Kamati Kuu ya CHADEMA yakutana Igunga

Mwl Joseph Mwandu Kashindye kuipeperusha bendera ya CHADEMA Igunga.Kamati Kuu imempitisha.Kila la heri Kamanda.
Thanks Regia, mimi naamini hakuna kamati kuu ya chama chochote iliyo makini kama ya CDM hivyo hata maamuzi yao hayana walakini. Kazi ni moja sasa.
 
Mheshimiwa Regia nakubali CDM mko serious lakini jambo dogo tu huwa tunamalizwa na CCM, mimi ni mzaliwa wa igunga na nimeishi igunga muda mrefu sana kwahiyo nafuatilia kwa karibu mchakato wa igunga tangu kujiuzulu kwa rostam, nawajua wafuasi wa CCM na CDM. weakness ya CDM Igunga hakuna uongozi imara wa CDM, nasema hivyo kwasababu mwenyekiti wa wilaya Majimoto, Kashindye na Pili mnene (amekuwa mwenyekiti wa wanawake wa chadema wilaya tangu kujiuzulu kwa rostam kabla ya hapo alikuwa ccm) walikuwa wakala wa rostam uchaguzi wa 2010.

Majimoto alijitoa kugombea ubunge kwa kupewa fungu na rostam, Kashindye alteuliwa kuhamasisha kura za uraisi kwa jakaya kwa kauli mbiu aliyokuwa anawambia wanaigunga vijijini kuwa DR. SLAA ni fisadi wa mapenzi ili wanawake wasimpigie kura. Pili Mnene amejengewa nyumba na rostam na mpaka sasa anasomesha mtoto wake chuo kikuu. Mheshimiwa diwani wetu wa chadema kwenye vikao vya council anapokea posho anayotoa RA ili kuweza vikao vya madiwani vipitishe matakwa yake kwa remote wakati yeye anakula raha jijini.

Sasa kabla ya kupitisha mgombea wenu kesho mheshimiwa kashindye muhakikishe mmesafisha jambo hilo kwani walimu wote wanajuwa kuwa alikuwa kibaraka wa rostam kufanya kampeni za ccm 2010 sasa wapiga kura wenu watakuwa na imani nae vipi kwasababu wanamtambua kama CCM na kwataarifa nilizo nazo hadi sasa wamekorofishana na DC igunga kwa kuwa wanajuwa kilichofanyika mwaka jana. Na siku chache baada ya kujiuzulu RA, Bashe alivyokuja igunga alimtumia Kashindye kuwapelekea wenyeviti wa kata salamu kutoka kwa rostam na kuwajulisha kuwa yupo nao pamoja fungu alilopewa alimficha boss wake DC na badala yake akatumia gari la ukaguzi na mafuta ya serikali bila kumgawia boss wake fungu.

TUPO NJIA PANDA wanaigunga kwa maana kwamba tutapata bora mbunge kwa maslahi yake mbunge na kuongeza fungu la posho kwenye chama au tunapata mbunge ili kuweza kuwatumikia wanaigunga? NITOE NJIA PANDA KESHO
Dah,ni balaa kama hali yenyewe ndo iko hivi kweli,....
Ila sidhani kama ushauri wako utafanyiwa kazi hapa,ungesifia ungepata "likes"
kama 100 hivi
 
Nyie mnaolazimisha CDM iungane na CUF kwanini CUF wasiungane na CCM halafu mtuambie ni wapi wapinzani waliungana wakashinda,
kama ni kugawana kura hata CCM itagawana na CUF maana CDM wanaenda bila kuwa na kura hata moja, ngoja niwape mahesabu yatavyokuwa,

Uchaguzi uliopita CCM walipa kura 35,000 safari hii watapata nusu ya hizo nusu iliyobaki itakwenda Chadema yaani 17,500.
CUF walipata kura 11,000 safari hii hata nusu yake hawapati basi tuwape nusu 5,500 na nusu iliyobaki itakwenda Chadema yaani 5,500.
Final results
Chadema kura 17,500 + 5,500 = 23,000.
CCM kura 35,000/2 = 17,500.
CUF kura 11,000/2 = 5,500.

Yes,...
Unapo ingia vitani ni vyema kuingia na mentality ya "lazima tushinde"
ila tunao waangalia tunajua nani ananguvu ya zana za vita na nani
ana nguvu ya maneno
 
chadema wanayo nafasi ya kushinda ila wako mtegoni mpaka sasa, CUF msijisumbue sana bora muwaunge mkono ccm kwani Dr. Kafumu ameyavulia nguo maji na hana budi kuyaoga mpaka ameacha budget ya wizara yake haijapita yupo kwenye mchakato. DANGER, mzimu wa rostam unasumbua igunga bado.

