Kamba aliyojinyongea mtu au Kabanga ina siri gani?

Segito wa Kalenga

JF-Expert Member
Aug 28, 2014
609
855
Habari zenyu wadau wote wa JF!

Ni matumaini yangu kuwa mnaendelea vyema na ujenzi wa Taifa.

Mwaka jana nilipata tatizo la ndugu yangu kujinyonga nyumbani kwangu.Kama ujuavyo sisi tuliopo nje ya nchi hutuchukua muda mrefu kupanga mazishi juu ya kusafirisha kurudisha msiba nyumbani.

Sasa nilikabidhiwa vitu vya marehemu ikiwemo nguo,vyeti na kamba aliojinyongea ambayo wa kwetu walisisitiza nirudi nayo. Tulizika salama tukamaliza msiba na kusahau.hayo yote ni mwaka jana mwanzoni.

Nikiwa sina hili wala lile jana usiku nilipata wageni watatu. Siwajui na wala sijawahi kuwaona. Walijitambulisha na wakasema wamekua wakinitafuta saaana. Shida yao kwangu ni ile kamba aliojinyongea nayo marehemu.

Nilishangaa sana. Nikawauliza nyie mwaitaka ya kazi gani? Wakacheka na kusema hata wao hawajui ila kuna mtu yupo Congo amewaagiza. Waliahidi kunipa Dola za Marekani 10,000 cash. Niliwajibu kama ndugu zangu waliichoma baada ya kumaliza msiba kwa hivi sina nayo tena. Walisikitika wakaondoka.

Ukweli ni kwamba ninayo hiyo kamba na haikuchomwa. Ila kabla sijawapa nataka nijue kwanini wanaitaka hiyo kamba vibaya sana na wanatoa pesa nyingi kiasi hicho kwa ajili ya kamba tu au kuna siri gani iliojificha?

Natanguliza shukrani na nasubiri kuwasoma.

Asanteni sana.

=========

Ushirikina unatumia vitu vingi na tofauti tofauti ili vyombo vikamilike, kuna vitu ambavyo ni rahisi kuvipata katika mazingira yetu kama vile baadhi ya miti, michanga ya kaburi, udongo wa kichuguu nk

Kuna vitu ambavyo ni vya kuhangaikia ama uvipate kwa bahati navyo ni kondo la uzazi, kitovu cha mtoto, mfupa wa mtu, kamba ya mtu aliyojinyongea, majivu ya nyumba iliyoungua au mtu, nyoka aliyekufa, maji ya kuoshea maiti nk

Hivi na vinginevyo ni rasilimali kubwa katika uchawi na wakati mwengine inabidi mtu kutoa pesa nyingi au kwenda mbali kuvitafuta, kwani nguvu ya uchawi inategemea na vitendea kazi unavyotumia (vyachira)

Tunapozungumzia uchawi wengi hujenga picha kuwa mchawi ni mtu masikini kabisa, hapana......wapo wachawi wakubwa na wenye pesa nyingi na hawa wapo tayari kununua chochote au hata kuua ili mradi wajiimarishe zaidi katika walichokusudia (rejea wanaohitaji ndg zetu albino)

Katika uchawi ni kama sayansi nyingine, huyu anaweza kutumia chuma kupasulia nazi, yule akatumia chuma kutengeneza mitambo na mwengine akatumia kujengea daraja ndivyo ulivyo uchawi vifaa vyake havina matumizi ya aina moja.

KAMBA YA ALIYEJINYONGA

Hii tayari imetenda, imeua na katika uchawi hii inafanyiwa vyombo na ikachanganywa na dawa nyingine ikatumika kuua kwa manuizi tu (kama ulivyomuua fulani basi na fulani afe)

Sasa mchawi ananufaikaje mtu huyo akifa?
Hana lazima akaua mtu ila kitendo cha kuwa na dawa hiyo tu wenzake watamfuata hata kwa pesa awapatie kiasi.

Pia hutumika katika mengi zaidi...

Uchawi unatokana na vitu halisi na ndani yake kuna nguvu za kiroho
Mfano udongo wa nyumba iliyohamwa unaweza kutumiwa kukuhamisha kazini, nyumban nk

Kaburi linaweza tumiwa kukufunga kauli nk nk
 
KAMBA KWA DOLA 10,000. SI UNGWAPA TU BADALA YA KUBAKI NAYO HUKU IKIKUONGEZEA MASWALI NA UZUNI KIBAO.
Mkuu mbele ya kuwapa hiyo kamba napaswa nijue kwanini wanaitaka vibaya sana?Kama wao watanipa mimi hiyo pesa wao watapata pesa ngapi?Mjini hapa!Na hivi nipo na njaa ya maajabu plus sina kazi mwaka wa pili huu naishi kwa kuunga unga hell no.Siwezi.
 
Back
Top Bottom