Kamati za bunge zinapashwa kujiepusha na kufanya kazi za kiutendaji

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Hivi karibuni kamati ya bunge ya nishati na madini imeunda kamati ndogo ya kuchunguza kiini cha uchakachuaji wa mafuta ya petroli. Kwa maoni yangu, hatua hiyo haikustahili, kwani kuna vyombo husika ambavyo kamati hiyo ingeliviagiza kufanya utafiti huo; hii ikiwa ni pamoja na EWURA na hata wizara yenyewe. Kama vyombo hivyo vingelishindwa au vingelipuuzia kufanya utafiti huo baada ya maelekezo hayo, basi kamati ingelichukua hatua ya kuwaripoti watendaji wakuu wa vyombo hivyo kwa mamlaka zao za ajira ili wachukuliwe hatua za kinidhamu.
 
Uchakachuaji ni tatizo la muda mrefu na hao watendaji walikuwepo. Acha kamati za Bunge zifanye kazi. Hatua ya kamati ndogo ni sahihi na itasaidia sana kulielewa tatizo kwa undani. Hao watendaji wanalipwa kufanya kazi na hawafanyi! Nao naamini watakuwa sehemu ya uchunguzi.
 
At the end of the day,the ad hoc committee is going to make unenforceable decisions.Enforcement is the major issue here,y'all need to motivate,not regulate!....I hope you get it,if not I can explain.
 
Kuna ombwe la uongozi katika nchi ndo maana kila mmoja anafanya anachotaka, Mrema ameshaanza kukata watu mishahara sijui madaraka hayo amepewa na nani kisheria, na wengienwengi. In other words our country is disorganized and consequently there is no chain of command.
 
Hivi karibuni kamati ya bunge ya nishati na madini imeunda kamati ndogo ya kuchunguza kiini cha uchakachuaji wa mafuta ya petroli. Kwa maoni yangu, hatua hiyo haikustahili, kwani kuna vyombo husika ambavyo kamati hiyo ingeliviagiza kufanya utafiti huo; hii ikiwa ni pamoja na EWURA na hata wizara yenyewe. Kama vyombo hivyo vingelishindwa au vingelipuuzia kufanya utafiti huo baada ya maelekezo hayo, basi kamati ingelichukua hatua ya kuwaripoti watendaji wakuu wa vyombo hivyo kwa mamlaka zao za ajira ili wachukuliwe hatua za kinidhamu.

Hivi karibuni ni kweli kamati za bunge zimejitokeza ni kufanya kazi za kiutendaji badala ya kuwa Oversight institution. Katika muktadha wa utawala bora kamati zinatakiwa ziwe zinahoji na wala siyo zenyewe kuingilia shuughuli za utendaji kwani mambo yakiharibika nani atawahoji wakati wenyewe walishiriki katika utendaji. Kiboko ni hii ya Mrema kuwachukulia hatua za kukata mishahara watendaji wa serikali. Kamti kila siku ziko kwenye ofisi za watendaji, ziwaache watendaji watende nazo zihoji na kuelekeza.
 
Kuwa wizara ifanye uchunguzi endapo itashindwa tume ikawaripoti wizarani are you serious.
 
Hivi karibuni ni kweli kamati za bunge zimejitokeza ni kufanya kazi za kiutendaji badala ya kuwa Oversight institution. Katika muktadha wa utawala bora kamati zinatakiwa ziwe zinahoji na wala siyo zenyewe kuingilia shuughuli za utendaji kwani mambo yakiharibika nani atawahoji wakati wenyewe walishiriki katika utendaji. Kiboko ni hii ya Mrema kuwachukulia hatua za kukata mishahara watendaji wa serikali. Kamti kila siku ziko kwenye ofisi za watendaji, ziwaache watendaji watende nazo zihoji na kuelekeza.
ni kulewa madaraka na katiba mbovu,si sahihi kamati za bunge kujifanya watendaji,na wamezidi kuropoka kumbuka kamati ya zitto kuishinikiza nssf kufanya mradi wa umeme!!!,hovyo kabisa na ndiyo maana mwisho inakuwa kama dowans
 
Kama kamati inashinikiza utekelezaji w mradi itakuwaje mradi huo ukiwa bogus nani atamhoji nani? Nadhani kamati za bunge zimeanza kutumiwa na mafisadi wanaotaka kufanya mambo yao. Bunge likiendelea hivi litakosa sifa ya kuwa chomba cha kuisimamia na kuihoji serikali bali litakuwa sehemu ya serikali kwa maana ya executive.
 
Back
Top Bottom