Kamati ya Madini ya Bunge yahongwa kupitisha Bajeti ya madini?

Maumivu nchi inayoyapata kutoka na blanda za ngeleja, kwa maslahi yake, linakula kizazi cha sasa na kijacho. Kwanini kijana huyu ngeleja aslambwe viboko? Sekta inayotegemea umeme, uzalishaji umekuwa wa ghari mno kiasi kwamba cost per unit imepanda sana kiasi kwamba nchi iko kwenye shida.

Fikiria tangu mwaka 2002mpaka sasa 2011 bado jibu la serikali kwamba inalishughulikia hili tatizo la umeme! Je sisi ni kondoo???????????
Mi jajiuliza
  1. Hakuna pesa ya kutosha ku- deal na issue hii ya umeme ili soln ipatikane?
  2. Je shirika halina planning officer yaani kujua miez flani maji yatapungua na juhudi gani zichuliwe ili kuhakikisha kila kitu kinakaa sawa?
  3. Au ni janja ya wale wanao deal na kuuza generators , na solar energy ili wauze kwa wingi ka kupata profit wahusika wa wizara wanahongwa?
  4. Mi siridhiki na wizara ya nishati inavyo operate, na kulichukulia kukatika kwa umeme ni jambo la kawaida.
  5. Binadamu gani asiye jisikia vibaya kwa mwenzake anavyo pata hasara? Vyombo vyote vinavyo tumia umeme, na vyakula vyetu, vimeharibika, kisa deal ya ngeleja awe tajiri kama Lowasa kwa gharama za watanzania?
  6. Mungu nisamehe kwasababu nina hasira.
Uzuri ni kwamba umejiuliza maswali na baadhi ya majibu tayari mwenyewe unayo. Zaidi sasa wananchi tunaweza kuelewa sasa kwamba kuna agenda yenye siri nzito sana katika mgao wa umeme. sio uhaba wa maji, sio uchakavu wa visima vya gesi, sio ku-service visima vya gesi, sio uhaba wa fedha za kuendeshea mitambo, na sio, sio, sio, sio.

Kama wizara inafikia mahali inawahonga wawakilishi wa wananchi tena bila kigugumizi cha aina yeyote basi ni wazi mambo yote yanayoongelewa kusababisha mgao wa umeme ni kutuzuga tu. Hapa kuna agenda ambayo wanaijua wakubwa kuanzia namba moja hadi kuporomoka mpaka Tanesco kwenyewe. Mikataba mibovu inasainiwa, miswada mibovu ya kuumiza wananchi inapitishwa bungeni kwa makofi na nderemo za watu wa magamba kumbe wameshapeana bahasha.

IRI NJE MMEUMBUKA!!! Haya pitisheni hiyo miswada yote jinsi itakavyoletwa mjengoni kwa kuwa ninyi ndiyo mnashika namba kubwa ya wabunge lakini siri yenu tumeing'amua kuwa mnajazwa mifukoni halafu mkifika mjengoni kila kitu saaaawaaaa.
 
Hayo ni mambo ya ubunifu wa magamba wa kujiongezea mapato baada ya CDM kutaka posho ziondolewe. Ni mambo ya ujasiriamali, si mnakumbuka BM alikuwa mjasiriamali akiwa ikulu,tehe tehe tehe...........
 
Sasa nimepata picha ni kwanini mbunge anasimama kwa mbwembwe na vijembe kwa wapinzani kisha anaunga mkono hoja by 100% bila kuchangia kitu chochote cha maana. Kumbe huwa kuna bahasha zimetembea kwahiyo pale ni maigizo tu! Unafiki mtupu. Dam it!
 
*Wasema ameshindwa kumaliza tatizo la umeme
*Wahoji JK kutafuta wawekezaji kwenye giza


Na Godfrey Ismaely

SAKATA la mgawo wa umeme unaoendelea katika maeneo mbalimbali hapa nchini limeendelea kuibua mapya huku Chama cha Wananchi (CUF) kumtaka
Waziri wa Nishati na Madini, Bw. William Ngeleja kujiuzulu kwa kushindwa kusimamia TANESCO kudhibiti mgawo huo.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Tanzania Bara, Bw. Julius Mtatiro wakati akitoa taarifa juu ya mgawo unaoendelea hapa nchini.

