Kamati ya Bunge Maalum la Katiba hatimae imependekeza kwa Rais posho ya tshs 500,000!

TwendeSasa

Senior Member
May 24, 2008
128
116
Posho Bunge Maalumu la Katiba kuwa 500,000 kwa siku.

Habari zilizoandikwa na gazeti la Mtanzania la Leo kwamba Kamati ya kufuatilia posho za wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba imependekeza kwa Rais posho ya tshs 500,000 kwa siku imethibitishwa ni kweli.

Natoa wito kwa Wananchi wote kushinikiza kwa Rais pendekezo hili asilikubali. Naunga mkono wazo la mjumbe wa Bunge Maalum ndg Julius S. Mtatiro la kuorodhesha majina ya wote wanaopinga nyongeza ya posho. Nitaweka sahihi kwenye petition yake hiyo mapema kesho asubuhi.

Wagombea uenyekiti nao wanaahidi kupandisha posho. Nawaonya wasithubutu kutoa ahadi hiyo kwani sio mamlaka yao. Mgombea mwenye sera ya posho hatapata kura yangu na nitashawishi wajumbe wengine wasimpe kura.


#NatakaKatibaSitakiPosho

Chanzo: Zitto Kabwe (FB Wall)

---------------------

Dodoma. Madai ya Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kutaka nyongeza ya posho ya vikao vya Bunge hilo yamegonga mwamba, Mwananchi limebaini.

Habari kutoka ndani ya kamati iliyoundwa na Mwenyekiti wa Muda wa Bunge la Katiba, Pandu Ameir Kificho ili kufuatilia madai hayo, zimedai kuwa baada ya uchunguzi wa kina, wajumbe wa kamati hiyo hawakuona sababu ya kupendekeza posho hizo kupandishwa.

Taarifa hizo zilidai kuwa wajumbe hao wamefikia uamuzi huo baada ya kupitia viwango vya posho vinavyolipwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Serikali na Mashirika ya Umma.

Pia kamati hiyo ilichambua viwango vya posho walivyolipwa wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba na viwango vya posho ya kujikimu vya Sh80, 000 kwa siku wanavyolipwa watumishi wa Serikali.

"Hili jambo linahitaji busara sana na kutazama mazingira ya nchi pia, kwa hiyo wajumbe wale baada ya kuoanisha viwango vya posho vya taasisi mbalimbali wameona Sh300,000 zinatosha," alisema mmoja wa wajumbe ambaye hakutaka jina lake kutajwa.

Mjumbe mwingine, ambaye pia hakutaka kutajwa, alisema kuwa watakaa leo kukamilisha taarifa ya utafiti wao, kabla ya kuikabidhi kwa Mwenyekiti Kificho.

Alisema pamoja na umuhimu wa kazi za mbunge, lakini isingekuwa rahisi kuongeza posho katika mazingira ya sasa, ambapo wananchi wanalia hali ngumu ya maisha.

Wajumbe hao walioteuliwa na Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalumu, Pandu Ameir Kificho ni William Lukuvi, Mohamed Abood Mohamed, Freeman Mbowe, Paul Kimiti, Jenister Mhagama na Asha Bakari.

Awali, taarifa kutoka ndani ya Bunge zilidokeza kuwa wajumbe hao walikuwa wakutane jana saa 9:00 alasiri ili kuandaa ripoti itakayopelekwa kwa Kificho ikiwa imebeba ushauri kuwa kiwango cha sasa cha posho kinatosha.

Sh300,000 wanazolipwa wajumbe wa Bunge Maalamu la Katiba zinajumuisha Sh80,000 kwa siku ambayo ni posho ya kujikimu na Sh220,000 kwa siku kama posho maalumu ya kuhudhuria kikao.

Posho maalumu ya Sh220,000 inajumuisha posho ya dereva inayopaswa iwe kati ya Sh40,000 na Sh45,000 kwa siku, usafiri wa ndani (mafuta ama teksi), mawasiliano na matumizi mengine binafsi.

Ofisi ya Bunge Maalumu
 
chukueni posho, pelekeni kwa watoto yatima, msizikae, hiyo pesa mkiikataa wengine wataila
 
mhhhh kama hii ni kweli ina maana wajumbe wale 6 walioteuliwa na Mwenyekiti wa muda wameungana so hata mzee wetu Mbowe nawe unataka uongezewe na wale memba wako wa kamati wakina Kimiti na wengineo?Jaman mmeenda kuomba muongezewe posho au kwa ajili ya katiba?nakumbuka Warioba jibu alilolitoa ni kua kama mtu hawez ajitoe au aandike barua kwa Raisi,tuachane ujinga wa kuchezea hela za watanzania mana hiyo laki tano ni hela kubwa sana hata hiyo laki 3 nayo ni kubwa sana na msituone watanzania ni wasio na uelewa labda mmoja lakini sio wote.

Mnaboa na ujinga wa kuchezea hela za nchi
 
Hivi tukikataa hawa wa Tanzania wenzetu kupewa hii posho ya 500,000 mnadhani ndo zitajengwa shule, au barabara, au dawa na vifaa hospitali? Acheni wapewe vinginevo semina, warsha na ziara za nje ambazo huwa hamjui kwa siku wanakula ngapi ndo zitaanzishwa kwa kasi. Acha jamaa zetu waonje asali na maziwa ya nchi yetu.
Nawasilisha
 
Simple arthmetic

Kwa siku 70
500,000* 70 = 35,000,000/=.
Kila mmoja ataondoka na Millioni Thelathini na Tano tu..


Ikiwa siku 90.
500,000*90 = 45,000,000/=
Millioni Arobaini na Tano tu.

NB;
Msimamo ni ule ule aisiyetaka Posho ya 300,000/= aondoke..

Tanzania tuna rasilimali watu ya kutosha...
 
Nishachoka sasa nami nitaanza kuiba vyuma vya reli, barabara na madaraja na chochote kilicho cha serikali mana dunia iko mwisho sasa kila mtu achukue anachoona kinamfaa. hakika si mbali tutakuja kuchinjana hapa tz
 
Imeandikwa mwenye nacho ataongezewa na yule alienacho kidogo asipo kiangalia vyema atanyanganywa hata kidogo alichokuwa nacho watanzani amkeni ni nani aliyewaroga? Kusoma hatujui hata picha kuitambua inatushinda? Weshalewa madaraka hawa hawatujui sisi wenye njaa na hii ndio dhambi ya ubaguzi ni mbaya kuliko sumu ya panya .
 
chuki hizo baadhi ya watu wanazozielekeza kwa zitto si afya kwa watanzania. Kapata habari katujuza eti mtu na akili zake kwanini aweke fb? Kwahiyo akae kimya? Kama hao mnaowaamini walio kaa kimya?
 
Back
Top Bottom