BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,011
Kamati ya Mwinyi yaonywa Dodoma Monday, 02 November 2009 07:47 *Yatakiwa isilenge kuziba midomo wabunge
*Wabunge waapa hatutaburuzwa na serikali
Na John Daniel, Dodoma
Majira
BAADHI ya wabunge wameonya kuwa iwapo Kamati ya Mwinyi inayokutana nao leo itakuja na sura ya kutaka waburuzwe na serikali Rais Jakaya Kikwete ajiandae CCM kupasukia mkononi mwake.
Wabunge hao wametoa onyo hilo kamati hiyo ikiwa tayari imekutana na Kamati ya Uongozi ya Wabunge wa CCM chini ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na badaye kukutana tena na Kamati ya Uongozi ya Bunge chini ya Spika, Samuel Sitta kwa nyakati tofauti kwa lengo la kupata picha na kujua uelekeo wa kikao cha leo cha wabunge wote wa chama hicho.
Kamati hiyo iliundwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kwa lengo la kuchunguza mahusiano baina ya wabunge na serikali yao, hasa baada ya kauli ya za wabunge hao bungeni kuwakera viongozi wa serikali na wa chama hicho.
Wakizungumza na Majira kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya wabunge walisema lengo la kamati ni kuwaziba midomo ili kuacha hoja za msingi
zinazotakiwa kujibiwa na serikali kwa ufasaha badala yake wakubali kuburuzwa jambo,ambalo limepitwa na wakati.
"Hivi sasa tunasubiri majibu ya serikali kuhusu Richmond, huku TAKUKURU inataka kutuziba midomo, huku Kamati ya Mhe. Mzee Mwinyi nayo inataka kutuziba midomo, haya mambo tusipoyaangalia kwa makini wakati wa CCM kugawanyika mkono mwa JK umefika, kwanza kuwepo kwa kamati hii ni kuficha ukweli, chanzo cha tatizo kinajulikana lakini hawataki kukishughulikia, wananazunguka.
"Chanzo cha tatizo ni kwamba kumejitokeza kundi dogo tu ndani ya CCM lenye nguvu ya fedha haramu, lenye lengo la kukibinafsisha au kukiendesha chama kama kampuni ya mtu binafsi, inapotokea wenye uchungu na nchi kuona hilo na kulipinga kwa nguvu zote matokeo yake ni kuundwa kwa kamati badala ya kushughulikia chanzo cha
tatizo," alisema mbunge mmoja.
Mbunge mwingine machachari wa CCM alisema yeye kama mwakilishi wa wananchi anasikitishwa na hali iliyopo ndani ya CCM ya sasa ya kuacha hoja za msingi na kupoteza muda kwa lengo la kuficha ukweli.
"Ninachoweza kuzungumza kwa sasa ni kwamba tunasubiri sana hiyo Kamati ya Wazee wetu kesho (leo), ila tunasikitika sana kwamba tunapoteza muda wa kulumbana badala ya kung'oa mzizi wa fitna, tatizo linajulikana, kinachotusumbua ni kutokubali kuwa wawazi na wakweli.
Hoja zinazotarajiwa kutawala mkutano ni pamoja na kuwepo kwa uhasama baina ya wabunge wa CCM, vikao vya CCM kushindwa kushughulikia matatizo ndani na kuyaweka hadharani bungeni na bunge kutumika kama rungu la kupiga serikali pamoja.
Habari kutoka ndani ya Kikao cha Kamati na ile ya Uongozi wa Bunge, zilieleza kwamba kulikuwa na mjadala mkali kuhusu hoja hizo huku baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wakiweka wazi kwamba kinachotakiwa ni kushughulikia matatizo si watu.
Ilielezwa kwamba kikao hicho kilikuwa na mvutano mkali huku baadhi ya wajumbe wakionya kamati hiyo kwamba iwapo haitasoma alama za nyakati uenda kikao cha leo kitakuwa kigumu zaidi na hata kuweza kuvunjika kwa kuwa wabunge wanatambua kuwa kilichopo nyuma ya kamati hiyo ni kutaka
kuwanyamazisha.