ILI kuhakikisha kwamba wanaotoa ahadi katika kampeni zinazoendelea hivi sasa wanazitekeleza, tena wanazitekeleza kwa wakati ninapendekeza kuundwa kwa kamati kuu ya kufuatilia ahadi za kitaifa na zile za kimkoa na kiwilaya kwa upande mmoja na kwa upande mwingine kamati za kimajimbo za kufuatilia ahadi kwa kila jimbo na kila kata.
Haifai kusema tu hatudanganyiki. Muhimu zaidi ni kuhakikisha kuwa wanaogombea udiwani, ubunge na urais wanapopiga kampeni zao wanatoa ahadi zinazowezekana lakini sio kuropoka tu majukwaani ili mradi washinde.
Lazima ijulikane kwa siku zake 100 za kwanza kiongozi anayechaguliwa atafanya nini na kisha kila robo mwaka, nusu mwaka na kila baada ya mwaka lazima pawe na tathmini inayoonesha ubora au udhaifu wake.
Iwepo sheria katika katiba mpya ya kumaliza muda wa ubunge wa mtu katikati ya njia bila kungoja miaka mitano.
Kamati hizi za ufuatiliaji hapa Tanzania zitachangia sio haba katika kuharakisha juhudi zetu za maendeleo na kuufukuza umasikini kwa kasi kubwa kuliko ilivyo hivi sasa.