Kamati ya kudumu ya bunge ya jamii msiwe kama mponda madactari muwe makini na mazungumuzo

Ndokeji

JF-Expert Member
Jun 9, 2011
698
475
BUNGE limeiagiza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii izungumze na Serikali na madaktari ili kumaliza mgomo wa madaktari.

Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, ameitaka kamati hiyo hiyo ifanye kazi hiyo haraka na itoe taarifa kuhusu yaliyojiri kwenye mazungumzo hayo na ushauri wa Bunge kwa pande husika.

Ndugai amesema, ushauri wa Bunge kwa pande hizo si lazima yawe maagizo, na kwamba, wabunge wanaruhusiwa kuhudhuria vikao vya kamati na pande husika, na kuchangia.

Leo mchana kabla ya kuahirisha kikao cha Bunge, Ndugai aliwaeleza wabunge kuwa, baada ya kamati ya Bunge kuwasilisha taarifa kuhusu mazungumzo na pande husika, Mbunge yeyote ambaye atahitaji mjadala ataruhusiwa kuwasilisha hoja mahsusi.

Kiongozi huyo wa Bunge ameiomba Serikali na madaktari watoe ushirikiano kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii.

Ametoa uamuzi wa kupeleka suala hilo kwenye kamati hiyo muda mfupi baada ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda kuwasilisha bungeni kauli ya Serikali kuhusu namna Serikali ilivyoshughulikia mgomo wa madaktari.

Ameitaka kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti, Magreth Sitta na Makamu Mwenyekiti wake, Dk. Faustine Ndugulile, ikutane na pande zote bila ubaguzi ikiwa ni pamoja na Chama cha Madaktari, Jumuiya ya Madaktari, na madaktari bingwa.

Wakati anawasilisha kauli ya Serikali, Dk. Mponda aliwaeleza wabunge kuwa, Serikali imedhamiria kwa dhati kutatua tatizo hilo hivyo madaktari, wataalam wengine wa sekta ya afya na wadau wote wa sekta hiyo watumie fursa hiyo.

Januari 30 mwaka huu, Serikali iliunda kamati ya kushughulikia maazimio yaliyowasilishwa kwa Waziri Mkuu ili kuyachambua na kutoa maoni na mapendekezo yatakayoisaidia Serikali kumaliza mgogoro wa watumishi wa sekta ya afya.

“Narejea kusema kuwa, ni matumaini yangu kuwa pande zote mbili katika mgogoro huu zitafikia muafaka na kuumaliza mgogoro huu kwa manufaa ya umma wa Watanzania” amesema Dk. Mponda.
 
Back
Top Bottom