"CUF tunamtaka Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja ajiuzulu kwani ameshindwa kusimamia TANESCO walau katika mfumo huo huo mbovu wa serikali ya CCM, ili apewe mtu mwingine ambaye anaweza kujaribu kuiondoa Tanzania kwenye tatizo la mgawo wa umeme usiokwisha," alisema Bw. Mtatiro.

Aidha alisema kuwa kitendo cha waziri huyo cha kuendelea kung'ang'ania kuongoza wizara hiyo wakati inaonesha wazi kuwa imemshinda ni dhahiri kwamba TANESCO kuna maslahi yake na wala hafikirii kuwahudumia Watanzania.

"Kuendelea kung'ang'ania madarakani kwa Bw. Ngeleja inaonesha wazi kuwa TANESCO kuna maslahi yake ilihali wizara tayari imemshinda na ni ishara ya wazi kwamba kwa mfumo huo hawafikirii hata kidogo Watanzania bali maslahi yake binafsi," alisema Bw. Mtatiro.

Wakati huo huo CUF imetamka kuwa mgawo wa umeme hapa nchini unachangiwa na chama tawala (CCM) kwa kufikia ukomo wa kufikiria namna ya kutatua kero za wananchi, huku Rais Jakaya Kikwete akiwa anatafuana fedha za umma kwa safari za nje kwa madai anaenda kuonana na wawekezaji ili waje kuwekeza kwenye nchi isiyokuwa na umeme.

"Sababu zimekuwa zile zile za uongo wa kila namna mabwawa hayajajaa, mitambo imeharibika, mafuta yameisha, hizi kwetu ni sababu za kijinga sana kwa nchi ambayo imepata uhuru wake kwa miaka 50 iliyopita, huku ikiwa na viongozi waliosoma kila aina ya elimu pamoja na rasilimali za kutosha zilizopo hapa nchini," alisema Bw. Mtatiro.

Bw. Mtatiro alisema kuwa pamoja na hali ngumu ya upatikanaji wa umeme Rais Kikwete kupitia hotuba yake ya kufunga mwaka 2010, aliwajulisha wananchi kuwa katika kipindi cha miaka mitano 2005 hadi 2010 TANESCO kupitia msaada wa serikali iliongezewa uwezo wa kuzalisha umeme kwa Megawati (MW)145 (MW 100 Ubungo na MW 45 Tegeta) kwa kutumia gesi asilia hali inayoonesha udhaifu.

"Hali halisi Rais ameendelea kuhaidi utekelezaji wa miradi mingine kadhaa inayotoa takribani megawati 1,130 katika kipindi cha 2011 hadi 2013, jambo ambalo litakuwa maajabu ya dunia. Serikali iliyoongeza uzalishaji wa megawati 145 kwa kipindi cha miaka mitano itaweza vipi kuzalisha megawati 1,130 katika kipindi cha miaka mitatu tu? Watanzania wanadangaywa kweupe tena bila chembe ya aibu," alisema Bw. Mtatiro na kuongeza.

"Serikali ya CCM, Wizara ya Nihati na Madini na TANESCO wanaendelea kuua uchumi wa Watanzania kutokana na uzembe hasa kwa kushindwa kutafuta suluhisho la matatizo makubwa ambayo ni misingi ya ahueni ya kiuchumi mahali popote hali inayodhirisha wazi kuwa wana udhaifu mkubwa na hata mtu mwenye ubongo mzuri anapojaribu kuwasaidia watanzania kupitia CCM anafeli kabla hajaanza," alisema Bw. Mtatiro.

Aliongeza: "Watanzania wasitafute mchawi wa mgawo wa umeme, mchawi wanamjua vizuri sana – Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Serikali ya CCM na Waziri wa Nishati na Madini Bw. Ngeleja."

