Kamati ya bunge ya Nishati na Madini; January Makamba atakwepaje uwajibikaji?

Mkuu Ringo endelea kupiga round huwa awajibu na wakijibu ni shutuma au kauli nyepesi nyepesi......Wacha wajipimie mwenye size ya kamba.

Mpaka sasa ndivyo wanafanya kwa kuwa kulikuwa hakuna uwanja wa kuwakaba koo sasa upo. Watajibu tu au wawe mabubu yasiyo na madaraka milele
 
Nimekuwa nikifuatilia hili kasheshe la mlungula unayoihusu kamati ya nishati na madini, lakini kitu kinachonishangaza mwenyekiti wake, January Makamba, ajaguswa kabisa. Ni dhahiri ya kuwa kama yale yanayosemwa ni ya kweli, basi Mwenyekiti naye ni guilt kwani vitu vyote vilitokea chini ya uongozi wake
Kinachonishangaza ni kwa nini huyu mtu aguswi kabisa na vyombo vya habari? Na jee media wamepewa nini au wanaexpect nini toka kwa huyu mheshimiwa.

Itakuwa vyema kama wananchi tutaambiwa in detail ni role gani mwenyekiti aliplay katika hili sakata.

Ndugu Rufiji, ukishangaa ya Musa utakapoona ya Firauni utazimia. Unaajua jinsi gani viongozi wa serikali na wanasiasa hapa Tanzania walivyo uozo. Mambo yanafunikwa uovu unabatizwa kuwa wema na wema unabatizwa kuwa uovu. Kwa mtazamo wa serikali yetu ya sasa Makamba kafanya an exellent job. Nasema hivi kwa sababu kama TAKUKURU, na Usalama wa Taifa wanafanya kazi ya kuondoa uovu ndani ya jamii, Makamba asingeteuliwa kuwa waziri.
 
Wana Jamvi

Ninasikitika sana na madudu ya TANESCO; kwa kweli Wabunge waliomuunga Mkono Waziri wa Nishati na Madini nawapa pongezi. Wabunge hawa walitoka kwenye vyama vyote; na walisimamia maslahi ya Tanzania.

Aidha; wale waliokula fedha za wauza mafuta na kupinga hatua za Waziri wa Nishati na Madini ni wa vyama vyote. Ikumbukwe kwamba ni Waziri wa Serikali ya JK ndio aliotekeleza wajibu wa kufichua haya kwa ToRs alizopewa na Bosi wake.

Haya ni madudu ya muda mrefu; tangu zama za Mheshimiwa William Maganga Ngeleja (Mb) akiwa Waziri wa Nishati na Madini na Mheshimiwa January Yussuf Makamba (Mb) akiwa Mwenyekiti wa Kamati. Aidha Mhe Adam Kighoma Malima (Mb) akiwa Naibu Waziri wa Ngeleja wakati huo na Bwana Davidi Kitundu Jayro akiwa Katibu Mkuu wa Hio Wizara. Hawa naamini wanapaswa kuwapatia watanzania maelezo ya kina. Aidha, ikumbukwe kwamba Mheshimiwa Amos Gabriel Makala (Mb) alikuwa Mjumbe wa kamati ya Nishati na Madini kabla ya kupewa dhamana na Mheshimiwa Rais.

Waheshimiwa Wabunge ambao ni wajumbe Wa Kamati hio ni kama ifuatavyo:-


  1. Selemani Jummanne Zedi -----------------CCM
  2. Diana Mkumbo Chilolo ---------------------CCM
  3. Shaffin Ahmedali Sumar -------------------CCM
  4. Lucy Thomas Mayenga -------------------CCM
  5. Josephine Tabitha Changula ....................CCM
  6. Aeshi Khalfani Hillary .............................CCM
  7. Mwanamrisho Taratibu Maalim Abama ...... CHADEMA
  8. Profesa Kulikoyela Kanalwanda Kahigi ...... CHADEMA
  9. DAVID Ernest Sinde .............................CHADEMA
  10. Yusufu haji Hamisi ...............................CUF
  11. Suleiman Masoud Nchambis Suleiman .......CCM
  12. Catherine Violet Magige .........................CCM
  13. Kisyeri Werema Chambiri ........................CCM
  14. Munde Abdallah Tambwe .........................CCM
  15. Anthony Gervase Mbassa .........................CHADEMA
  16. Vicky Paschal Kamata ............................CCM
  17. Abia Nyabakari Muhama .........................CCM
  18. Mbaruku Salumu Ali .............................CUF
  19. Charles John Paul Mwijage ....................CCM
  20. Sara Msafiri Ali ...................................CCM
  21. Yusufu Abdala Nasir ............................CCM
  22. Dkt Festus Bulugu Limbu ..................... CCM ----------------Wanajamvi; huyu aliwahi kukumbwa na kashfa wakati wa Mkapa Wizara ya Fedha.
  23. Grace Sindati Kiwelu ...........................CHADEMA
  24. Mussa Hamis Silima ............................CCM
  25. Christopher olonyoike Ole Sendeka ........CCM
  26. Mariamu nasoro Kisangi .....................CCM

Kamati ni kubwa na inajumuisha wabunge wengi. Hivi haya madudu yote yakitokea wanakamati hawana habari???
Washazoea kwenda kula fedha za umma kwenye mashirika kwa tamaa zao; Ubunge ni kutumikia umma sio kuufisidi.

SPIKA hana nguvu za kisheria; sana sana atavunja kamati tu.

Hawa walaji wataendelea kupeta, tena wataendelea kuwa ndani ya Bunge letu tukufu. Refer to maneno aliyotoa Mheshimiwa John Momose Cheyo; alisikitishwa sana na hii hali.

SOMETHING RIGHT NEEDS TO BE DONE

Ingefaa kila mbumge aonyeshwe jinsi alivyoshiriki katika kashfa hii. Kama wapo ambao hawakushirikishwa kwa sababu yoyote ile tujue. Yawezekana siyo wote ni wachafu
 
Back
Top Bottom