Kambayuwayu ka Kikwete kalikotaka kuwa tetere!

Du! Hao ndege wazee, wasio na manyoya tena waliwezaje kuruka hadi kwenye mkutano wa Mkwere in time, at a very short notice?
 
This time JK alikuja na nguvu kubwa ya hoja na data. Aliwaanika pabaya hao viongozi wa mbayuwayu na kuwaita waongo (whichis a bit too strong and undiplomatic)lakini hoja ilifika mahali pake. Viongozi wa wafanyakazi wanatakiwa kukaa na kujiangalia kama wanazo hoja zinazoweza kukubaliwa na kupambwa na data. Haiwezekani wafanyakazi wakala mapato yote ya nchi na kuacha hamna hela ya maendeleo mengine.

Kikwete alisema kwa maneno yake mwenyewe kuwa asilimia 30 ya bajeti ya kila mwaka huishia mikononi mwa mafisadi (siyo wafanyakazi). Kiasi hicho kingetosha kutoa nyongeza ya karibu shs laki 4.3 kwa kila mfanyakazi bila kujali kigezo kingine chochote. Wanaokula mapato "yote" ya nchi ni wamafisadi siyo wafanyakazi! Kwa hilo hakuwa na hoja!!


tatizo ninaloliona ni kwamba wakati hizo hela za kuwapa hazipo

Ndio tatizo hilo! Kwa vile "Rais kasema hazipo" basi wote mnaamini kuwa hazipo! Gavana wa Benki Kuu analipwa karibu dola elfu 15 pamoja na posho nyingine na nyumba na ulinzi! Hivi tukisema tuondoa elfu 8 na kumuachia hivyo vitu vingine, hizo elfu nane kwa kima cha chini cha 350 (nimeweka parity ya dola 1 kwa tsh 1000) ni watu wangapi wangeweza kuajiriwa kwa mwezi? - Jibu ni watu 22! bado unaamini hazipo?

Tukikata kiasi cha Tsh. 500,000 toka kwa malipo ya wabunge wote kwa mwezi, tungeweza kukusanya - tungeweza kuwalipa watu 460 kiasi cha 350,000 kwa mwezi! bado unaona hazipo

Ningeweza kwenda kwa kuangalia kuwapunguzia walio juu mishahaya yao japo kwa wastani wa dola 500 tu, ungeona kuwa tungeweza kuajiri watu wengine kwa malipo mazuri tu.



lakini mbayuwayu wanawaona wateule wakiendelea kununua mashangingi na kujilipa posho nono.

Lakini umesema fedha hazipo!!!

JK angefaulu zaidi kama angesema maneno yote hayo lakini akaonyesha mfano kwa kubana matumizi kwa watendaje wake vile vile. Inaumiza sana kuona kiongozi ananunua landcruiser V8 bila aibu yoyote.

aone aibu ya nini wakati mnaamini Rais kasema fedha hazipo na nyinyi mnakubali wakati macho yenu yanawaambia vingine?
 
Aliionyesha hasira kama hizo pale Airport wakati jamaa wa itifaki waliposhindwa kuandaa gari la Mapokezi kwa ajili ya First Lady wa mgeni wake,Pia pale alipokuja mkurugenzi wa wilaya ya Ngorongoro... Basi...

au pale penye magari ya ambulance! all in wrong places!
 
Sijui tukiite kituko ama kioja cha mkwere, anacha hoja analeta taarabu na misuto ya UWT? eti wanaweka saini wanachukua posho za vikao si zao? mbona kina kapuya pia wanachukua za vikao hivyo hivyo? huyu mwenye shamba hajua nani anayemlisha? kinamuuma wenye mali wakichukua chao ila yeye na watu wake wale cha wenzao? halafu eti mie ndio muajiri wenu anajidanganya na msala upitao? hao mbayuwayu uliwakuta sio wako na utawaacha wako wako nyumbani kwako mikocheni hata hao wa ikulu huwezi kutamba kwamba wako, aliwaacha Mkapa, Mwinyi na hata wengine wa Nyerere kama mtoto wa mkulima wewe wakupita tu sawa na upepo wa vuli. Nimeshangaa kusikia kiongozi anayedai haihitaji kura za civil service, anatukana wakunga? halafu anadiriki kutoa amri ya vyombo vya dola kuua watu? anahamasisha kimbari? kakuta wenzake wametengeneza amani? halafu tunamchekea? historia itasema mahakama ziko hajifunzi ya taylor? alitamba mobutu atakua yeye? sasa tuone na wahadhiri wa vyuo vikuu pia atawapiga risasi? halafu hawa wazee wanatia aibu sana hata miiko wameisahau, wenzao walivuliwa nguo salender bridge wao wanaona sawa? watoto wao wananyimwa haki wao wanashangilia? mwenye shamba hana ufahamu hajui kwamba Mgaya ni muwakilishi wa watu anamtangazia vita? ujumbe aupate hatumtaki na hatufai ajue kabisa anatawala kwa mabavu na sio kwa ridhaa na atang'olewa tu. Bravo Mbayuwayu ku retreat sio kushindwa twendeni kwenye go slow ili hata hizo za kuliwa na mashoga zake zikosekane. Bravo Mwanakijiji kwa kutuunganisha
 