Alisema kuwa licha ya hali ya mgawo inayoendelea kwa sasa Rais ameendelea kutumia fedha nyingi za umma kwa ajili ya kufanyia safari za nje dhumuni likiwa ni kuwatafuta wawekezaji ambao hajui wakifika hapa nchini watatumia nishati gani ili kuendeshea shughuli zao kwa kuwa mgawo umeendelea kushika kasi.

"Kwa maana nyingine kama Rais anapotafuta fedha za umma kwa safari za nje 'kiguu na njia' kwa ajili ya kuonana na wawekezaji ili kuwashawishi waje kuwekeza hapa nchini anawahadaa ama kuwadanganya kwani hadi sasa wawekezaji waliopo ukiongeza na zaidi ya asilimia 10 ya nyumba zilizounganishiwa umeme wapo katika mgawo mkubwa ambao hauna ukwamo," alisema Bw. Mtatiro.

Alisema chama hicho kinamshauri Rais Kikwete aachane na safari zake zinazomfanya kupoteza muda kwa ajili ya kwenda kuwasaka wawekezaji nje ya nchi kwa kuwa walioko kwa sasa serikali imeshindwa kuwapatia umeme wa uhakika.

"Gharama anazotumia kwenda kutafuta wawekezaji ni kiini macho tu kwa sababu duniani haijawahi kutokea wawekezaji wenye mitaji yao ya uhakika kuja kuwekeza gizani.

"Gharama anazotumia kwenda kutafuta wawekezaji ni kiini macho kwa sababu duniani kote hajawahi kutokea mwekezaji au wawekezaji wenye mitaji yao ya uhakika kwa ajili ya kwenda au kuja kuwekeza gizani," alisema Bw. Mtatiro na kuhitimisha:

"Kwa kifupi mgao wa umeme usiokwisha ni sawasawa na shetani litialo umasikini kwa jamii ya watu ambao tayari ni masikini. Na kwa hakika, Serikali ya Tanzania imebadilisha umeme kutoka kuwa tatizo linalotatuliwa hadi kuwa janga la taifa.

Juhudi za gazeti hili kumtafuta Waziri Ngeleja kupata maoni yake zilishindikana jana baada ya simu yake kutopatikana.
 
Why it is not possible to change the tittle? If u make a mistake, the mistake stays? Or we need to check with the admin's?

Help help help
 
Ni mbunge gani wa CDM ambaye yuko kwenye hii kamati aanze kwa kujiuzulu. nitajieni anaitwa nani
 
Ningependa kujua mnyika nae alichukua? Maana nimiongoni mwa wanakamati

Mwache naye achukue bwana!!

Yaani nchi yetu ina watu wa aina gani hawa wasiokuwa na huruma hata chembe!!!??

Na sisi waTZ sijui mazoba vile!! Tunachekelea tu kila tunachoambiwa na hawa wapumb***vu chama cha magamba. Tungehamasika kama Waarabu tungeenda kuwachomoa ofisini tukianzia na huyu mtalii mpuuzi huyu!!!
 
Ni mbunge gani wa CDM ambaye yuko kwenye hii kamati aanze kwa kujiuzulu. nitajieni anaitwa nani
John Mnyika,ila kwa taarifa nilizozipata Mnyika na mbunge mwingine sijamjua jina bado wao walizikataa hizo bahasha na kuripoti kwa mwenyekiti wa kamati juu ya mchezo huo mchafu
 
Mheshimiwa supika naunga Mkono HOJA KWA ASILIMIA MIAMOJA.......kumbe huwa wanahongwa
 
nchi zilizopoteza mwelekeo bwana. ngeleja unazidi kunitia aibu brother! typical of failed state leaders! akyanani hawa jamaa wana kila sababu ya kuwekwa pembeni
 
Hii ni hatari sana, kila kukicha mara unasikia wabunge wa kamati fulani wameongwa au wameomba hongo.

Sasa kama watu tuliowapa dhamana wanafanya hivi sasa kuna hope jamani? Ndo maana miswada ya kifisadi na ya kuwaumiza wananchi itapitishwa kila kukicha despite of too much noise from wananchi, this is weird! Wanatufanya sisi wapumbafu?

