Kamati ya Ngwilizi yawatia hatiani Prof. Muhongo na Eliakim Maswi, yawasafisha Zitto na wenzake!

Mwikimbi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,762
825
Tuliwahi kuandika hapa jamvini kuwa mwishoni mwa siku ZITo ataibuka mshindi, someni nnipashe leo. sakata la wale wabunge wanaotuhumiwa kula rishwa sasa ni wazi limefikia mwisho, na badala yake PROFESA NA MWASWI ndo watuhumiwa wa kwanza kwa kupindisha taratibu za manunuzi.

Ni vema wananchi kuwaelewa viongozi wao, hasa wanapotaka kuugeuza ukweli kuwa uongo ili kushangiliwa. nani asiyejua kuwa nchi ipo kwenye mgao mkali wa umeme? lakini wafanyakazi waTanesco wameonywa kuwa endapo mtu atasema ukweli kuhusu mgao unaondelea atafukuzwa kazi.

Nchi ya waongo wanaoishi kwa kusema uongo, hata profesa anakuwa sehemu ya uongo!!!!
 
tuliwahi kuandika hapa jamvini kuwa mwishoni mwa siku ZITo ataibuka mshindi, someni nnipashe leo. sakata la wale wabunge wanaotuhumiwa kula rishwa sasa ni wazi limefikia mwisho, na badala yake PROFESA NA MWASWI ndo watuhumiwa wa kwanza kwa kupindisha taratibu za manunuzi. ni vema wananchi kuwaelewa viongozi wao, hasa wanapotaka kuugeuza ukweli kuwa uongo ili kushangiliwa. nani asiyejua kuwa nchi ipo kwenye mgao mkali wa umeme? lakini wafanyakazi waTanesco wameonywa kuwa endapo mtu atasema ukweli kuhusu mgao unaondelea atafukuzwa kazi. nchi ya waongo wanaoishi kwa kusema uongo, hata profesa anakuwa sehemu ya uongo!!!!

Hapa tanzania ndipo msemo huu unafanyakazi:" MKUKI KWA NGURUWE KWA BINADAMU MCHUNGU" Serikali inapounda kamati inakuwa siyo huru, lakini BUNGE linapounda kamati kujichunguza kamati hiyo inakuwa huru kweli kweli. Hivi matokeo ya kamati hii yanakubaliwa kuwa ni sahihi kwa sababu imetenda haki? kwa kuwa watuhumiwa walikuwa si wa chama kimoja? au watanzania sasa tumeshakuwa mazezeta wa kuwamini kuwa kila lisemwalo na wabunge ni sahihi? Binafsi ningefurahi kama ingeundwa tume nje ya Bunge ili tuone kama itakuja na majibu yanayofanana.
 
he! sasa umeshaambiwa chanzo ni gazeti la nipashe, kanunue gazeti au azima then ndo ujue ukweli, sasa kuniita mkuda kwan i miye ndo nilikuwa mwanakamati? tatizo mnataka kuambiwa uongo,sasa ngwilizi kaupata ukweli hamuamini. siku mtakaposikia kuwa magufuli ni mla rushwa namba wani kupitia taasisi za umma kama SUMAJKT, TBA NDO HAMTAAMINI KABISAAAAA
 
Tanganyika ya wadanganyika, hizo nguzo zinazotolewa na kupelekwa Mombasa na kurudi nazo wamezingelea au wameishia kubwabwaja tu kuhusu kanuni na sheria za manunuzi? Tangu mwanzo tulijua kuwa walikiuka hizo kanuni za kifisadi lakini kwa maslahi mapana ya umma. Bei ya kulipia nguzo moja ya umeme ilikuwa shilingi ngapi kabla ya Maswi na Profesa kuingia wizarani na sasa ni shilingi ngapi?
Kamati ya Ngwilizi, huyu ambaye ana hekaru kule Lushoto pamoja na Ben? I will be the last to trust them.
 
Ndugu zangu niliandika hapa jukwaani jinsi William lukuvi kwa kusaidiana na maswi walitengeneza zile tuhuma ili kuondoa concentration ya nini kijadiliwe kwenye bajeti ya nishati, na walifanikiwa sana, ni kweli kuna wabunge wanafanya biashara na tanesco wapo, taarifa imewataja na Bahati nzuri,wote ni ccm. Kamati haijathibitisha rushwa yeyote na badala yake inayeonekana alikula rushwa ni maswi , kwa nini aliondoka akaenda mlango wa nyuma akaipa zanuni kampuni ya puma kisa Ina bei ndogo bila kuziuliza kampuni zingine ukizingatia kuwa hapo awali puma alibid kwa bei kubwa? Sasa wameumbuka wakiwamo waliotaka kushambulia Akina zitto kisa tu wanasema sheria ifuatwe, nimeongea na j Mushi , nitaiweka hiyo taarifa ya bunge hapa wiki hii.
 
lakini wafanyakazi waTanesco wameonywa kuwa endapo mtu atasema ukweli kuhusu mgao unaondelea atafukuzwa kazi. nchi ya waongo wanaoishi kwa kusema uongo, hata profesa anakuwa sehemu ya uongo!!!!

Haya magazeti nayo siku hizi hayaaminiki. Yanaandika habari za mtaani. Mfano vyombo vingi vya habari vya Kenya viliweka habari ya balozi wa Tanzania kufukuzwa Malawi

Hata hivyo kusema ukweli nimeanza kumstukia prof Muhongo. Alitoa ahadi ya wiki mbili kufanya mapitio ya mikataba kisha umma ujulishwe. Mwezi unaisha bila bila
 
badala yake inayeonekana alikula rushwa ni maswi , kwa nini aliondoka akaenda mlango wa nyuma akaipa zanuni kampuni ya puma kisa Ina bei ndogo bila kuziuliza kampuni zingine ukizingatia kuwa hapo awali puma alibid kwa bei kubwa?
Kwahilo mimi bado niko upande wa Maswi. Kama nakumbuka alisema sheria hiyo ya manunuzi inampa uhuru wa kufanya maamuzi yenye maslahi kwa taifa. Sasa kama bei imepunguzwa tatizo lipo wapi?
 
Tuangalie na history, hivi sakata la Mtungi na Maswi pale UDSM mwaka 1994 nani alikuwa mkweli na kusimamia haki ya wengi? Na alipokuwa wizara ya TAMISEMI record zinasemaje? Na pale Ministry of Finance ilikuwaje? Kama kote ni safi, iweje kwenye nishati awe mchafu?! Mbona wengi wanaopitia wizara ya nishati wanageuka au ni wachafu? shida ni wao au wenye nguvu walionyuma ya pazia?
 
Tanganyika ya wadanganyika, hizo nguzo zinazotolewa na kupelekwa Mombasa na kurudi nazo wamezingelea au wameishia kubwabwaja tu kuhusu kanuni na sheria za manunuzi? Tangu mwanzo tulijua kuwa walikiuka hizo kanuni za kifisadi lakini kwa maslahi mapana ya umma.

Pamoja sana, mkuu
 
Unajidanganya ukweli na uongo inatokana na mazingira utayokutana nayo sio suala kua Profesa wala nini mimi naamini aliyekua hajawai kudanganya ni mmoja tuuuuuuuuuuuuuu
 
Hivi hakuna mgongano wa maslahi kwa wabunge kuwa wajumbe wa kamati inayochunguza tuhuma dhidi ya wabunge wengine wa bunge hilohilo? Hii kisheria imekaaje? Haki inaweza kutendeka au kuonekana kuwa imetendeka katika mazingira kama hayo?
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom