Kamati ya Madini ya Bunge yahongwa kupitisha Bajeti ya madini?

JOHN MADIBA

JF-Expert Member
Jan 30, 2011
251
155
WIZARA ya Nishati na Madini imeingia katika kashfa nzito ambapo baadhi ya maofisa wa wizara hiyo wanatuhumiwa kuwahonga baadhi ya wabunge katika Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kwa kile kinachodaiwa kutaka bajeti ya wizara hiyo kupita kwa urahisi, Mwananchi limebaini.

Habari zilizopatikana kutoka Dodoma na Dar es Salaam zimedokeza kuwa taarifa za uovu huo tayari zimefikishwa mezani kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye amesema atalishughulikia baada ya kuwa amewasiliana na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.

Kwa mujibu wa habari hizo suala hilo pia tayari limefikishwa kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda na kwamba kamati ya uongozi ya bunge anayoiongoza pia imearifiwa kuhusu suala hilo.

Kashfa hiyo imeikumba wizara hiyo katika kipindi kigumu ambacho nchi iko gizani huku wizara hiyo ikilaumiwa kutokana na uhaba wa nishati ya umeme kiasi cha Waziri Ngeleja kutangaza mgawo wa saa 10 wakati wa mchana na saa sita wakati wa usiku "ni janga la kitaifa".

Habari zaidi zinasema miongoni mwa mambo muhimu ambayo kamati hiyo ilikuwa ikitaka maelezo ni mapendekezo ya wizara hiyo kutaka kujenga jeno la makao yake makuu jijini Dar es Salaam kinyume cha ilani ya CCM ambayo inaweka wazi kwamba hakutakuwa na ujenzi wa makao makuu ya wizara jijini humo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Habari zilizolifikia Mwananchi zilidai kwamba, Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini ya Bunge, January Makamba ndiye aliyewasilisha malalamiko kwa Pinda na Makinda baada ya kubaini 'ulegevu' miongoni mwa wajumbe wa kamati yake wakati wa mchakato wa kujadili mapendekezo ya bajeti ya Wizara hiyo na kwamba mapema alikuwa ameishapokea taarifa kuhusu baadhi ya wajumbe wake kuhongwa.

"Mwenyekiti (January) alipewa taarifa za wajumbe wawili wa kamati yake ambao walikataa hongo hiyo, na baada ya kufanya uchunguzi alibaini kwamba kuna kila dalili kwamba baadhi ya wabunge katika kamati yake walikuwa wamebadili msimamo katika baadhi ya mambo," kilieleza chanzo chetu mjini Dodoma.

Habari zaidi zilidai kuwa kufuatia hali hiyo, January aliitisha kikao cha wabunge ambao ni wajumbe wa kamati yake na kugeuka mbogo, huku akiweka bayana kuchukizwa kwake na taarifa za wajumbe wake kuhongwa na kwamba alikwenda mbali zaidi akitishia kujiuzulu nafasi ya uenyekiti ili kutoa nafasi kwa wabunge hao kuchagua mwenyekiti mwingine ambaye atakuwa tayari kuvumilia uovu huo.

"Yule kijana (January) alikasirika sana, alichukizwa kweli kweli na hali hiyo kwa sababu ni kama wajumbe waliopokea hizo bahasha walikuwa wakimzunguka kwani tayari walikuwa wanajua nini wanachopaswa kufanya ili kuziokoa sekta za nishati na madini,"kilieleza chanzo hicho.

Kadhalika suala hilo la hongo lilijadiliwa katika kikao cha pamoja baina ya wajumbe wa kamati hiyo na viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini, ambapo Waziri Ngeleja na Naibu wake, Adam Malima waliomba radhi kutokana na tukio hilo, hivyo kamati hiyo kuagiza maofisa wa wizara waliohusika wachukuliwe hatua.

"Ni kama Ngeleja na Malima walimalizana na kamati, si unajua maana ni kama January alikuwa peke yake, kama kulikuwa na wanaomsapoti (wanaomuunga mkono) walikuwa ni wachache, hivyo kama waziri na naibu wake waliomba radhi hakukuwa jinsi zaidi ya kumalizana nao," zilidai taarifa hizo na kuongeza:

"Hata hivyo Mwenyekiti na baadhi ya wajumbe walimwagiza Ngeleja na Malima kuwachukulia hatua maofisa waliohusika na ugawaji wa fedha hizo kwa baadhi ya wabunge".

Kauli za viongozi

Mwananchi liliwasiliana na January ili kufahamu undani wa suala hilo, lakini mbunge huyo wa Bumbuli hakukanusha wala kukubali kuhusu baadhi ya wajumbe wake kupokea rushwa.

"Nani kakwambia bwana, mimi siwezi kuzungumza lolote, mambo ya kamati jamani si yote tunayoweza kuweka wazi, lakini siku hizi hatufanyi vikao bila kuwaruhusu waandishi wa habari, kama hayo yangetokea si yangeonekana wakati huo?,"alihoji January.

Waziri Ngeleja kama ilivyo kwa January naye hakukubali wala kukanusha kuwepo kwa tuhuma hizo na badala yake alisisitiza kwamba anayeweza kuzizungumzia ni mwenyekiti wa kamati akimaanisha January.

"Unasikia, kama jambo limetokea kwenye kamati mimi sina mamlaka ya kulizungumzia hata kidogo maana nitakuwa navunja kanuni, kama wengine nilivyowaambia maana naona leo wengi wananitafuta kwa habari hii, mpigieni mwenyekiti wa kamati yeye ana mamlaka, mimi kwangu no comment (siwezi kusema chochote),"alisema Ngeleja kwa simu.

Spika wa Bunge, Makinda kwa upande wake pia alikanusha kupokea taarifa hizo. "Mimi ndiyo nazisikia kutoka kwako, pengine kama zimeletwa kwa barua sijaiona, lakini sifahamu kitu kama hicho," alisema Makinda alipozungumza kwa simu na Mwananchi.

Kwa upande wake Naibu Spika Job Ndugai alisema kuwa hana taarifa hizo kwa kuwa yeye alikuwa nje ya nchi kikazi. "Ndugu yangu, pengine ukimpata Spika anaweza kukusaidia, mimi nimerudi jioni hii (jana jioni) ndio naingia hapa Dodoma najiandaa kwa ajili ya kesho,"alisema Ndugai.
 
Ngeleja anaomba msamaha na kuonkana kama amemalizana na kamati!!hao maofisa wa wizara wamezitowa wapi hizo hela kama sio wizarani? Je, waziri hausiki kwa hili? Maana bila yeye waziri kuwaagiza maofisa wasinge gawa hongo, kuna jambo limejificha.

Na huyu makinda mbona mara nyingi maswali ya kushtukiza huwa anakwepa? Then baada ya kukutana na wanamagamba anakuja na majibu yake. izWara inatia aibu kwanini hizopesa za hongo wasingenunulia majenereta wakapelea Kigoma, Rukwa na Ruvuma ili wananchi wapate umeme?
 
Mimi siamini kama mbunge wa Tanzania - Mwakilishi wa wananchi zaidi ya 5,000 ambaye kazi yake ni kuwasemea dukuduku zao na na kuwatetea mbele ya serikali, huyu naye achukue bahasha? - Wakuu tuwe serious na hili jambo hili tunapolijadili ni zito sana.

Kama kweli ikithibitika kuwa ni kweli basi nchi hii imekwisha - imeoza kwa rushwa na tusitegee maendeleo yoyote bila kubadili uongozi wa nchi hii kwa haraka sana.

Hii ni hatari kwa usalama wa taifa letu.

MWAKILISHI WA WANANCHI ANAPOKUWA NA TAMAA YA PESA A.K.A POSHO - HUYU HAFAI KUWA KIONGOZI.
 
Kuna watu wanatafuta umaarufu kupitia hii wizara, ata the same hii wizara imefanywa mtaji wa kisiasa kila mwenye kuweza anafanya anavyotaka. Am tired with blah blah za hii nchi. Tuamkeni jamani!!
 
Makubwa haya.

yaani mpaka wawakilishi wa wananchi wanahongwa.

PCCB huko Tanzania / Tanganyka fanyeni kazi Yenu
 
Mimi siamini kama mbunge wa Tanzania - Mwakilishi wa wananchi zaidi ya 5,000 ambaye kazi yake ni kuwasemea dukuduku zao na na kuwatetea mbele ya serikali, huyu naye achukue bahasha? - Wakuu tuwe serious na hili jambo hili tunapolijadili ni zito sana.

Kama kweli ikithibitika kuwa ni kweli basi nchi hii imekwisha - imeoza kwa rushwa na tusitegee maendeleo yoyote bila kubadili uongozi wa nchi hii kwa haraka sana.

Hii ni hatari kwa usalama wa taifa letu.

MWAKILISHI WA WANANCHI ANAPOKUWA NA TAMAA YA PESA A.K.A POSHO - HUYU HAFAI KUWA KIONGOZI.

Atafanyaje wakati akitoka tu nje ya viwanja vya bunge wananchi wanamzunguka wanataka awatatulie matatizo yao. ni bora aongeze kipato kupitia rushwa zinazojileta kama hizo. Pinda si kahalalisha uombaomba wa watanzania....
 
WIZARA ya Nishati na Madini imeingia katika kashfa nzito ambapo baadhi ya maofisa wa wizara hiyo wanatuhumiwa kuwahonga baadhi ya wabunge katika Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kwa kile kinachodaiwa kutaka bajeti ya wizara hiyo kupita kwa urahisi, Mwananchi limebaini.

Kwa jinsi wabunge wetu wanavyopenda pesa, inawezekana kabisa hii habari ikawa ya kweli!
 
MAOFISA WA JUU WATUHUMIWA KUIHONGA KAMATI YA MAKAMBAMwandishi Wetu
WIZARA ya Nishati na Madini imeingia katika kashfa nzito ambapo baadhi ya maofisa wa wizara hiyo wanatuhumiwa kuwahonga baadhi ya wabunge katika Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kwa kile kinachodaiwa kutaka bajeti ya wizara hiyo kupita kwa urahisi, Mwananchi limebaini.
Habari zilizopatikana kutoka Dodoma na Dar es Salaam zimedokeza kuwa taarifa za uovu huo tayari zimefikishwa mezani kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye amesema atalishughulikia baada ya kuwa amewasiliana na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.
Kwa mujibu wa habari hizo suala hilo pia tayari limefikishwa kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda na kwamba kamati ya uongozi ya bunge anayoiongoza pia imearifiwa kuhusu suala hilo.
Kashfa hiyo imeikumba wizara hiyo katika kipindi kigumu ambacho nchi iko gizani huku wizara hiyo ikilaumiwa kutokana na uhaba wa nishati ya umeme kiasi cha Waziri Ngeleja kutangaza mgawo wa saa 10 wakati wa mchana na saa sita wakati wa usiku "ni janga la kitaifa".
Habari zaidi zinasema miongoni mwa mambo muhimu ambayo kamati hiyo ilikuwa ikitaka maelezo ni mapendekezo ya wizara hiyo kutaka kujenga jeno la makao yake makuu jijini Dar es Salaam kinyume cha ilani ya CCM ambayo inaweka wazi kwamba hakutakuwa na ujenzi wa makao makuu ya wizara jijini humo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Habari zilizolifikia Mwananchi zilidai kwamba, Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini ya Bunge, January Makamba ndiye aliyewasilisha malalamiko kwa Pinda na Makinda baada ya kubaini 'ulegevu' miongoni mwa wajumbe wa kamati yake wakati wa mchakato wa kujadili mapendekezo ya bajeti ya Wizara hiyo na kwamba mapema alikuwa ameishapokea taarifa kuhusu baadhi ya wajumbe wake kuhongwa.
"Mwenyekiti (January) alipewa taarifa za wajumbe wawili wa kamati yake ambao walikataa hongo hiyo, na baada ya kufanya uchunguzi alibaini kwamba kuna kila dalili kwamba baadhi ya wabunge katika kamati yake walikuwa wamebadili msimamo katika baadhi ya mambo," kilieleza chanzo chetu mjini Dodoma.
Habari zaidi zilidai kuwa kufuatia hali hiyo, January aliitisha kikao cha wabunge ambao ni wajumbe wa kamati yake na kugeuka mbogo, huku akiweka bayana kuchukizwa kwake na taarifa za wajumbe wake kuhongwa na kwamba alikwenda mbali zaidi akitishia kujiuzulu nafasi ya uenyekiti ili kutoa nafasi kwa wabunge hao kuchagua mwenyekiti mwingine ambaye atakuwa tayari kuvumilia uovu huo.
"Yule kijana (January) alikasirika sana, alichukizwa kweli kweli na hali hiyo kwa sababu ni kama wajumbe waliopokea hizo bahasha walikuwa wakimzunguka kwani tayari walikuwa wanajua nini wanachopaswa kufanya ili kuziokoa sekta za nishati na madini,"kilieleza chanzo hicho.
Kadhalika suala hilo la hongo lilijadiliwa katika kikao cha pamoja baina ya wajumbe wa kamati hiyo na viongozi wa Wizara ya Nishati na Madini, ambapo Waziri Ngeleja na Naibu wake, Adam Malima waliomba radhi kutokana na tukio hilo, hivyo kamati hiyo kuagiza maofisa wa wizara waliohusika wachukuliwe hatua.
"Ni kama Ngeleja na Malima walimalizana na kamati, si unajua maana ni kama January alikuwa peke yake, kama kulikuwa na wanaomsapoti (wanaomuunga mkono) walikuwa ni wachache, hivyo kama waziri na naibu wake waliomba radhi hakukuwa jinsi zaidi ya kumalizana nao," zilidai taarifa hizo na kuongeza:
"Hata hivyo Mwenyekiti na baadhi ya wajumbe walimwagiza Ngeleja na Malima kuwachukulia hatua maofisa waliohusika na ugawaji wa fedha hizo kwa baadhi ya wabunge".
Kauli za viongozi
Mwananchi liliwasiliana na January ili kufahamu undani wa suala hilo, lakini mbunge huyo wa Bumbuli hakukanusha wala kukubali kuhusu baadhi ya wajumbe wake kupokea rushwa.
"Nani kakwambia bwana, mimi siwezi kuzungumza lolote, mambo ya kamati jamani si yote tunayoweza kuweka wazi, lakini siku hizi hatufanyi vikao bila kuwaruhusu waandishi wa habari, kama hayo yangetokea si yangeonekana wakati huo?,"alihoji January.
Waziri Ngeleja kama ilivyo kwa January naye hakukubali wala kukanusha kuwepo kwa tuhuma hizo na badala yake alisisitiza kwamba anayeweza kuzizungumzia ni mwenyekiti wa kamati akimaanisha January.
"Unasikia, kama jambo limetokea kwenye kamati mimi sina mamlaka ya kulizungumzia hata kidogo maana nitakuwa navunja kanuni, kama wengine nilivyowaambia maana naona leo wengi wananitafuta kwa habari hii, mpigieni mwenyekiti wa kamati yeye ana mamlaka, mimi kwangu no comment (siwezi kusema chochote),"alisema Ngeleja kwa simu.
Spika wa Bunge, Makinda kwa upande wake pia alikanusha kupokea taarifa hizo. "Mimi ndiyo nazisikia kutoka kwako, pengine kama zimeletwa kwa barua sijaiona, lakini sifahamu kitu kama hicho," alisema Makinda alipozungumza kwa simu na Mwananchi.
Kwa upande wake Naibu Spika Job Ndugai alisema kuwa hana taarifa hizo kwa kuwa yeye alikuwa nje ya nchi kikazi. "Ndugu yangu, pengine ukimpata Spika anaweza kukusaidia, mimi nimerudi jioni hii (jana jioni) ndio naingia hapa Dodoma najiandaa kwa ajili ya kesho,"alisema Ndugai.

