Kamati ya Nchimbi Inaingilia Uhuru wa Mahakama

Tumesikia hilo kuwa kuna maaskari nane Morogoro wamekamatwa kuhusiana na kuuwawa kwa Ally Zona. Hatujasikia majibu ya hiyo TUME zaidi ya kumsikia Nchimbi kabla hata ya kamati zake na taarifa ya awali ya madaktari kuwa marehemu aliuwawana kwa kugongwa na kitu chenye ncha kali na kuelezwa waliofanya hivyo ni wananchi maana askari walikuwa umbali naye mita 300. Tumeshangaa leo Polisi wanakamatwa kinyemela baada ya sakata la Mwangosi. Inamaana hao Polisi waliokamatwa ni wafuasi wa CDM, maana propaganda za awali zilikuwa zinaeneza kuwa ameuwawa na wafuasi wa CDM.
Kitu kizito chenye ncha kali, kinaweza kuwa jini makata hiki.
 
Tayari katika vyombo mbalimbali vya habari, tumepata taarifa ya kufunguliwa kesi ya mauaji ya Iringa.

Vilevile inaonyesha Waziri chimbi jana ametoa waraka unaelezea tuhuma za mlalamikiwa. Sasa kama

hata Bunge letu tukufu huwa haliruhusiwi kuzungumzia suala lililo mahakamani, inakuwaje basi hii tume

ya Nchimbi, kuhusu suala hilo hilo iendelee kufanya kazi ambayo mahakama inaifanya. Ina maana Waziri

hana imani na mahakama? Je hapa huu muhimili mkuu katika ile mihimili mitatu hauingiliwi kiutendaji?

Naomba wataalamu na Thinkers mnisaidie hapa naona kama kuna tatizo.

Nawakilisha.

Daudi-Mwangosi.jpg

Nafikiri mahakama inaweza kutumia vielelezo vilivyopo na ikamliza hii kazi, hizo pesa za kamati zipelekwe mahakamani


Katiba:
107B. Katika kutekeleza mamlaka ya utoaji haki, mahakama zote zitakuwa huru na zitalazimika kuzingatia tu masharti ya
Katiba na yale ya sheria za nchi.

Na hii jee haingilii uhuru wa mahakama
attachment.php

kwan aliyekwambia Tanzania kuna Uhuru wa Mahakama nan?hapa ni UHURU WA CCM TUU...Tuchukue hatua porojo hizi hazijengi mkuu.
 
Its obvious Kamati inaingilia uhuru wa Mahakama. Lakini nadhani serikali ina hahaha kwani ukiangalia kuna vitu vinakinzana:-

1. Kwanza Mwanzo taarifa ya kwanza ya polisi ilisema Mwongosi amepigwa na kitu cha ncha kali kutoka upande waliokuwa wananchi au wafuasi wa chadema
2. Picha zilipotoka kuonyesha hali halisi ya tukio hii story ikapotezewa na wakakurupukua kuunda Kamati
3. Kamati imeundwa lakini imepingwa vikali kutokana na composition yake wakaamua wapeleke Mahakamani

Maswali ya kujiiuliza yote hayo matatu yanafanywa na serikali hiyo hiyo na ni dhahiri yanaoshesha hali ya kutokuwa na maamuzi dhabiti kama si kupagawa na kuwa katika "state of fear". Kwa mtizamo wangu Kamati kwa vile imeundwa na serikali ilipaswa kumaliza kazi yake na ndipo hatua za kisheria zifuatwe kama ingependekezwa hivyo. Hili lilifanyika wakati wa Zombe pia. Lakini Kamati na Mahakama haviwezi kufanya kazi kwa pamoja hata kidogo. Kisheria Kamati sasa haina kazi tena maana mambo yapo mahakamani na Kamati haina tena Mamlaka ya kufanya shughuli hiyo....

Askari Pacificus ameonewa (katolewa kafara). "Wamefunika kombe ili mwanaharamu apite"
 
Ndio matunda ya bora utawala, sikuizi watu wanakwenda na dhana ya uongozi bora, bado Tanzania tu.
 
Back
Top Bottom