I love this about JF,kila anae leta argument kuhusu chadema
huyo ni mwana CCM,CUF etc,.....mimi ni mwanachama na shabiki wa TANZANIA
sina chama chochote!!!
 
..ndivyo inavoelekea kuwa,ktk mazingira haya ya utawala wa ccm, wapo watu wa kuwaamini but si watu wa caribre ya Kashindye, ccm wanaweza kutumia fedha kununua madiwani zaidi ya sita sembuse mtu mmoja tena mwajiriwa wa serikali wanayoiongoza..!lini ccm wameanza siasa za ustaarabu..? wanayo karata moja tu karata waliyobaki nayo sasa KUNUNUA WAGOMBEA NA KUWAFANYA MAMLUKI..!hawana uwezo wa kushinda uchaguzi kwa hoja! hata wakeshe majukwaani!

Hivi mnawajua waratibu kata wa vijijini nyie? na jinsi wanavyopata hizo nafasi..? kwa anejua Bw. Kasindye is not a person to trust as a material candidate! labda CHADEMA wakiamua kusindikiza uchaguzi wa lgunga

Si mara zote kuwa mtu aweza nunuliwa. Kumbuka hata katika miji ya sodoma na gomora historia inatuambia kuwa bado kulikuwako na manti wenye bikra! Yawezekana ikawa Kashindye ndiye mfano wa hao manti wa enzi hizo za Sodoma na Gomora. Ila ni vizuri kuliweka hilo kama angalizo ilikupunguza risk ya hayo kutokea.
 
Speaker
Comments zako ni interesting. Namkumbuka Maggid Mjengwa. Naye alitabiri kuwa Chadema ingeibuka ya tatu kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana based on historical evidence...za nguvu ya kafu na ushindi wao wa huko nyuma. You know what happened.

Utabiri wako, kama wa Maggid, unaacha some important variables in the model.
 
Siasa za vitabuni. Njoo field uone.Picha zimepigwa nyingi tu kwa bahati mbaya hatujakaa in a position ya kuzirusha zitarushwa tu wakati ukifika. Assumption kwenye siasa sio mahali pake.

Tunaruhusiwa kuassume kwenye maths,physics na mambo mengine yanayofanana a calculations ila game hili lasiasa sio kabisa. Inavyoelekea umeanza mwaka Jana kufuatilia siasa ndio maana hata hujui record ya CHADEMA kwenye chaguzi ndogo za Biharamulo, Busanda na Mbeya Vijijini na nguvu ya CUF kwa kutumia mataokeo ya uchaguzi mkuu wa nyuma yake.

Uwe unasoma before you post men!
Mara nyingi retreat is not Ignorance na sio sign ya weakness,...Hata kwenye movies tunaona ili umshinde adui lazima sometimes u-salende kwenye kambi yakethen from ndani ndo utajua jinsi ya kupigana nao.Chadema haina nguvu Igunga,sikatai kwamba wasisimamishe mgombea maana wakisimamisha ndo itakua mwanzo wa chadema kuanza kufahamika vyema huko.Lakini ukweli ni kwamba chadema kushinda Igunga kwenye huu uchaguzi mdogo ni sawa na ngamia kupita kwenye tundu la sindano ila kushiriki kwao Igunga ni maandalizimazuri ya 2015.Kama ni kweli chadema inakubalika Igunga kama alivosema sis.Regia na "mamia" waliwapokeabasi usingekawia kuona picha hapa,....trust me.Anyway,i wish them the best katika maandalizi ya 2015 sio saivi,.....i still stand on my bet kwamba chadema will rank number 3 kwenye huo uchaguzinyuma ya CCM na CUF,......Lets be realistic kidogo
 
Speaker
Comments zako ni interesting. Namkumbuka Maggid Mjengwa. Naye alitabiri kuwa Chadema ingeibuka ya tatu kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana based on historical evidence...za nguvu ya kafu na ushindi wao wa huko nyuma. You know what happened.

Utabiri wako, kama wa Maggid, unaacha some important variables in the model.

