Kamati ya Bunge yamweka kitimoto Anne Kilango; Ni kuhusiana na tuhuma za Rushwa

MKUU ALIZOPEWA SI ZA FUNGATE, bali za kugombea UKIKWETE (uraisi) mwaka 2015. Wakati zinapelekwa dodoma "inasemekana majambazi wa mabwepande wakatumwa na mtandao kuzipora"

Huyo mama si inasemekana hata pesa za fungate lake yeye na baba yake le mutuz walipewa na fisadi wa EPA? Anaitwa nani kumbe yule jamaa aliye tajwa na Sofia mnyama pale bungeni?
 
*Ahojiwa na Kamati ya Bunge kwa saa mbili
*Ni kuhusiana na tuhuma za rushwa

Mtanzania | JUMAPILI, AGOSTI 12, 2012 | NA MWANDISHI WETU

HATIMAYE Mbunge wa Same Mashariki (CCM) na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Anne Kilango, juzi amehojiwa karibu saa mbili kutokana na tuhuma mbalimbali za rushwa zinazomkabili.

Habari za kuaminika ambazo MTANZANIA Jumapili imezipata kutoka mjini Dodoma, zinasema Kilango aliitwa mbele ya Kamati Ndogo ya Bunge, iliyoundwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda kuchunguza tuhuma za rushwa zinazowakabili wabunge mbalimbali.

Kamati hiyo, ambayo inaongozwa na Mwenyekiti Brigedia Jenerali mstaafu, Hassan Ngwilizi, ilimhoji Kilango kuhusiana na madai ya kupokea rushwa katika mradi wa ujenzi wa gati namba 12 katika Bandari ya Dar es Salaam.

“Kama unavyosema ni kweli, juzi ameitwa mbele ya kamati kuja kutoa maelezo yake, kwa sababu amekuwa akihusishwa na tuhuma hizi kwa muda sasa… kama unavyojua yeye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu.

“Tuliona ni mtu muhimu mno kwetu, kwa kweli alitupatia ushirikiano mzuri kwa kile anachokijua… sasa mambo mengi siwezi kuyasema ndugu yangu,” kilisema chanzo chetu.

“Moja ya masuala makubwa tulilomhoji ni kuhusiana na tuhuma za rushwa katika ujenzi wa geti namba 12 katika bandari ya Dar es Salaam, pia tulimhoji juu ya yeye kutajwa kupokea rushwa na kumtetea aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), William Mhando.

“Kama utakumbuka Kilango ni mmoja wa wabunge ambao wanadaiwa kumtetea kwa nguvu zote Muhando, wakati anasimamishwa pale TANESCO… tumepata maelezo yake, lakini nakushauri ndugu yangu uwe na subira wakati huu ambao kamati inaendelea na kazi yake,” kilisema chanzo chetu.

Habari zinasema, pia Kilango anadaiwa kuwa mstari wa mbele kumtetea Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakimu Maswi, kuwa hakupokea rushwa kutoka kwa moja ya makampuni makubwa ya kuagiza mafuta kutoka nje ya nchi (majina tunayo).

Kamati hiyo, inaundwa na Mwenyekiti Brigedia Jenerali Hassan Ngwilizi, ambaye pia ni Mbunge wa Mlalo (CCM), wajumbe wengine ni Kapteni John Chiligati (Manyoni Mashariki-CCM), Riziki Omar Juma (Viti Maalum-CUF), Said Arfi (Mpanda Mjini-Chadema) na Gosbert Blandes (Karagwe-CCM).

Kesha shindwa kwenye UWT maana yeye ni kundi la Sitta kwisha habari yake hakuna cha rushwa wala nini
 
Kilango alikuwa mpiga kelele sana mpaka akapata tuzo ya USA ya Mwanamke JASIRI. Leo Anna Kilango siye yule wa mwanzo amekuwa hana msimamo na mtetezi wa wezi. Hatujui kama kavuta mshiko lakini tunapata picha kuwa YAWEZEKANA:

Huyu Anna Kilango huwa nashindwa kumuweka kundi gani? ila baada ya naibu spika kusema baadhi ya wabunge huwa wanatumia mambo fulani, basi moja kwa moja nilimuweka katika kundi hilo
 
Siasa chafu tu hapa , hamna kingine , inakuwaje mwandishi anasema mama kilango alikuwa mbele kumtetea Mhando and then Maswi at the same time ,tuache wafu wazikane na siasa chafu zao ili 2015 iwe kazi ya kusukuma mlevi tu
 
Bahati mbaya mamaangu Anne hana watu humu maana tukianza action zetu za utotoni nani atasimama. Mbinu za UWT hizi maana imekuwa issue ili aonekana hafai. Basi kati ya waovu hutu aweza kutibu na kubadilika na kuwa mwema.

umeamua kuingia ulingon kumtetea?????
 
[
IMG_0122.jpg


DHAIFU alishasema hakuna ushahidi wa kutosha kuhusu ufisadi wa RADA huyo jamaa yupo mahakan kwa kosa la RADA
 
Siasa chafu tu hapa , hamna kingine , inakuwaje mwandishi anasema mama kilango alikuwa mbele kumtetea Mhando and then Maswi at the same time ,tuache wafu wazikane na siasa chafu zao ili 2015 iwe kazi ya kusukuma mlevi tu

isije ikwa ni wewe ndo umeandika stori ya mrs chella,maana jina la gazeti na id yako kuna kaufanano fulani hivi
 
Bahati mbaya mamaangu Anne hana watu humu maana tukianza action zetu za utotoni nani atasimama. Mbinu za UWT hizi maana imekuwa issue ili aonekana hafai. Basi kati ya waovu hutu aweza kutibu na kubadilika na kuwa mwema.

Siasa za UWT zinawezakuwepo, lakini ukweli ni kuwa kelele za Anne Kilango ni danganya toto. Huyu ni mpokeaji na mgawaji rushwa wa uhakika. Hata kwenye uchaguzi wa ubunge wa EAC alifanya hivyo. Kufoka kwake kote ni kuficha uchafu wake. Hata hivyo wapo CCM ambao sio tu hawapokei au kutowa rushwa bali pia wanachukia rushwa. Ninaamini wapo kama hao vyama vingine na hata huko wala rushwa pia wapo. Hivyo tusijumuishe watu kwenye maovu kutokana na itikadi za vyama, dini au rangi. Wapinga rushwa vyama vyote hoyee, na waendelezaji rushwa ziiiii. Mwisho mwa kabila la Warushwa unaenda mwisho. Mungu ibariki Tanzania
 
Wangezungumzia uchimbaji wa madini jimboni kwake labda hasa uharibifu unaofanyika mlima shengena ingeleta msisitizo.
 
Back
Top Bottom