Kamati ya Cheyo yatumika kuwakingia kifua akina Mkapa na Yona.

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Jana mwenyekiti wa hesabu za serikali, kwa niaba ya kamati yake alinukuliwa na tbc akiitaka serikali kuchukua hatua za haraka kukabidhi mgodi wa kiwira kwa NSSF kama hatua ya kulipatia ufumbuzi tatizo la uhaba wa umeme hapa nchini. Wadadisi wa mambo wanaiona kauli hiyo kuwa haikustahili kutolewa na Cheyo kama mwenyekiti wa hesabu za serikali, kwani huko ni kuingilia kazi za kamati ya bunge ya nishati na madini; suala linaihusu kamati hiyo ni la fedha zipatazo shs.15 bilioni ambazo serikali ilikopesha mgodi huo na ambazo inaaminika zilitumiwa kwa matumizi binafsi na wamiliki wa KCPL. Inavyoelekea Cheyo angelitaka mgodi huo ukabidhiwe kimya kimya ili ukweli wa deni hilo husijulikane
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom