Kamati ya Bunge Maalum la Katiba hatimae imependekeza kwa Rais posho ya tshs 500,000!

Bunge bhana. Siku mbili milioni. Wote tunakula ChakoNchako, tunalala Veta, tunatumia taxi za dom town, nyagi na bia za rose garden bei moja, club 84 bei moja, watoto wa Udom bei ileile nk kutwa nzima hata laki na nusu hujamaliza baada ya starehe zote hizi.
Balance laki tatu kwa siku. mara siku sitini milioni kumi na nane faida kwenye posho tu. Mungu akupe nini Tanzania?
 
Imeandikwa mwenye nacho ataongezewa na yule alienacho kidogo asipo kiangalia vyema atanyanganywa hata kidogo alichokuwa nacho watanzani amkeni ni nani aliyewaroga? Kusoma hatujui hata picha kuitambua inatushinda? Weshalewa madaraka hawa hawatujui sisi wenye njaa na hii ndio dhambi ya ubaguzi ni mbaya kuliko sumu ya panya .
Wanaokula maisha ni wanasiasa wengine wasindikizaji.
 
Imefika wakati siwachukii wanaofanya hivyo ila nawachukia sana walala hoi kama mimi wanaowaunga mkono hawa mafisadi ndiyo maana wanawapa kibri cha kufanya lolote na hawaogopi tena hata kunyimwa kura.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Hii ni njia moja ya upashanaji habari. Na unapotaka ku-mobilize watu, imedhihirika sehemu nyingine duniani mitandao ya kijamii kama facebook ina nguvu sana. Si lazima kusubiri mpaka upewe mic, maana hutapewa.
Hawa wanasiasa wetu bwana kwa kukimbilia kwenye mitandao ya kijamii...sasa kama ni msimamo wake, si asubiri kesho ndiyo aweke hiyo saini?
 
Imefika wakati siwachukii wanaofanya hivyo ila nawachukia sana walala hoi kama mimi wanaowaunga mkono hawa mafisadi ndiyo maana wanawapa kibri cha kufanya lolote na hawaogopi tena hata kunyimwa kura.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums

Upo sahihi kabisa. Walala hoi tulitakiwa tuanze kwa pamoja kwenda pale Mjengoni na kuwatoa kwa wingi wa umma. Lakini tutabaki kusaga vidole tu humu kwenye MITANDAO. POOR TANGANYIKANS, HELPLESS, IGNORANT, COWARDS, DESTITUTE, CRIPLLED, RETARDED, YOTE TU.
 
Hawa wanasiasa wetu bwana kwa kukimbilia kwenye mitandao ya kijamii...sasa kama ni msimamo wake, si asubiri kesho ndiyo aweke hiyo saini?

Bila kuja mtandaoni wengine tusingejua hii habari. Au hujui kazi mitandao mkuu?
 
mhhhh kama hii ni kweli ina maana wajumbe wale 6 walioteuliwa na Mwenyekiti wa muda wameungana so hata mzee wetu Mbowe nawe unataka uongezewe na wale memba wako wa kamati wakina Kimiti na wengineo?Jaman mmeenda kuomba muongezewe posho au kwa ajili ya katiba?nakumbuka Warioba jibu alilolitoa ni kua kama mtu hawez ajitoe au aandike barua kwa Raisi,tuachane ujinga wa kuchezea hela za watanzania mana hiyo laki tano ni hela kubwa sana hata hiyo laki 3 nayo ni kubwa sana na msituone watanzania ni wasio na uelewa labda mmoja lakini sio wote.

Mnaboa na ujinga wa kuchezea hela za nchi

UNADHANI (MAN ALONE ) MBOWE ATAWEZA kuyapinga MAFISI ?
 
posho hii ni rushwa Kwa wajumbe wa katiba ni lazma kikwete ataikubali, vinginevyo watanzania tuikatae kitu ambacho watanzania sio utamaduni wetu kwani ukisema maandamano sisi ambao kiuchumi tumepigika ndio tunaongoza kupinga Kwa kutumiwa na wenye fedha
 
Back
Top Bottom