Kwa mtindo huu Umeme nchii utabaki history! na sasa tunaingia katika Old stone age again.
 
Jamani naombeni muwataje kwa majina na vyama watokavyo hao wabunge wajumbe wa kamati hiyo waliopokea na waliokataa hongo
 
Serikali ya CCM haiaminiki tena kwa watanzania ni serikali ya kilaghai,GEREJA inabidi ajiuzuri,mgawo wa umeme sasa hivi unakuja wa masaa 24 harafu chadema wakisema utasikia eti CHADEMA,wanawachochea wanachi waichukie serikali,kwa hali ya kawaida upuuzi unaoendelea nchini hauitaji hata uwe na elimu ya degree uujue,poleni mlioichagua CCM,.
 
Jamani msinimeze kwamba ushahidi huko wapi. Mimi ni mwandishi tena wa mwananchi. Lazima niwape Ukweli...

Hii story hapa chini, tulishtuliwa na na Mh.January Makamba Mwenyewe. Na katika utafiti wetu tumegundua kwamba, ni yeye ndiye aliyewachuuza wanasiasa (wabunge katika kamati yake) wenzake na watumishi kwenye wizara ya Nishati na Madini.

January alisuka mpango mzima na kisha kujivisha kilemba cha ukoka. Lengo kuu la JM ni kummaliza Ngeleja taratibu. Aliwadanganya wasaidizi wa Ngeleja kutoa rushwa, aadae akaja kutuambia kuhusu hilo sakata.....

January jipange vizuri unaelekea kubaya. Vita vya kisiasa unavyovianzisha siyo nzuri kwa maisha yako ya kisiasa. Unaelekea kumtoa ngeleja madarakani, lakini kumbuka siku yako inakuja

********************************************************************************************************

CHANZO Kashfa nzito Wizara ya Ngeleja

WIZARA ya Nishati na Madini imeingia katika kashfa nzito ambapo baadhi ya maofisa wa wizara hiyo wanatuhumiwa kuwahonga baadhi ya wabunge katika Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kwa kile kinachodaiwa kutaka bajeti ya wizara hiyo kupita kwa urahisi, Mwananchi limebaini.

Habari zilizopatikana kutoka Dodoma na Dar es Salaam zimedokeza kuwa taarifa za uovu huo tayari zimefikishwa mezani kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye amesema atalishughulikia baada ya kuwa amewasiliana na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.

Kwa mujibu wa habari hizo suala hilo pia tayari limefikishwa kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda na kwamba kamati ya uongozi ya bunge anayoiongoza pia imearifiwa kuhusu suala hilo. Kashfa hiyo imeikumba wizara hiyo katika kipindi kigumu ambacho nchi iko gizani huku wizara hiyo ikilaumiwa kutokana na uhaba wa nishati ya umeme kiasi cha Waziri Ngeleja kutangaza mgawo wa saa 10 wakati wa mchana na saa sita wakati wa usiku "ni janga la kitaifa".

Habari zaidi zinasema miongoni mwa mambo muhimu ambayo kamati hiyo ilikuwa ikitaka maelezo ni mapendekezo ya wizara hiyo kutaka kujenga jeno la makao yake makuu jijini Dar es Salaam kinyume cha ilani ya CCM ambayo inaweka wazi kwamba hakutakuwa na ujenzi wa makao makuu ya wizara jijini humo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Habari zilizolifikia Mwananchi zilidai kwamba, Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini ya Bunge, January Makamba ndiye aliyewasilisha malalamiko kwa Pinda na Makinda baada ya kubaini 'ulegevu' miongoni mwa wajumbe wa kamati yake wakati wa mchakato wa kujadili mapendekezo ya bajeti ya Wizara hiyo na kwamba mapema alikuwa ameishapokea taarifa kuhusu baadhi ya wajumbe wake kuhongwa.

