Kamati ya Cheyo yawatimua viongozi wa Lindi

Lilombe

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
242
39
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), John Cheyo amekataa kusikiliza maelezo yoyote ya utetezi na kuwatimua viongozi wa Mkoa wa Lindi, baada ya kubaini ufisadi wa mamilioni ya fedha ndani ya Mkoa huo.
Viongozi hao wa Mkoa wa Lindi walifika jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuhojiwa na kamati hiyo kuhusu mahesabu yao ya mwaka 2010/2011, lakini baada ya Cheyo kubaini uozo huo alikataa kuwapa nafasi ya hata ya kujitambulisha wala kuzungumza chochote.
"Ndugu wajumbe hawa viongozi hakuna haja ya wao kujitambulisha badala yake tuanze moja kwa moja kuangalia hoja iliyoletwa mbele yetu," Cheyo alisikika akiwaambia wajumbe wa kamati yake.
Baada ya kumaliza kutoa kauli hiyo ndipo alipoanza kuchambua kurasa mbalimbali za taarifa hiyo ya mahesabu ambapo kila alipopekua alizidi kushikwa na hasira jambo lililomfanya asitishe zoezi hilo na kuwataka viongozi watoke nje na kuondoka kurudi kwao Lindi.
Cheyo muda mfupi baada ya kuanza kupitia kwa haraka haraka taarifa hiyo, alibaini kuna fedha nyingi zimetumika bila ya maelezo yoyote ya kina na kwamba kamati yake haiwezi kupoteza muda kwa ajili ya kujadili madudu kama hayo.
Alitoa mfano kuwa kuna malipo ambayo yalifanywa kabla ya kupata taarifa ya malipo (Invoice) kitu ambacho ni kinyume na utaratibu wa serikali.
Kamati hiyo ilipomuuliza Katibu Tawala wa Mkoa huo, Thomas Soum, kuwa ameshika wadhifa huo kwa gani, aliwajibu kuwa ni mwaka mwaka mmoja na kabla yake yeye alikuwepo, Claudia Bitegenye ambaye kwa sasa amehamishiwa Mkoa wa Manyara.
Baada ya maelezo hayo, Cheyo aliahidi kumwandikia barua Mlipaji MKuu wa Serikali ili amuondolee, Bitegenye wadhifa wa kuwa Ofisa Masuhuli huko aliko pamoja na kumwuandikia Waziri anayehusika wa Makatibu Tawala ili amkate mshahara wake kwa asilimia 15.
Aidha, Cheyo aliahidi kuwaita tena viongozi hao mkoani Dodoma ili watoe maelezo ya kina wakiwa na aliyekuwa Katibu Tawala wao Bitegenye kwa kuwa yeye ndiye atakuwa na majibu.
Alimwagiza Soum kuwa mkali na kuhakikisha anasimamia masuala yote ya fedha ikiwemo manunuzi ya vitu mbalimbali ili mwaka wa fedha ujao wawe na hati safi.
Kamati ilibaini zaidi ya Sh. milioni 200 katika Mkoa huo wa Lindi zimepotea kupitia malipo mbalimbali ambayo hayakuzingatia taratibu na Sheria za serikali.
Kutokana na kuwekwa kiti moto’ na kutolewa jasho, viongozi hao wa Mkoa wa Lindi walijikuta wakiondoka bila hata kunywa chai licha ya kamati hiyo kuwakaribisha.
Source: Gazeti la Nipashe, Mei 28, 2011

Mheshimiwa Cheyo na Kamati yake BIG UP!






 
Okay wamegundua kuna wizi so what next?...kwanini asingekabidhi hiyo ripoti kwa TAKUKURU??..hii nchi ni kulkula tu, hata mchwa wana nafuu!!
 
Kwa vile hawa wametafuna pesa ya umma wanastahili nao wafikishwe mahakamani maana kukatwa mshahara haitoshi,Cheyo njoo na Sikonge,Tabora viongozi wanatumbua tu
 
Okay wamegundua kuna wizi so what next?...kwanini asingekabidhi hiyo ripoti kwa TAKUKURU??..hii nchi ni kulkula tu, hata mchwa wana nafuu!!

TAKUKURU? Are you serious? Wataalamu wa KUSHINDWA kesi? Bora hata kuchukua administrative actions against the suspects kama alivopendekeza Cheyo!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom