Kamati ya bunge Huduma za Jamii yakataa bajeti ya Wizara ya Afya

Jackbauer

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,038
2,199
Kamati imesema bajeti haijakidhi viwango. Bajeti hiyo haijazingatia makubaliano ya Abudja yanayotaka bajeti ya afya kuwa angalau 15% ya bajeti ya serikali.

Pia bajeti haijaonyesha ongezeko kwenye maslahi ya watoa huduma hasa madaktari.

Wizara imetakiwa kuongeza fedha kwa ajili ya ununuzi wa madawa.

Source: ITV
 
nina uhakika haya ni matokeo ya kupuuza madai ya watendaji(madaktari ) ambayo yaliimbwa sana katika migomo miwili iliyopita.
 
Kwanza namshukuru Mungu,

WILLIAM MGIMWA ASIJITETEE KWA UGENI WAKE KWENYE WIZARA HII,BAJETI Ya 2012/2013 ni bomu kuliko zote zilizowahi kutokea kwa miaka yote 50 iliyopita.

NAFURAHI KWA MGIMWA KUANZA KUKIONA CHA MOTO, ili apone akubaliane na Zitto ili bajeti ya upinzani itumike.
 
Kwanza namshukuru Mungu,WILLIAM MGIMWA ASIJITETEE KWA UGENI WAKE KWENYE WIZARA HII,BAJETI Ya 2012/2013 ni bomu kuliko zote zilizowahi kutokea kwa miaka yote 50 iliyopita.NAFURAHI KWA MGIMWA KUANZA KUKIONA CHA MOTO,ili apone akubaliane na Zito ili bajeti ya upinzani itumike.

bajeti za copy n paste ndio madhara yake haya.kwa nini wamesahau kuwa miezi kadhaa nyuma kulikuwa na mgomo wa madaktari ambao baadhi ya madai yake yalionekana ni magumu kutejelezeka kwa sababu ya bajeti?hii ni dharau kwa wananchi na kada ya afya.
 
nina uhakika haya ni matokeo ya kupuuza madai ya watendaji(madaktari ) ambayo yaliimbwa sana katika migomo miwili iliyopita.

mkuu hiyo ni mbinu ya kutokea pale madaktari watakapogoma. Eti bunge linashughulikia. Mark my words
 
Kamati imesema bajeti haijakidhi viwango. Bajeti hiyo haijazingatia makubaliano ya Abudja yanayotaka bajeti ya afya kuwa angalau 15% ya bajeti ya serikali.

Pia bajeti haijaonyesha ongezeko kwenye maslahi ya watoa huduma hasa madaktari.

Wizara imetakiwa kuongeza fedha kwa ajili ya ununuzi wa madawa.

Source: ITV
Usiku hawatabadili maamuzi na kuikubali?
 
mkuu hiyo ni mbinu ya kutokea pale madaktari watakapogoma. Eti bunge linashughulikia. Mark my words
mgomo unaokuja ni mkubwa na hautakoma kwa maneno ya 'tunashughulikia' au tupeni muda.muda wa miezi sita ni mwingi,kama srikali ilikuwa na nia ya dhati ya kushughulikia swala hili ingeonekana kwenye bajeti.
Eti chanjo ya homa ya ini itatolewa kwa awamu!huu ni uhuni lazima ukomeshwe.
 
Watanzania sasa wanatakiwa wajue kwamba serikali inachezea uhai wetu, na ndio maana madaktari wametishia kugoma
 
Tanzania hakuna bunge. Kama unategemea chochote toka kwa hao wagonga meza utapoteza rasilimali muda.
 
ccm imetumia milioni 200 kwenye mkutano wao wa jangwani.fedha hii inaweza kulingana na bajeti ya dawa na vifaa tiba vya hospitali ya halmashauri mbili za wilaya kwa miezi kumi.
 
Bado sijalewa mantiki ya kamati za bunge kupitia bajeti siku chache kabla ya bajeti kusomwa bungeni! Kama wanakataa bajeti leo Wizara itafanya nini kwa muda huu uliobakia ukizingatia watu wako njiani kuelekea Dodoma?
 
yawezekana wizara ya afya iliyajua madudu waliyofanya na hivyo kuchelewesha makusudi wakisubiri kuhonga.
 
mgomo unaokuja ni mkubwa na hautakoma kwa maneno ya 'tunashughulikia' au tupeni muda.muda wa miezi sita ni mwingi,kama srikali ilikuwa na nia ya dhati ya kushughulikia swala hili ingeonekana kwenye bajeti.
Eti chanjo ya homa ya ini itatolewa kwa awamu!huu ni uhuni lazima ukomeshwe.

mkuu shida nyingine ni baadhi ya madaktari ni traitors. Hili litatatuliwa vipi?
 
sasa hivi naona karibia kila wizara bajeti zao zinakataliwa na hizo kamati husika...hizi wizara zinalipua lipua tu bajeti zao huko bungeni safari hii lazima kieleweke
 
Back
Top Bottom