"Mwenyekiti (January) alipewa taarifa za wajumbe wawili wa kamati yake ambao walikataa hongo hiyo, na baada ya kufanya uchunguzi alibaini kwamba kuna kila dalili kwamba baadhi ya wabunge katika kamati yake walikuwa wamebadili msimamo katika baadhi ya mambo," kilieleza chanzo chetu mjini Dodoma.Habari zaidi zilidai kuwa kufuatia hali hiyo, January aliitisha kikao cha wabunge ambao ni wajumbe wa kamati yake na kugeuka mbogo, huku akiweka bayana kuchukizwa kwake na taarifa za wajumbe wake kuhongwa na kwamba alikwenda mbali zaidi akitishia kujiuzulu nafasi ya uenyekiti ili kutoa nafasi kwa wabunge hao kuchagua mwenyekiti mwingine ambaye atakuwa tayari kuvumilia uovu huo.

"Yule kijana (January) alikasirika sana, alichukizwa kweli kweli na hali hiyo kwa sababu ni kama wajumbe waliopokea hizo bahasha walikuwa wakimzunguka kwani tayari walikuwa wanajua nini wanachopaswa kufanya ili kuziokoa sekta za nishati na madini,"kilieleza chanzo hicho.

Kadhalika suala hilo la hongo lilijadiliwa katika kikao cha pamoja baina ya wajumbe wa kamati hiyo na viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini, ambapo Waziri Ngeleja na Naibu wake, Adam Malima waliomba radhi kutokana na tukio hilo, hivyo kamati hiyo kuagiza maofisa wa wizara waliohusika wachukuliwe hatua. "Ni kama Ngeleja na Malima walimalizana na kamati, si unajua maana ni kama January alikuwa peke yake, kama kulikuwa na wanaomsapoti (wanaomuunga mkono) walikuwa ni wachache, hivyo kama waziri na naibu wake waliomba radhi hakukuwa jinsi zaidi ya kumalizana nao," zilidai taarifa hizo na kuongeza: "Hata hivyo Mwenyekiti na baadhi ya wajumbe walimwagiza Ngeleja na Malima kuwachukulia hatua maofisa waliohusika na ugawaji wa fedha hizo kwa baadhi ya wabunge".

Kauli za viongozi
Mwananchi liliwasiliana na January ili kufahamu undani wa suala hilo, lakini mbunge huyo wa Bumbuli hakukanusha wala kukubali kuhusu baadhi ya wajumbe wake kupokea rushwa. "Nani kakwambia bwana, mimi siwezi kuzungumza lolote, mambo ya kamati jamani si yote tunayoweza kuweka wazi, lakini siku hizi hatufanyi vikao bila kuwaruhusu waandishi wa habari, kama hayo yangetokea si yangeonekana wakati huo?,"alihoji January. Waziri Ngeleja kama ilivyo kwa January naye hakukubali wala kukanusha kuwepo kwa tuhuma hizo na badala yake alisisitiza kwamba anayeweza kuzizungumzia ni mwenyekiti wa kamati akimaanisha January.

"Unasikia, kama jambo limetokea kwenye kamati mimi sina mamlaka ya kulizungumzia hata kidogo maana nitakuwa navunja kanuni, kama wengine nilivyowaambia maana naona leo wengi wananitafuta kwa habari hii, mpigieni mwenyekiti wa kamati yeye ana mamlaka, mimi kwangu no comment (siwezi kusema chochote),"alisema Ngeleja kwa simu.Spika wa Bunge, Makinda kwa upande wake pia alikanusha kupokea taarifa hizo. "Mimi ndiyo nazisikia kutoka kwako, pengine kama zimeletwa kwa barua sijaiona, lakini sifahamu kitu kama hicho," alisema Makinda alipozungumza kwa simu na Mwananchi.

Kwa upande wake Naibu Spika Job Ndugai alisema kuwa hana taarifa hizo kwa kuwa yeye alikuwa nje ya nchi kikazi. "Ndugu yangu, pengine ukimpata Spika anaweza kukusaidia, mimi nimerudi jioni hii (jana jioni) ndio naingia hapa Dodoma najiandaa kwa ajili ya kesho,"alisema Ndugai.
 
Back
Top Bottom