungufu yaliyojitokeza kutayarisha hotuba na nyaraka mbali mbali na kujipanga kusoma hotuba za Mawaziri Vivuli katika bunge. Ni dhahiri kuwa muda Mawziri Vivuli wanaoutumia katika shughuli hizi ni mwingi sana kiasi cha kuathiri utendaji wao kwa wapiga kura wao na kupoteza matumaini ya wananchi waliyokuwa nayo juu ya mbunge husika. Kwa mtazamo wangu hali hii ilichangia sana kupunguza umaarufu na hatimaye kura za wabunge toka chama cha CUF katika uchaguzi mkuu wa 2010.

Nikiwa na wazo hili kichwani nilitazama kwa kina ushiriki wa wabunge wa CDM ambao waliingizwa bungeni kwa matumaini makubwa toka kwa wananchi katika bunge hili lililoanza Juni 2012. Hii ni bajeti ya pili CDM ikiwa ni Kambi Rasmi ya upinzania hivyo kuunda Mawaziri Vivuli.

Nini maoni yako kuhusu mapokeo ya wananchi kuhusu jukumu hili la wapinzani.

Je kiwango cha uwekezaji wa muda wa kuwahudumia wapiga kura, raslimali na ufanisi wa mbunge husika wa wabunge ambao ni mawaziri vivuli ili kuweza kuwa na hotuba inayostahili kinaweza kuleta tija iliyokusudiwa kwa wananchi, chama na kutimiza matarajio ya wananchi na wapiga kura wa jimbo atakalo mbunge au ndio itakuwa hadithi ya kubadili chama kikuu cha upinzani kama CCM itashinda kila bada ya uchaguzi mkuu kutokana na chama na wabunge wake kuonekana kupwaya kutokana na kupoteza muda mwingi wakifanya kazi ( kufuatilia utendaji wa wizara, kutayarisha bajeti na hotuba) ambazo mawaziri wa Serikali hufanyiwa na wataalamu lukuki walioajiriwa katika wizara mbali mbali?.

Je kama hali ndio hii kile wanachi wanachona ni kupwaya kwa chama na wabunge toka kamabi rasmi ya upinzani kinaweza kutafisiriwa ni kutokana na kukubali kuvikwa vilemba vya ukoka kuwa wabunge hao ni "MAWAZIRI HEWA" na hivyo kuwa na majukumu yanagharimu muda mwingi na utendaji wao? Kama hii ni ukweli CDM wafanya nini kujinasua katika mtego huu?
 
Back
Top Bottom