Okey,...
siidharau chadema,na sijawahi ila nachosema ni facts kabisa, kwamba wanaenda Igunga sio kwa ajili ya kushinda, ila kwa ajili ya kukijienga chama maana ni opportunity imepatikana na lazima waitumie
(that is good kwa chama chochote cha siasa, nashangaa kwanini NCCR na wengine hawajatangaza nia ya kusimamisha wagombea so far)

Ila ninacho tofautina na maono ya wengi hapa, ni kama naonekana nawavuta shati wasiende
na nguvu na imani ya kushinda, ila ni vyema kuwa realistic "hata kama siasa ni lazima useme nitashinda tu"

Hakuna jinsi chadema itashinda Igunga, ila wana nafasi nzuri sana kujijenga sasa Tabora nzima na 2015
wakisimamisha watu wasio kua mamluki watashinda majimbo mengi sana
 
@ chadema ,Cuf na CCM

Je, wamejipanga vipi kuhakikisha daftari la wapiga kura linamajina yote ya wahusika wa kupiga kura

hili zoezi lazima walifanye kabla ya siku hazijaisha na vilevile wahakiki kuwa hakuna majina yaliyoondolewa kimakosa kwani kwa habari za ndani ya vyama vingine wameweza kupata daftari hili sijui kinachoendelea
 
Speaker

vyama vingi vinapoteza ushindi katika chaguzi ndogo kwasababu ya mbinu na kutokuwa na mamlaka juu ya tume za uchaguzi, nadhani kuna vyama vyenye uwezo ata wa kumshinikiza muhusika wa daftari la wapiga kura kuondoa au kuongeza majina ya wapigakura (ghost voters)
 
CHADEMA must be counting their chicken before they hatch by inanely hoping to grab Igunga.
 
Mwl Joseph Mwandu Kashindye kuipeperusha bendera ya CHADEMA Igunga.Kamati Kuu imempitisha.Kila la heri Kamanda.

huyo kashidye tumesoma mambo yake humu ndani sio mazuri,chadema msipende mambo ya kulipua maadam mshinde
kuweni makini jamani
 
@speaker

vyama vingi vinapoteza ushindi katika chaguzi ndogo kwasababu ya mbinu na kutokuwa na mamlaka juu ya tume za uchaguzi, nadhani kuna vyama vyenye uwezo ata wa kumshinikiza muhusika wa daftari la wapiga kura kuondoa au kuongeza majina ya wapigakura(ghost voters)

Mkuu,
hawa watu wanaharibu kwa kukosa maarifa.
haiwezekani unajua kabisa swali flani formula yake ni xxxx alafu unaingia
kwenye mtihani bila kuifanyia kazi hiyo formula,.....
ukifeli una lalamika kuonewa na mwalimu.
 
Ahsante kwa taarifa mpiganaji wetu.zingatieni kua magamba ni wazuri sn katika rafu na rushwa katika uchaguzi
na ni vema mkumbuke kua cuf hawaipendi cdm na wapo tayari kuwasaport ilimradi cdm ikose ushindi.
Hivyo nashauri makamanda muwe makini na mumtumie sn huyo diwani wetu wa hapo igunga.

Kumbuka kilachama kilichopo Igunga kinatafuta ushindi na si kimpende nani wala kumchukia nani mbona Chadema wanafanya kampeni chafu ya kuichafua CUF igunga.Je chadema wanaipenda CUF?.Mahona wa CUF anaungwa mkono sanaaaa.
 
Mkuu,
hawa watu wanaharibu kwa kukosa maarifa.
haiwezekani unajua kabisa swali flani formula yake ni xxxx alafu unaingia
kwenye mtihani bila kuifanyia kazi hiyo formula,.....
ukifeli una lalamika kuonewa na mwalimu.

vyama vingi vimeweza kuweka vitengo mbali mbali lakini tatizo ni kuwa hakuna chama chochote katika Tanzania walioweka kamati ya uchaguzi ambayo ni endelevu wakati wote, vingi vinaunda kitendo hiki kwenye chaguzi tu, na hili ni kosa kubwa litaloendelea kuvigharimu vyama vya siasa.

chama chochote kinachohitaji ushindi ni lazima kiwe na kitengo kinachoshughulika na uchakuzi siku zote na kiwe macho wakati wote na kifanye tathmini wakati wote na tafiti maeneo yote ili chama kijue kwanini kimeshinda jimbo fulani na kwanini kimepoteza jimbo fulani


ukifanya uchunguzi kwanini umepoteza jimbo ukaacha kwanini umeshinda jimbo fulani basi umepoteza 50% ya mipango ya baadae
 
Naona kuna kila dalili za kushinda uchgauzi huko na pia kuna ulazima wa kufanya tunafanya vizuri sana katika siasa za huko dada na pia tunawaomba sana wanannchi wa Igunga kufanya badadiliko maan waliuziwa mbuzi kwenye gunia na sasa wanaweza kufanya vizuri wa kuchagua CHADEMA
 
Du unataka mpaka alie muonee huruma bas coz mmewe nape kazibwa domo. Hongeren tuko nyuma
 
Back
Top Bottom