Source Mwananchi new paper, 04th July 2011
 
Maumivu nchi inayoyapata kutoka na blanda za ngeleja, kwa maslahi yake, linakula kizazi cha sasa na kijacho. Kwanini kijana huyu ngeleja aslambwe viboko? Sekta inayotegemea umeme, uzalishaji umekuwa wa ghari mno kiasi kwamba cost per unit imepanda sana kiasi kwamba nchi iko kwenye shida.

Fikiria tangu mwaka 2002mpaka sasa 2011 bado jibu la serikali kwamba inalishughulikia hili tatizo la umeme! Je sisi ni kondoo???????????
Mi jajiuliza
  1. Hakuna pesa ya kutosha ku- deal na issue hii ya umeme ili soln ipatikane?
  2. Je shirika halina planning officer yaani kujua miez flani maji yatapungua na juhudi gani zichuliwe ili kuhakikisha kila kitu kinakaa sawa?
  3. Au ni janja ya wale wanao deal na kuuza generators , na solar energy ili wauze kwa wingi ka kupata profit wahusika wa wizara wanahongwa?
  4. Mi siridhiki na wizara ya nishati inavyo operate, na kulichukulia kukatika kwa umeme ni jambo la kawaida.
  5. Binadamu gani asiye jisikia vibaya kwa mwenzake anavyo pata hasara? Vyombo vyote vinavyo tumia umeme, na vyakula vyetu, vimeharibika, kisa deal ya ngeleja awe tajiri kama Lowasa kwa gharama za watanzania?
  6. Mungu nisamehe kwasababu nina hasira.
 
wasisumbue wananchi, wanataka kuzuia ufisisadi na uozo wao usionekane. katika hilo ndio wamezidi kuonyesha ni mafisadi na amna
kipya wanachofanya kuondoa janga na hadha ya umeme kwa watanzania.Na wameonyesha jinsi gani wanavyozivuruga pesa za
walipa kodi bila ya huruma kwa ajili ya maslahi yao binafsi, kwa kwa kutaka kuwapa matumaini watanzania kwa bajeti yao ya
udanganyifu. Na kuomba samahani kwa hilo ni waziri mwenye dhamana kujiuzuru pamoja na watendaji wake wote.
 
Kumbe hoja ya zito ina mashiko: "Baraza la mawaziri lilivamiwa na ma-lobysts."

Sishangai kwa kamati zinazoundwa na majambazi wengi wa magamba!!!
Nchi yetu imekwishauzwa zamaniii!!!!!!!
 
Mimi siamini kama mbunge wa Tanzania - Mwakilishi wa wananchi zaidi ya 5,000 ambaye kazi yake ni kuwasemea dukuduku zao na na kuwatetea mbele ya serikali, huyu naye achukue bahasha? ....
Pole sana ndugu fuso; unaishi nchi gani wewe?
Ebu jaribu kufuatilia ni wakati gani wabunge wa ccm huitwa kwenye vikao vya kamati ya wabunge wa ccm; then read between the lines!!
 
Back
Top Bottom