Kutokana na uelewa huo mbayuwayu walidhamiria kuona kuwa shamba hilo linaenda kwa mtu mwingine au apewe mkulima mwingine mwenye kujali maslahi ya ndege wote siyo wale tu wenye sauti nzuri na rangi za kuvutia kama tetere!

Nimeipenda hii mkuu. Hiyo ndio changamoto kwa mbayuwayu wote na familia zao.


 
hii imekaa vizuri sana mkuu. mbayuwayu wamemtikisa sana mkwere so far. nina imani mbayuwayu hawatatulia, tena walivo wepesi! wanajipanga tu watamsumbua mkwere hadi atajuuuuuuuuuuuuuuta kuwaongoza mbayuwayu!!
 
Nimesikia mapinduzi ya machungwa na mapinduzi ya mierezi.. nadhani mwaka huu tutaona mapinduzi ya mbayuwayu!!
 
Mbayu mbayu watajuuuta kuwa na mnayapara kama mkwere hafai hata kulumangia
 
Halafu alimaanisha nini kuwepo kwa viongozi wale wote wa juu wa taasisi za usalama kwa swala la 'utaratibu wa kuhutubia wananchi'? Hopeless
 
Kikwete has once again demonstrated that he is a pathetic lightweight who only managed to climb the ranks of CCM due to patronism and a lack of meritocracy. Mtu aliyepitia pressure za a meritocracy hawezi kuwa feebly minded kama hivi.

Which points to a bigger problem than Kikwete. Right now we have a snowball's chance in hell of getting a capable leader, because we lack the required meritocracy.

Kwa hiyo if you think Kikwete is the worst we can do we subiri utakaposikia siku moja mjinga mjinga mmoja kama Emmanuel Nchimbi anakuja kuwa rais, watu tunabaki midomo wazi. Hatuna meritocracy, CCM na Politburo yake vinaamua rais wananchi wanapitisha tu.

Tulipopewa Mwinyi tukafikiri that was the worst, now Kikwete is proving us wrong, and I bet it is going downhill from here.

I hope I am wrong, but the facts tell me otherwise.
 
Suala la mbayuwayu limemfikia baba mwenye nyumba wa sasa. Lakini naona na yeye alikuwa anajaribu kunasua mbavu zake maana aikuwa amebanwa vibaya. Sina uhakika kama wawindaji wangemsaidia katika hilo kwani hata wao wana machungu yao.
Ila inabidi asome alama za nyakati kwa maana amewatukana waliokuwa wakimsaidia kuiba karatasi za kisomo (Oct 2010). Sasa nani atasimama mahala hapo. Sikuwa nautaka ubaba mwenye nyumba lakini kwa turufu hii aliyotoa na mimi nachukua fomu mwaka huu.

Byebye syesyemu
 
Mzee


Nilikuwa najiuliza mbona umeaka kimya ..

Nilikuwa na mpango wa kuandika shairi la mbayuwayu..

Nyani haoni kondole lake..


Basdo natafakari kichungaji!
 
Mzee Mwanakijiji

Hii naomba uichapishe..itoke na tuone salva ataijibu vipi?

alishindwa Mmasai je huyu ataweza..

Narudi rasmi siku si nyingi...

Kulikuwa na haja gani ya kuwa na CDF kama hata walimu wenyewe wana maisah duni?kuna haja gani ya kuongeza Taasisi zingine?
 
mzee mwanakijiji homgera sana, wewe ni mwanafalsafa duu akilli ni nywele changanya na zako.
 
Du! Kunashuka mistari hapa balaa!!! Mod... Naomba ubadilishe name yangu nataka kuitwa Mbayuwayu... Mwanakijiji nastahili?
 
Mzee Mwanakijiji

Hii naomba uichapishe..itoke na tuone salva ataijibu vipi?

alishindwa Mmasai je huyu ataweza..

Narudi rasmi siku si nyingi...

Kulikuwa na haja gani ya kuwa na CDF kama hata walimu wenyewe wana maisah duni?kuna haja gani ya kuongeza Taasisi zingine?

inatoka kesho mkuu...wakati naenda kulala jana nilikuwa nimesikia hicho kisa cha mbayuwayu wa Kikwete.. kikaa nikaa kichwani hadi nikaota ninaandamana nakundi la mbayuwayu!!
 
Back
Top Bottom