Mtoboasiri
JF-Expert Member
- Aug 6, 2009
- 5,101
- 1,946
Kamati ya Zitto yatabiri kifo cha TBC
NA RICHARD MAKORE
24th May 2011
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), imesema Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) liko hatarini kufirisika na kufa kama ilivyotokea kwa mashirika mengi ya umma hapa nchini kwa kuwa kumebainika kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha pamoja na kushindwa kukusanya madeni yanayofikia Sh. bilioni 4.8.
Kadhalika, kamati hiyo imeshangazwa na TBC kuingia mkataba wa kufanya biashara na kampuni ya Star Media bila kuijulisha Wizara ya Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo ambayo shirika hilo lipo chini yake.
Mjumbe wa kamati hiyo ambaye ni mbunge wa Jimbo la Mwibara mkoani Mara (CCM), Alphaxard Lugola alisema matumizi mabaya ya fedha kunatishia kuliua shirika hilo la umma.
Alisema TBC lilipoanza wakati huo likiitwa TVT lilikuwa likienda vizuri lakini bahati mbaya hivi sasa linaelekea kufirisika na hatimaye kufa kabisa.
Kwa mwenendo huu wa mahesabu TBC halina muda mrefu kuendelea kuwepo kwa kuwa mmeshindwa kudhibiti matumizi yenu pamoja na kuwa wakali katika kukusanya madeni yenu alisema.
Aliongeza kuwa baada ya kusoma vitabu vya mahesabu ambavyo vilikabidhiwa kwa kamati alibaini kwamba Shilingi bilioni nane zilitumika kununua mafuta ya magari bila kufuata taratibu za manunuzi.
Alikiri kuwa hakuna uhalali wotote wa matumizi ya fedha hizo kwa ajili ya kujaza mafuta ya magari katika kituo cha mafuta cha Victoria cha jijini Dar es Salaam.
Alisema makubalinao ya mkataba wa kujaza mafuta hayo yalifanywa kwa mdomo badala ya maandishi kama sheria na taratibu za manunuzi ya serikali zinavyosema.
Kuhusu mkataba kati ya TBC Star Media, wajumbe hao walisema ulisainiwa kirafiki bila hata wizara inyosimamia shirika hilo kujulishwa.
Baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo walihoji kwa nini TBC inazidi kuporomoka badala ya kupanda kama ilivyoanza huko nyuma.
Makamu mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe, aliiambia kamati hiyo kuwa siku za TBC kuendelea kuwepo zinahesabika.
Alisema TBC inakabiliwa na uhaba wa fedha za kuiendesha hatua ambayo imeanza kusababisha matatizo ikiwemo Televisheni yake kushindwa kufika baadhi ya mikoa hapa nchini.
Kwa upande wake, uongozi wa TBC ulikiri kuwa matangazo yao hivi sasa hayawafikii wananchi wengi kutokana na mitambo yake kuchakaa na kwamba hakuna fedha za kuweza kununua mipya.
Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Clement Mshana alijaribu kutoa majibu kwa kamati hiyo lakini mara kadhaa wajumbe wake walimkatisha baada ya kuhisi kama yalikuwa hayajitoshelezi.
Kuhusu ukusanyaji wa madeni ya TBC kutoka taasisi za umma, Mshana alisema wameajiri kampuni ya udalali ya Majembe kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.
CHANZO: NIPASHE